Thursday, July 13, 2017

Yanbian v Shanghai SIPG

Baada ya kupata matokeo mabovu juma lililopita dhidi ya changchun Yatai. Na kukosa nafasi ya kuongoza ligi kuu ya China. Juma hili wanaingia uwanja wakiwa na mastaa wao (Hulk na Wu Lei) pamoja na Kocha mkuu Andre-Villas Boas ambao walikuwa wamefungiwa mechi mbili kila mmoja 
Wata kuwa wageni wa Yanbian Wanaoshikilia mkia wa Ligi kuu ya China na wakiwa na lengo la kushinda na Kuongoza ligi

Yanbian wamekuwa na kiwango kibovu msimu huu
Wakiwa wamekosa ushindi katika ligi kuu kwenye mechi 9 zilizopita
Hapa watawakaribisha Shanghai SIPG katika uwanja wao wa nyumbani PEOPLE'S STADIUM

Hapa naona Shanghai SIPG wakipata ushindi wa zaidi ya Goli 2 na kushika na kuongoza Ligi hiyo
Mechi itachezwa jumamosi
Majira ya 10:30 asubuhi kwa huku kwetu

Ubashiri
Shanghai SIPG
Asian handicap 1.0
Odds 1.96 @meridianbet


Matokeo:
Yanbian 1-3 Shanghai SIPG

Mkeka umeshinda..

Wednesday, July 12, 2017

Huu Ndio Utajiri Mkubwa Utakaoupata, Kama Utaamua Kufanya Biashara Hii

MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani.

Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.

Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.

Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira, ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

TAKUKURU: Kurudisha Hela Hakukuondoi Kwenye Tuhuma, Sheria Kufuata Mkondo Wake


JF Jana  Wali- tweet kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa au TAKUKURU kwa kifupi imesema kuwa mtu kurudisha hela aliyopewa iliyotokana na ufisadi au utakatishaji pesa hakumuondoi kwenye mashitaka.

Mnakumbuka jana Ngeleja alirudisha hela aliyopewa na Rugemalira kwa madai kwamba hakujua kuwa hela hiyo inatokana na ufisadi.

Imevuja: Yanga Kumsajili Erasto Nyoni

KIUNGO anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi, Erasto Edward Nyoni yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa Tanzania, Yanga baada ya kumaliza mkataba wake Azam FC

Nyoni yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa kwa mchezo na Rwanda Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee – na Yanga wanatarajia kumalizana naye kabisa baada ya mechi hiyo.

“Mazungumzo na Nyoni yamekwenda vizuri na wakati wowote tunaweza kumalizana naye, pengine baada ya mechi tu dhidi ya Rwanda,”kimesema chanzo kutoka Yanga.

Benchi la Ufundi la Yanga, chini ya Kocha Mkuu, Mzambia George Lwandamina kwa kushirikiana na Sekretarieti chini ya Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha kwa pamoja wamejiridhisha Nyoni ni mchezaji ambaye wanamuhitaji kikosini.

Na hiyo ni kwa sababu huyo ni ‘kiraka’ anayeweza kucheza nafasi yoyote ya ulinzi kuanzia kiungo wa ulinzi – lakini uzoefu na weledi wake kisoka ni vitu vingine vinavyomuunganisha na Yanga katika siku za mwishoni za maisha yake ya uwanjani

Everton inafungulia Milango Tanzania - Mwakyembe

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema ujio wa timu ya Everton nchini utaweza kufungua fursa nyingi kwa kuwa dunia nzima sasa itaitazama Tanzania kupitia mchezo kirafiki dhidi ya Gor Mahia.


Mwakyembe amebainisha hayo muda mchache alipoupokea ugeni huo huku akizisisitizia timu za Tanzania kutumia viwanja vilivyopo nchini vizuri ili waweze kuinua vipaji kwa hali ya juu.
"Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kwanza kuwaona hawa nyota wa Everton ni timu kongwe kutoka Uingereza lakini pili inafungua fursa sana maana inatutangaza watanzania kidunia, wamekuja na watangazaji kutoka nchi mbalimbali. Kwa hiyo inafungua milango kwa timu nyingi zaidi, nasi tuzishawishi zaidi timu zetu zije kutumia viwanja vyetu vya kisasa tulivyo navyo", amesema Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Mwakyembe amewatuliza wanahabari pamoja na wapenzi wa soka kuwa na moyo wa uvumilivu kwa kuwa hawataweza kupata nafasi ya kukiona kikosi hicho kikiwa kinafanya mazoezi yake kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kutokana na kuwepo na ulinzi mkali.

"Nafikiri kesho kutakuwa na mchezo mzuri kweli, leo watafanya mazoezi katika uwanja Taifa lakini naona wenzetu hawataki kabisa kuona vyombo vya habari pale, hatuwezi kuwapinga kwa hilo. Kwa hiyo vijana wangu msihangaike hata kwenda pale maana kuna ulinzi mkali lakini kesho nitahakikisha kila mmoja wenu anapata nafasi nzuri kuweza kufuatilia mchezo huo jioni", amesisitiza Mwakyembe.

