Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Monday, February 8, 2016

korea kaskazini yarusha kombora la masafa marefu

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea Kaskazini kurusha Kombora la masafa marefu.

Umoja wa Mataifa umesema wamekubaliana kuiwekea nchini hiyo vikwazo vya kiuchumi mapema iwezekanavyo

Lakini pia baraza hilo limeilaumu Korea Kaskazini kwa kukiuka maazimio ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kulipua bomu la nyuklia mwezi Januari.

Kauli hizo za kuilaani hatua hiyo ya Korea Kaskazini zimetolewa maeneo mbalimbali duniani pamoja na kulaumiwa na dunia, Korea Kaskani yenyewe imesema imelipua kombora hilo ili kutuma mitambo ya satellite angani,jambo linalopingwa na mahasimu wake kuwa hiyo ni danganya toto kwani ina nia ya kujaribu kombora angani.

Akitoa taarifa ya kulaani hatua hiyo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambaye pia ni Balozi wa Venezuela Rafael Ramirez Carreno amesema wanachama wamekubaliana kulaani kile alichosema ukiukwaji Korea Kaskazini wa azimio la Umoja

Monday, September 21, 2015

RAIS KENYATTA: HATUWEZI KULIPA WALIMU

Wakati shule zote za serikali na za binafsi nchini Kenya zikianza kufungwa kuanzia hii leo, rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali yake haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Ametoa wito kuwa, mgogoro huo utatuliwe kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo. Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu nchi nzima ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za serikali na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi majumbani mwao. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.

Mlanguzi Mkuu wa Madawa ya Kulevya Aliyetoroka Jela Akamatwa Huko Brazil....

brazil (2)Mlanguzi mkuu wa madawa ya kulevya Brazil, Mario Sergio Machado Nunes 'O Goiano'  akiwa mikononi mwa wanausalama.brazil (3)Mario Sergio Machado Nunes akiwa chini ya ulinzibrazil (1)
WANAUSALAMA nchini Brazil wamemtia mbaroni mmoja wa walanguzi wakubwa wa madawa ya kulevya nchini humo.
Mario Sergio Machado Nunes, ambaye pia anafahamika kama 'O Goiano' amekuwa mafichoni tangu atoroke jela miaka miwili iliyopita.
Polisi wanasema kuwa alifanyiwa upasuaji ili kubadili umbo lake na alikuwa akitumia stakabadhi bandia.
Mnamo miaka ya themanini, O Goiano alikuwa kati ya watu wachache waliokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na aliyekuwa mlanguzi maarufu wa madawa ya kulevya raia wa Colombia, Pablo Escobar.
Amekuwa akisafirisha madawa ya kulevya kati ya Marekani Kusini na Afrika.
O Goiano alikamatwa akiwa katika jumba moja la kifahari katika mji wa pwani wa Guajura.
Hapo jana, maafisa wa kupambana na mihadarati walitangaza kiinua mgongo cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayetoa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa kiongozi wa genge la wauazaji mihadarati Joaquin Chapo Guzman ambaye kama Goiano alitoroka gerezani.

Monday, August 24, 2015

Wahamiaji 2000 waokolewa Mediterranea


Walinzi wa italia wanasema kuwa takriban wahamiaji 3,000 wako mashakani
Walinzi wa pwani wa Utaliano wanasema kuwa waliaongoza shughuli za kuwaokoa wahamiaji 2,000 hivi ambao walituma ishara ya kuwa taabani kwenye mashua nje ya pwani ya Libya. Mashua kadha zinashiriki katika uokozi.
Mashua kama 18 za raba na mashua nyengine zilizojaa wahamiaji zimetuma ujumbe kwamba ziko mashakani.
Bahari baina ya Libya na Utaliano, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu, na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia Ulaya.
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja wa mataifa unasema kuwa bahari ya Mediterranea ndio kivukio maarufu.

