0
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya GeoPoll ya Marekani ambayo ina ofisi jijini Nairobi Kenya, Clouds TV na ITV ni vituo vya runinga vinavyoangaliwa zaidi nchini.


Utafiti huo ni kuanzia April 1 hadi June 30 mwaka huu.

Clouds TV inaongoza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi wafikao asilimia 19.11% ya watazamaji wote wa runinga ikifuatiwa na ITV yenye 18.32% na EATV yenye 18.20%.


Utafiti huo umeonesha kuwa ITV hutazamwa zaidi kuanzia saa 2:00 hadi 2:30 usiku kwenye taarifa yake ya habari huku Star TV na TBC1 zikiwa na watazamaji kiasi kati ya 1:30 jioni hadi 2:30 usiku.


EATV pia hupata wazamaji wengi kuanzia 2:30 hadi saa 3:30 usiku.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top