JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeumarisha ulinzi kipindi chote cha sikukuu ya Idd Elfitry ili wananchi washerekea kwa amani na utulivu. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).
Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Kanda hiyo Seleiman Kova alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuwaondolea wananchi wasiwasi.
Kova amesema jeshi limeweka mikakati mbali mbali ya kukubaliana na uhalifu unaojitokeza kipindi cha sikukuu ikiwa pamoja na kushikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama
Amesema kuwa wamepanga kutumia kikosi maalumu cha intellijinsia,Kikosi Kutuliza ghasia (FFU),Askari wa mbwa na farasi na doria za askari wa miguu na pikipiki ili kuzuia matukio au mipango ya kufanya matukio ya uvunjifu wa amani.
Aidha, amesema ulinzi utaimarishwa sehemu za kufanyia ibada ,kumbi za starehe,fukwe za bahari na kuzitaka familia kutotelekeza makazi yao bila kuacha ulinzi.
Ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi wasiwache watoto wao wakiogelea katika fukwe bila uangalizi wao huku akipiga marufu disco toto kwenye mkusanyiko mkubwa.
“Jeshi halita vumilia aina yoyote ya uhalifu au majaribio ya matukio ya uvunjifu wa amani na jeshi litapambana na watu ambao wanatumia siku hizi za siku kuu kama siku za kufanya uhalifu na wale wanywaji wa pombe wasinywe kupitiliza ni hatari” amesema Kova
Amesema wananchi watoe taarifa wakihisi uvunjifu wa amani na matukio kupitia namba zifutazo RPC Ilala :Lucas Mkondya 0715009980 ,RPC Temeke :Andrew Satta 071500979 na RPC Kinondoni Camilius Wambura 0715009976.
Hata hivyo amesisitiza jeshi linaendelea na msako mkali kufuatia tukio la kuuawa kwa askari wanne na raia watatu lilotokea katika kituo cha Polisi Sitakishari na raia watatu wiki hii.

Post a Comment Blogger Facebook