Kufikia sasa takriban watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia .
Manuari ya Kijeshi ya Norway ilikuwa imewaokoa wahamiaji 320 jumamosi asubuhi


Sunday, August 23, 2015

KIMBUNGA CHAUA UFILIPINO

Waokoaji Kaskazini mwa Ufilipino wanachimbua ardhini kwa lengo kutafuta mamia ya wachimba madini, baada ya kukumbwa na kimbunga.
Zaidi ya watu kumi na tano wameripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo.
Mmomonyoko wa udongo ulisababishwa na kimbunga ambacho kilifukia migodi mitatu kaskazini mwa kisiwa cha Luzon.Kimbunga Goni kwa sasa kimepungua kasi na kinaelekea Japan katika kisiwa cha Ryukyu

Monday, August 17, 2015

MAMBO 10 MUHIMU YA KUEPUKA ILI KUEPUKANA ADHABU YA SHERIA YA MITANDAO TANZANIA (cyber crime)

Sheria ya mitandao inaanza kutumika rasmi tarehe 1 septemba 2015, haya mambo 10 muhimu ili sheria hii isikukamate
1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao
2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao
3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp,Facebook,Youtube,Instagram n.k
4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii
5. Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu ( kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu
6. Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu
7. Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu
8. Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu
9. Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini
10. Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu
Hukumu: Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika

SHEKAU ASEMA YU HAI


Kiongozi wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Nigeria, Boko Haram, amekanusha ripoti kwamba ameuwawa au kutolewa katika uongozi.

Katika rikodi ya sauti inayoaminiwa ni ya Abubakar Shekau, anaeleza kuwa ni uongo ripoti kwamba amefariki, amelemaa au ni mgonjwa.
Juma lilopita rais wa Chad, Idriss Deby, alisema kuwa Boko Haram imemteua kiongozi mpya na kuzusha tetesi kwamba Bwana Shekau ameuawa.
Ujumbe wake huo umewekwa katika mitandao ya kijamii na ulilengwa kwa kiongozi wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi.
Awali mwaka huu, Boko Haram ilitangaza kuwa ni tiifu kwa IS.

Sunday, August 16, 2015

Mtoto wa OSAMA BIN LADEN Aibuka..Atoa Ujumbe Mzito Kwa Marekani...Aagiza Mashambulizi

Kundi la kigaidi la A Qaeda limetoa ujumbe wa sauti ambao unadai kwamba umetoka kwa Hamza Bin Laden ,mwana wa Osama Bin Laden.

Ujumbe huo unaaminika kuwa wa kwanza wa propaganda za Al Qaeda kumshirikisha Hamza Bin Laden kama mwanachama wa kundi hilo.

Katika ujumbe huo uliosambazwa na Al Qaeda katika mtandao wa twitter,Hamza Bin Laden anaagiza mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake.

Osama bin Laden aliuawa na vikosi maalum vya Marekani mnamo mwaka 2011 katika uvamizi nyumbani kwake huko Abbotabad,Pakistan.

Friday, August 7, 2015

Nigeria yapanga kuunda silaha zake


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameiamuru wizara ya ulinzi kujenga uwezo wa taifa hilo kujitengenezea silaha zake, haya ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisi ya rais.
Rais Buhari ametaja kuwa jambo ''lisilokubalika'' kwa taifa hilo ''kutegemea sana mataifa mengine kupata zana muhimu za kivita,'' taarifa hiyo imesema.
"Wizara ya Ulinzi inapewa jukumu la kutoa mipango iliyo bayana ya kujenga kiwanda cha cha zana za kivita nchini Nigeria," Rais Buhari amenukuliwa akisema.

Monday, August 3, 2015

Kundi la waislamu lahukumiwa miaka 22 jela


Mahakama moja nchini Ethioipia imelipiga hukumu ya miaka 22 jela kundi moja la waislamu chini ya sheria tata ya kukabiliana na ugaidi.
Washukiwa hao 18 walishtakiwa mwezi uliopita kwa mashtaka ikiwemo lile la ugaidi na njama ya kubuni taifa la kiislamu.
Walikamatwa miaka mitatu wakati wa maandamano ya kupinga serikali kuingilia maswala ya kidini.
Walikana mashtaka hayo na kulalama kwamba walinyanyaswa wakati walipokuwa kizuizini.
Wakati wa ziara ya rais Obama nchini humo baadhi ya wanaharakati walimueleza kuhusu kesi hiyo.
BBC

Mabadiliko ya tabia ya nchi kupata Dawa?


