0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Bara anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Magdalena Sakaya, amejibu mapigo baada ya mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kutangaza jana ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’. Kubenea amedai kuwa oparesheni hiyo inalenga kumuondoa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Akijibu mpango huo uliotangazwa na Chadema inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Sakaya ambaye ni kambi ya Profesa Lipumba alisema kuwa anawasikitikia Chadema kwa kuingilia mgogoro usiowahusu.

Sakaya ameongeza kuwa Mpango huo wa Chadema hautafanikiwa kamwe na kwamba wanachokifanya ni Kuingilia mambo yasiyowahusu.

Katika hatua nyingine, Kubenea alipozungumzia majibu ya Sakaya amedai kuwa CUF ni sehemu ya Ukawa, hivyo inapoonekana inataka kudhoofishwa ina maana kuwa Ukawa itadhoofika pia, hivyo hawako tayari kuliona hilo

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top