Kiungo
mpya wa Manchester United Paul Pogba amesimamishwa kuitumikia timu yake
kwa mchezo wa kwanza wa Premier League, chama cha soka cha England
kimethibitisha.
Pogba, 23, alirejea Old Trafford kutoka Juventus kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya £89.3 million, miaka 4 baada ya kuhamia klabu ya Turin kwa ada ya £800,000 kufuatia kukosa muda wa kucheza na mgogoro wa mkataba mpya.

Hata
hivyo Pogba itambidi asubiri mpaka wiki ijayo kucheza mchezo wake wa
kwanza na klabu yake mpya kwa sababu amefungiwa kucheza mchezo wa
Jumapili dhidi ya Bournemouth.
Kiungo
huyo wa Ufaransa amesimamishwa kwa kosa la kupata kadi mbili za njano
katika msimu uliopita wa mashindano ya Coppa Italia, na adhabu yake
imehamia katika michezo inayosimamiwa na Chama cha soka cha England.
Post a Comment Blogger Facebook