Rais wa Marekani, Barack Obama amezindua kile alichokiita hatua muhimu zaidi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema kizazi hiki ni cha mwisho chenye kushughulikia suala hilo na kwamba imelazimu Marekani kuchukua hatua.
Obama amesisitiza hatua kali kuchukuliwa haraka, kupunguza gesi ya ukaa inayotoka katika viwanda nchini Marekani, theluthi moja, ifikiapo mwaka 2030.
Wachambuzi wa mambo wanasema mpango huo unatazamwa kama changamoto kwa nchi nyingine zikielekea kabla ya mkutano mkuu utakaofanyika jijini Paris.
Umoja wa Mataifa umepokea vyema mpango wa Marekani pia Umoja wa Ulaya huku ukipingwa vikali na wapinzani kutoka chama cha Republican.
BBC

Jeshi la Nigeria laokoa mateka 178 mikononi mwa Boko Haram


Jeshi nchini Nigeria limewaokoa watu 178 waliokuwa wakishikiliwa mateka na kundi la Boko Haram, wakiwemo watoto zaidi ya 100 katika jimbo la Kaskazini la Borno.

Msemaji wa Jeshi hilo Kanali Tukur Gasau amesema kati ya watu hao walikuwa watoto 101, wanawake 67 na wanaume 10.

Katika Operesheni hiyo ya uokoaji iliyofanyika katika eneo karibu na Aulari takriban kilometa 70 kusini mwa Maiduguri ambao ni mji mkubwa kaskazini mwa Nigeria, Kamanda mmoja wa kundi la Boko Haram pia alikamatwa.

Miezi ya hivi karibuni Jeshi la Nigeria limetangaza kuwaokoa mamia ya watu waliokuwa wakishikiliwa mateka na kundi la Boko Haram, haswa katika eneo sugu la msitu wa Sambisa, ambao ni ngome kubwa ya wapiganaji hao wa kiislam.

Kundi la Boko Haram limewaua raia takriban 5,500 nchini Nigeria tangu mwaka 2014.

Mpaka sasa zaidi ya wanafunzi wasichana 200 wa Chibok hawajulikani walipo, ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu walipotekwa shuleni kwao kaskazini mwa Nigeria, ambapo wengi kati ya waliotekwa ni wakristu.

Mwezi Oktoba mwaka jana serikali ya Nigeria ilisema imefikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa wanafunzi hao, lakini kundi la Boko Haram limekanusha madai hayo.

Thursday, July 23, 2015

Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa

Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa imetua.
Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.
Awali idara ya polisi nchini Kenya ilikuwa imetangaza kuwa anga yote ya Kenya itafungwa kwa muda wa siku tatu kabla ya ziara hiyo lakini kwa mujibu wa shirika la KCAA ndege zote zinazopaa chini ya futi elfu ishirini hazitaruhusiwa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyatta na uwanja wa wilson mjini Nairobi kuanzia siku ya Ijumaa hadi siku ya jumatatu, wakati wa kongamano la kimataifa ya ujasiriamali litakalofanyika mjini Nairobi.
Agizo hilo sasa linamaanisha ndege zote ndogo ndogo ambazo uhudumu kati ya Nairobi na Somalia na viwanja vingine vidogo vidogo katika kanda ya Afrika Mashariki, havitaruhusiwa kutua Nairobi hadi mkutano huo utakapomalizika.
Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa mjini Nairobi siku ya Ijumaa usiku ambapo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kibiashara kwa pamoja na mwenyeji wake rais uhuru Kenyatta.
Wakati huo huo, idara ya polisi nchini Kenya imetangaza ratiba ya usafiri wakati wa mkutano huo wa kimataifa.
Barabara kuu kati kati mwa mji mkuu wa Nairobi na zile zinazoelekea, katika makao makuu ya umoja wa mataifa mjini Nairobi zitafungwa wakati wa mkutano huo, na idara hiyo imetoa wito kwa Wakenya kujiepusha na shughuli katikati mwa mji na maeneo ya mkutano huo kuanzia siku ya ijumaa hadi siku ya jumapili.

