
Na Mahmoud Rajab
“Hatuwezi kushindana au kwashinda washindani wetu ambao wana pesa
nyingi kuliko sisi. Tunapaswa kuwa makiini sana, kufanya machaguo
sahihi.”Hayo nia aina ya maneno ambayo kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa
wakisikia kutoka kwa kocha na viongozi wao juu ya wapinzani wao. Ni
Arsenal wenyewe kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wao Ivan Gazidis
waliwaaminisha washabiki wa wapenzi wao kwamba, klabu ina akiba ya kiasi
cha paundi mil 200 kwaajili ya usajili, hivyo wana uwezo wa kuleta
mchezaji yeyote.
Bila kupepesa macho ni ukweli kwamba, Arsene Wenger ndiyo meneja bora
tangu Herbert Chapman na ataacha historia kubwa pale atakapoondoka.
Miaka ishirini ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mfululizo yanabaki kuwa
mafanikio makubwa kwake na klabu, makombe matatu ya Ligi ya England na
sita ya FA bila kusahau kumaliza msimu wa ligi bila kupoteza mchezo ni
jambo la kujivunia sana.
Hata hivyo, licha ya mambo yote hayo niliyotaja hapo juu ambayo ni ya
kujivunia kwa klabu hiyo, Arsenal hawajatwaa taji la Ligi ya England
kwa miaka 12 sasa, hawajavuka hatua ya 16 bora kwenye Uefa kwa miaka
sita mfululizo na kuwa klabu pekee kwenye ligi kubwa tano Ulaya
kutosajili mchezaji wa ndani kwenye dirisha usajili lililopita licha ya
kuwa na uhitaji wa wachezaji.
Mwanzoni mwa dirisha hili alianza kuwahadaa washabiki na wapenzi wa
Arsenal. Pengine alikuwa kocha wa kwanza miongoni mwa makocha wa vilabu
vikubwa barani Ulaya kuanza kusajili baada ya kumsajili kiungo Granit
Xhaka kutoka Borussia Monchengladbach kwa ada ya paundi mil 35, kabla ya
kumuongeza kinda wa Kijapan Takuma Asano, beki Rob Holding (20) na
kinda wa Kinigeria Kelechi Nwakali (18). Na kwa namna inavyoonekana ni
wachezaji Xhaka na Holding pekee ndio watakaokuwa kwenye kikosi cha
kwanza msimu huu, huku Asano and Nwakali wakisubiri vibali vyao kwaajili
ya kutolewa kwa mkopo kwa ili kupata uzoefu zaidi.
“Inabidi tufuate gharama zinazolipwa na watu wengine,” hivi karibuni
Wenger alisema. “Bei zimekuwa juu sana kwasababu upatikanaji wa pesa uko
juu sana. Na ndiyo maana unaona sasa tumevuka mpaka paundi mil 100 kwa
usajili wa mchezaji mmoja tu.
“Tunataka kutumia pesa tulizonazo,” aliongeza. “Lakini tunaheshimu
pia pesa tulizonazo, ni vigumu sana kupata wachezaji wenye ubora halisi
kwenye soko la sasa. Licha ya uwepo wa pesa nyingi sana hapa England
lakini bado utaona watu wanafanya usajili taratibu sana.
Hayo ndiyo maneno ya Arsene Wenger ambayo kila siku amekuwa
akiyasema. Arsenal wanahitaji nini hasa? Wanahitaji beki wa kati mwenye
uzoefu wa kutosha kusaidiana na Per Mertesacker, Laurent Koscielny
pamoja na Gabriel Paulista. Wanahitaji mshambuliaji mwingine wa
kusaidiana na Olivier Giroud. Giroud tayari ameshidndwa kuonesh kila
ambacho wenzake kama Thierry Henry na Robin van Persie walionesha katika
nyakati zao.