Everton itashuka dimbani kesho (Alhamis) kuchapana na Gor Mahia mchezo wa kirafiki baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa michuano ya Sportpesa Super Cup 2017

Duh.. Afande Sele Amuombea Mabaya Aliyekuwa Rais wa TFF...Acha Magufuli Awanyooshe

Msanii mkongwe wa Hip hop nchini Afande Sele amefunguka na kumuombea mabaya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi na kusema ni bora aende kwani katika kipindi chake hakuna jambo lolote la maendeleo amelifanya.

Afande Sele ametumia ukurasa wake wa facebook na kusema yake ya moyoni kwa kulinganisha ofisi na hatua ambazo zimepigwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Sudan na kusema Malinzi anapaswa kuondoka tu kwani ni aibu.

"Ofisi ya chama cha soka cha Sudan na ofisi ya chama cha soka Tanzania..aibu yetu..acha Magufuli atunyooshe tu kwani tulizidisha uwendawazimu. Nenda Malinzi nenda tuuu" alisisitiza Afande Sele

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanagombea nafasi ya Urais katika shirikisho hilo lakini jina lake lilienguliwa katika mchakato huo baada ya kushindwa kuhudhuria katika usaili wa wagombea uliofanyika siku ambayo yeye yupo rumande kutokana na kesi inayomkabili ya matumizi mabaya ya ofisi.

KIMENUKA...CUF ya Lipumba Yatangaza Vita Kwa Chadema.....

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Bara anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Magdalena Sakaya, amejibu mapigo baada ya mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kutangaza jana ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’. Kubenea amedai kuwa oparesheni hiyo inalenga kumuondoa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Akijibu mpango huo uliotangazwa na Chadema inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Sakaya ambaye ni kambi ya Profesa Lipumba alisema kuwa anawasikitikia Chadema kwa kuingilia mgogoro usiowahusu.

Sakaya ameongeza kuwa Mpango huo wa Chadema hautafanikiwa kamwe na kwamba wanachokifanya ni Kuingilia mambo yasiyowahusu.

Katika hatua nyingine, Kubenea alipozungumzia majibu ya Sakaya amedai kuwa CUF ni sehemu ya Ukawa, hivyo inapoonekana inataka kudhoofishwa ina maana kuwa Ukawa itadhoofika pia, hivyo hawako tayari kuliona hilo

Sunday, December 4, 2016

Mchezaji wa Mbao FC U 20, Ismail Mrisho afariki uwanjani


Kinda wa Mbao FC ya Mwanza, Ismail Mrisho Khalfan amefariki dunia Jumapili ya jana baada ya kuanguka uwanjani alipogongana na beki wa Mwadui FC katika michuano ya Ligi ya Vijana U20 inayoendelea.
dv2a0262
Akiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka
Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na juhudi kubwa zilifanyika kuokoa maisha ya kinda huyo, lakini haikuwezekana.
mchezaji
Akitolewa nje baada ya kuanguka
“Inaonekana alishafariki dunia pale uwanjani, tulifanya juhudi kubwa mimi na wenzangu. Tulisaidiana na watu wengine pia waliokuwa uwanjani, lakini ilionekana hakukuwa na majibu mazuri,” alisema mmoja wa madaktari waliojaribu kuokoa maisha ya kijana huyo.
Mwenyezi Mungu Amrehemu.

Thursday, December 1, 2016

Mambo Yazidi Kuwa Magumu kwa Wadaiwa Bodi ya Mikopo, Sasa Kukatwa 15% ya Kipato Chao kwa Mwezi



MAMBO yanazidi kuwa magumu kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu baada ya asilimia ya marejesho ya mkopo huo kwa kila mwezi kuongezeka kutoka 8% hadi 15%.

Mabadiliko haya yamekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuwa tayari amekwishasaini mabadiliko ya sheria yanayomtaka mwajiri kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kulipa deni lake analodaiwa na Bodi ya Mikopo.


Hatua hii imekuja ikiwa wadaiwa hao tayari wamepewa siku 30 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul Razaq, aliyesema wadaiwa hao sugu watachukuliwa hatua kali iwapo hawatarejesha mikopo hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Katika maelezo yaliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoendeshwa kupitia mtandao wa facebook wa East Africa Television, Naibu Waziri Manyanya alisema sheria hiyo tayari imesainiwa na siku za hivi karibuni itaanza kutumika.

“Hii asilimia 15, kimsingi ninavyofahamu ilishasainiwa, baada ya hapo kuna kuiangalia iendane na kanuni zetu, baada ya kuicheki imeendana na kanuni zetu kama kuna sehemu itahitaji kuboreshwa kidogo haitazidi miezi miwili au mitatu, baada ya hapo tutaweza kutumia hiyo 15%, na asilimia 15 ya safari hii ni tofauti na siku za nyuma, siku za nyuma tulikuwa tunachaji asilimia 8”, alisema Manyanya.

Hapo awali wadaiwa hao wa mikopo walikuwa wanakatwa asilimia 8, lakini sheria ya sasa itaruhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kukatwa asilimia 15 ya kipato chao.