Tuesday, July 21, 2015

UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO

 

Mama ambaye amejifungua mara ya kwanza anaweza kuhitaji msaada katika kunyonyesha. Msaidie ili aweze kuwa mtulivu na makini kwa kazi hiyo. Msaidie kwa kutumia mablanketi na miito ili aweze kukaa wima na kujisikia vizuri. Waombe wanafamilia na wageni kumpa mama na mtoto faragha. Mtie moyo. Unyonyeshaji huwa rahisi kadri mama atakavyoendelea kunyonyesha na kupata uzoefu.

Maziwa ya mama ni bora kwa mtoto kuliko aina yoyote nyingine ya maziwa au mchanganyiko wowote wa vyakula vingine
Mwepushe mama maumivu kutokana na michubuko ya chuchu kwa kumweka katika mkao mzuri wa unyonyeshaji. Geuza mwili wote wa mtoto umwangalie mama ili shingo yake isipinde. Subiri hadi atapopanua mdomo wake. Halafu mweke kwenye ziwa. Chuchu na eneo jeusi linalozunguka linapaswa kufunikwa ndani ya mdomo wa mtoto.


Chuchu ndani ya mdomo wa mtoto
Mdomo wa chini ukiwa umefunika sehemu ya chini ya eneo jeusi la ziwa
Mdomo ukiwa wazi kabisa
Mtoto akiwa ameshikiliwa karibu na mwili wa mama yake
Kama hivi.
Siyo kama hivi. Mkao mbaya unaweza kumsababisha maumivu kutokana na michubuko kwenye chuchu.

Maziwa ya mwanzo ya mama ni sawa na kimiminika cha dhahabu

Maziwa ya mwanzo hutoka katika kiwango kidogo, lakini kiwango hicho ni sahihi kwa mtoto ambaye ndiyo amezaliwa. (Tumbo la mtoto ambaye ndiyo amezaliwa hubeba kiasi cha vijiko vya chai vichache tu vya maziwa kwa wakati.) Maziwa ya kwanza yananata na huonekana ya njano njano. Lakini ingawa huonekana tofauti, ndiyo chakula sahihi kwa mtoto ambaye amezaliwa . Maziwa hayo yana virutubishi muhimu vilivyotengenezwa na mwili wa mama yake kwa ajili ya kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi . Usimwage au kupoteza maziwa ya kwanza: ni muhimu kwa mtoto kuliko dawa yoyote ile. Unyonyeshaji ndani ya siku 2 za mwanzo ni muhimu kwa sababu husaidia kufungulia maziwa yaliyokamaa ambayo mama huanza kuzalisha ndani ya siku 3 baada ya kujifungua. Kadri mtoto anavyonyonya ndivyo na wingi wa maziwa ambayo mama yake atazalisha.

Je mtoto anapata maziwa ya kutosha?

Usiruhusu mtu yoyote akwambie kuwa huwezi kuzalisha maziwa ya kumtosha mtoto wako, hasa katika siku chache za mwanzo wakati mwili wako ndiyo unaanza kuzalisha maziwa.
Kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa watu wengine na kutojiamini, akina mama( au mabibi, mashangazi au wakunga ambao wanasaidia kutoa msaada) huanza kuwalisha watoto ambao ndiyo wamezaliwa au watoto wachanga maziwa ya kopo, au uji, au vyakula vingine. Vyakula hivi vya ziada ni kupoteza fedha bure na pia vinaweza kusababisha mtoto kuharisha. Kuharisha husababisha mtoto kupoteza uzito na kuwa dhaifu.Na matumizi ya vyakula hivi husababisha mama atengeneze maziwa kidogo.Hivyo, hujikuta akiamini zaidi kwamba hawezi kumlisha mtoto wake vya kutosha kwa kutumia maziwa yake pekee. Kama wewe ni mfanyakazi wa afya, unaweza kuzuia mduara huu wa matatizo makubwa ya afya kwa kuwaonyesha akinamama kuwa una imani na uwezo wao wa kuwanyonyesha watoto wao. Msaidie mama kumweka mtoto katika mkao mzuri wa kunyonya, lakini pia mpatie mama nafasi ya kujifunza yeye mwenyewe jinsi gani unyonyeshaji unamsaidia mtoto. Ongea naye vizuri, taratibu. Kuwa na subira.