Ikumbukwe kwamba nyuma ya Giroud kuna fundi wa pasi Mesut Ozil ambaye
msimu uliopita aliweka rekodi ya kutengeneza nafasi nyingi ikiwa ni
pamoja na pasi za magoli. Sasa ili Ozil azidi kufanya kile
wanachotarajia watu wengi, inahitajika straika mwingine wa kumpa
changamoto Olivier Giroud na kutoa upinzani mkubwa kwa timu nyingine.
Kwa sasa Per Mertesacker and Gabriel Paulista watakuwa nje kutokana
na kusumbuliwa na majeraha. Hii sasa imemlaziku Wenger kutoka kwenda
kutafuta mbadala ambaye atazidi pengo hilo, na taarifa zilizopo zinadai
kwamba Shkodran Mustafi anatajwa kumalizana na klabu hiyo hivi karibuni.
Huyu walau atakuwa msaada mkubwa kutokana na ubora na uwezo wake wa
kusoma mchezo, kitu ambacho Arsenal inahitaji kwa kiasi kikubwa kwa
sasa.
Lakini wasiwasi unabaki kwamba, Je, Wenger ataleta mshambuliaji?
Kushindikana kwa uhamisho wa Jamie Vardy na kuamua kubaki Leicester na
kukataliwa kwa ofa yao ya kwanza ya paundi mil 29 na Lyon juu ya
mshambuliaji Alexandre Lacazette ni mifano ya hai ya changamoto
anayokumbana nayo Arsene Wenger kwenye nafasi ya ushambuliaji.
Siku 16, michezo mitano, nchi nne, magoli 17 ya kufunga na matano y
kufungwa. Arsenal wamemaliza kwa namna hiyo msimu wao wa pre-season
kufuatia safari zao kwenye nchi za Ufaransa, Marekani, Norway na Sweden.
Walihitimisha mechi yao ya mwisho kwa ushindi mujarab wa magoli 3-2
dhidi ya Manchester City. Wameonekana kuimarika kwa kadri walivyozidi
kucheza mechi zao za kirafiki.
Chuba Akpom ameonesha kuimarika baada ya kufunga kwenye michezo minne
mfululizo. Ilielezwa kwamba angeweza kuanzishwa kwenye mchezo dhidi ya
Liverpool lakini kiwango kizuri cha Walcott kwenye mechi mbili dhidi ya
Viking FK na Manchester City kunaweza kusababisha aanze badala ya Akpom.
Hata hivyo kwa jinsi hali ilivyo bado anahitajika straika mwingine
mwenye ‘killer instincts’, Akpom bado hana uzoefu wa kutosha.
Ujio wa makocha kama Pep Guardiola, Jose Mourinho na Antonio Conte,
jumlisha usajili wa wachezaji kama Zlatan Ibrahimovic, Paul Pogba, Ilkay
Gundogan na N’Golo Kante, Arsenal watakuwa na kibarua kigumu sana msimu
huu kwenye mbio za kuwania taji la EPL. Kwenye mchezo dhidi ya
Liverpool watakuwa na wasiwasi mkubwa pale safu yao ya ulinzi
itakapokuwa chini ya makinda wasio na uzoefu Rob Holding and Calum
Chambers, huku mapema kabisa wakianza kuandamwa na mkosi wa majeruhi.
Kuna wasiwasi wa utimamu wa Santi Cazorla ambaye ametoka kuuguza
majeraha yake ya goti bila kusahau spana mkononi Jack Wilshere ambaue
pamoja na kutocheza kwa muda mrefu, majeraha yamekuwa sehemu ya maisha
yake na sasa anasumbuliwa na maumivu ya goti.
Msimu huu ambao unaonekana kuwa na ushindani mkubwa zaidi kuwahi
kutokea baada ya kipindi kirefu, unaweza kushuhudia Arsenal wakiangukia
pabaya zaidi kama hawataenda na upepo unavyotaka. Bado kuna muda mwingi
tu wa usajili, na kama Arsene Wenger akiendelea kubania pesa za usajili
ama hakika anaweza kuandika historia mpya, huku akiwa anaelekea ukingoni
mwa mkataba wake