Pia Manyanya amesisitiza kuwa kwa wale ambao hawajaajiriwa, lakini wanafanya biashara zao wanatakiwa kuwasilisha angalau shilingi 120,000 kila mwezi na kuwashauri kuwa ni vema wakapeleka zaidi ili wamalize haraka madeni yao.

Kuhusu wasio na kazi, amesema haiwezekani mtu asome halafu akose shughuli ya kufanya na kuwataka kutafuta shughuli yoyote ya kufanya ili waanze mapema kulipa madeni yao ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu masomo.

TAHARUKI...Panya Road Wavamia Nyumba na Kupora..Majirani Washindwa Kusaidia



DAR: Kundi kubwa la vijana wanaosadikika kuwa ni 'Panya Road' wavamia nyumba moja na kupora vitu mbalimbali usiku wa kuamkia leo.

Inadaiwa kuwa mhanga wa tukio hilo alijaribu kuomba msaada kwa majirani bila mafanikio kwakuwa majirani hao waliogopa kutoka na kupambana na Panya Road hao.

Mmoja wa majirani amenukuliwa akisema kuwa Vijana hao walikuwa na Mapanga Marungu, Jambia na Baruti walizokuwa wakizilipua ili kutisha watu kuwa ni Risasi.

KWA Hili Lady Jaydee na Clouds Media Group Wanastahili Pongezi


Najua hakuna aliyetarajia kuona hili likitokea lakini kwa uwezo wa Mungu limefikia mwisho.

Nakumbuka Machi 21 ya mwaka huu kaka yangu Fredrick Bundala aliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari kinachosomeka “Ninachotamani: Lady Jaydee na Clouds Media Group wamalize tofauti zao” hatimaye hilo limesikika na kila kitu kimeonekana kuwa sawa kutokana na pande zote mbili kuamua kufukia mabaya yote yale yaliyowahi kutokea.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, napenda kumpongeza Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa busara yake aliyoitumia ya kujibu swali aliloulizwa kwenye kipindi cha XXL kuhusu kumaliza ugomvi wao na malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Jaydee.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema Ruge kwenye kipindi hicho.

Aliongeza kwa kusema kuwa ni muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo alidai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Hatimaye ujumbe ule ulimfikia Jaydee na nampongeza hakutaka kuliacha jambo hilo lipite kwa kuwa limedumu kwa muda mrefu na hakuna jipya lililotokea kwa kuwa kila mtu bado anafanya kazi zake huku mashabiki ndio wakibaki njia panda wakishindwa cha kufanya.

Jumatano hii uongozi wa Jide ulitoa taarifa yake rasmi kuwa wapo tayari kufanya kazi tena na kituo hicho cha redio. “Hatuna tatizo na Clouds Media Group kuanza kupiga nyimbo za Lady Jaydee. Wanaweza kuanza kupiga wakati wowote watakapokuwa tayari kwakuwa chochote kilichotokea hapo nyuma kimefikia tamati, la msingi sasa ni amani na upendo vitawale. Kuanzia leo wana uhuru wa kupiga na kutaja jina la Lady Jaydee kadri wawezavyo,” yalisema maelezo yake.

Kitendo hicho kilichofanywa na pande zote mbili kitawarudisha upya tena baadhi ya mashabiki waliogawana upande pamoja na kuwapa nafasi wasanii ambao walikuwa wakitamani kufanya kazi na Jide kwa muda mrefu lakini walikuwa wakihofia nyimbo zao kutochezwa kwenye kituo hicho.

Kama hili limewezekana basi natamani pia kuona siku moja wasanii wengine ambao hawapatani na kituo hicho na vituo vingine vya habari wakiyamaliza matatizo yao na kuendelea kuufanya muziki wetu kusonga mbele kwa kuwa wote tupo kwenye safari moja na kila mtu anamtegemea mwenzake ili kuhakikisha hilo linatimia.

By Salum Kaorata

MWAMVITA Makamba Atapeliwa na Sheria Ngowi......


Katika pitapita zangu Twitter nimekumbana na Tweet moja ya Mwanadada Mwamvita Makamba akidai yeye kama Mwekezaji binafsi katika tasnia ya Fashion ametapeliwa na Mbunifu wa Suti matata Bwana Sheria Ngowi.

Hapo alikuwa akimpa taarifa jamaa anayeendesha kipindi kipya mjini cha Papo Kwa Papo na Papi kinachoruka kila jumatano saa 3 kamili usiku kupitia YouTube na kinakuwa Mubashara.

HATIMAYE Rolls Royce la Diamond Liko Njiani Kuja Tanzania.....


The Rolls Royce musician from east africa aka diamond hatimaye amekamilisha ndoto zake za siku nyingi baada ya order yake ya gari aina ya rolls royce kukamilia na gari hilo liko njiani kuwasili mikononi mwake punde... Gari hilo aina ya rolls royce Drop Head coupe 6.7 litre V-12 ambalo limeagizwa kupitia kampuni ya Newline Luxury Motors ambalo order yake ina waiting time ya six months kuanzia unapolipia hadi litengenezwe hadi likufikie mteja..

Post Labels