Kutengeneza maziwa ya kutosha

  • Nyonyesha mara kwa mara. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.
  • Tumia vinywaji vya kutosha na kula zaidi. Mlishe mtoto wako kwa kujilisha mwenyewe.
  • Pumzika mara kwa mara.Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.
Kadri unavyonyonyesha mara nyingi ndivyo utakuwa na maziwa mengi zaidi.
Watoto wengi hupoteza uzito kidogo katika wiki yao ya kwanza. Hili ni jambo la kawaida. Lakini baada ya hapo, upunguaji uzito humaanisha mtoto hapati lishe yakutosha. Vilevile, watoto hawakojoi sana siku yao ya kwanza, lakini baada ya hapo wanapaswa kutoa mkojo kila baada ya saa chache. Iwapo mtoto hatakojoa sana baada ya siku 2, atakuwa hapati maziwa ya kutosha. Je, kama mtoto atakuwa ananyonya mara kwa mara lakini hakojoi au kuongezeka? Katika hali kama hiyo ambayo siyo ya kawaida, unaweza kuhitajika kutafuta maziwa mbadala. Usimpe sukari au maji ya mchele. Usimpe maziwa mbadala ya makopo isipokuwa kama utakuwa na uhakika wa kumpatia kiasi kilichopendekezwa (kuongeza maji husababisha mtoto kuharisha na kuugua). Na usitumie chupa: hazisafishiki kwa urahisi na hivyo hueneza vijidudu ambavyo husababisha mtoto kuharisha.
Maziwa mbadala yanaweza kutolewa iwapo mama atafariki au atatengana na mtoto wake, au kwa nadra sana iwapo atakuwa kweli hatengenezi maziwa ya kutosha. Unaweza kumuomba mama mwingine kumnyonyesha mtoto huyu. Lakini kwanza apate kipimo cha virusi vya UKIMWI kujua iwapo yu salama. Hii ni kwa sababu virusi vya UKIMWI vinaweza kuenezwa kwa mtoto kupitia unyonyeshaji. Njia nyingine ni kutumia maziwa ya wanyama, mfano maziwa ya ngo’mbe au mbuzi yakiandaliwa kama ifuatavyo:
Changanya:
Kipimo 2 vya maziwa ya ngo’mbe au mbuzi
Kipimo 1 cha maji
Kijiko 1 kikubwa cha sukari
AU
Kipimo 1 cha maziwa ya kondoo
Kipimo 1 cha maji
Kipimo 1 cha kijiko kikubwa cha sukari

AU
Vipimo 2 vya maziwa ya kopo yaliyotelewa mafuta na ambayo hayajakolezwa sukari kiwandani
Vipimo 3 vya maji
Kipimo 1 kijiko kilichojaa sukari

Chemsha maziwa uliyotengeneza ili kuua vijidudu. Halafu ruhusu yapoe ndiyo umpatie mtoto kwa kutumia kikombe au kijiko kisafi.
Kukamua ziwa kwa mkono
Kama unalazimika kwenda kazini au kumuacha mtoto nyuma kwa sababu yoyote ile, unaweza kujaribu kukamua maziwa yako ili utakapokuwa umeondoka mtu mwingine aweze kumpa mtoto maziwa hayo.

  1. Nawa mikono yako vizuri na kusafisha chombo cka kukamulia.
  2. Kamata ziwa kwa vidole vyako na dole gumba likiwa pembeni mwa eneo jeusi linalozunguka chuchu. Kandamizia ziwa kwenye kifua chako. Halafu bonyeza vidole vyako pamoja ukiwa unalekea kwenye chuchu. Jisikie huru na fikiria kuhusu mtoto wako wakati unakamua maziwa hayo-hii itasaidia maziwa kutoka kwa urahisi

    Maziwa ya mama yatabaki salama kwa saa 8 kama hakutakuwa na hali ya joto kali nje.

Maambukizi ya kuvu mdomoni

Tumia kitambaa kidogo kisafi kusambaza dawa ndani ya mdomo wa mtoto.
Mabaka meupe ulimini au ndani ya shavu na kero wakati wa kunyoya vinaweza kuwa dalili ya maambukizi ya kuvu mdomoni. Maambukizi hayo yanaweza kwenea hadi kwenye chuchu ya mama na kusababisha wekundu, mwasho, na maumivu.
Jaribu kusuza chuchu na siki (vinegar), na baadaye kwa maji ya kawaida. Au kama huna siki, jitahidi tu kusafisha na kukausha chuchu yako kila baada ya kunyonyesha. Iwapo hii haitasaidia, paka dawa ya Jiivi kidogo kwenye chuchu mara 2 kwa siku 3. Pia paka Jiivi ndani ya mdomo wa mtoto mara moja kwa siku. (Kila kitu kitageuka kuwa na rangi ya zambarau lakini ni salama). Kama Jiivi haitasaidia, mpe mtoto dawa ya nistatini (nystatin).
Kama maambukizi ya kuvu yatakuwa yanapotea na kurudi, mtoto anaweza kuwa na tatizo lingine ambalo linadhoofisha kinga yake ya kupambana na maambukizi. Kwa mfano, watoto wachanga wenye VVU wanaweza kupatwa na kuvu mdomoni mara nyingi zaidi. Angalia VVU na UKIMWI (kinaandaliwa).

Maumivu ya ziwa, uvimbe, kuziba, au maambukizi

Wakati mwingine maziwa yanaweza kuziba mrija (njia ndogo ndani ya ziwa ambazo husafirisha maziwa). Ziwa huanza kuvimba, hugeuka kuwa jekundu na kutoa maumivu. Mara baada ya hapo, maambukizi yanaweza kuanza.
Dalili
  • Eneo lenye moto, wekundu na gumu kwenye ziwa
  • Maumivu katika ziwa wakati wa kunyonyesha
Kama kuna homa, basi mrija ulioziba umepata maambukizi.
Matibabu
  • Pumzika. Tumia vinywaji kwa wingi.
  • Nyonyesha angalau kila baada ya saa 2. Unyonyeshaji hata kama ziwa lina maambukizi ni salama kwa mtoto na ndiyo njia pekee ya kuyaondoa maambukizi.
Gandamiza kwa kwenda chini
ili kukanda eneo lililoziba
  • Hakikisha upo katika mkao mzuri wa kunyonyesha. Mwili mzima wa mtoto lazima umwangalie mama yake. Mdomo wa mtoto unapaswa kufunguka sana, na chuchu ingizwe ndani ya mdomo wake.
  • Nyonyesha upande unaouma kwanza, na uruhusu mtoto kumaliza maziwa yote kwenye ziwa.
  • Kukanda polepole kwa kutumia kitambaa kisafi na maji ya vuguvugu, au kuoga maji ya moto vinaweza kusaidia.
Wezesha ziwa lipate joto dakika 15 au 20 ,angalau mara 4 kwa siku. Au, weka nguo baridi au majani ya kabiji kwenye ziwa ili kupunguza uvimbe.
Kama kuna homa, mpatie dawa ya erithromaisini (erythromycin), miligramu 250 mara 4 kwa siku.

VVU na unyonyeshaji

Hivi sasa kuna dawa ambazo husaidia wanawake wajawazito wenye VVU kuwa wenye afya zaidi na kuzuia mambukizi ya virusi hivyo kwa watoto wao.Ili kuwalinda wanawake na watoto, kila mwanamke mjamzito anapaswa kupata kipimo cha VVU. Na iwapo atakuwa na VVU, anapaswa kupewa dawa za VVU, kwa muda wote atakapokuwa ananyonyesha, na baadaye kama atazihitaji. Angalia VVU na UKIMWI (kinaadaliwa).
Je, ni salama kunyonyesha iwapo una VVU?
Dawa za VVU huzuia uenezaji wa maambukizi wakati wa unyonyeshaji. Aidha mama au mtoto lazima atumie dawa hizo kila siku hadi mtoto atakapofikia hatua ya kuachishwa ziwa. Afya ya mtoto hulindwa pia kwa kumpatia maziwa ya mama kwa miezi 6 ya kwanza (au hadi atakapoota meno yake ya kwanza). Uji na vinywaji vingine siyo vizuri kwa afya ya mtoto.
Dawa za VVU kwa mama na mtoto zitawasaidia wote wawili kuwa na afya.
Bila dawa za VVU, kuna hatari ya maambukizi kupitia unyonyeshaji. Lakini hatari kutokana na kumlisha mtoto vyakula mbadala ni kubwa zaidi. Akina mama wengi wenye VVU hawana maji safi na salama, nishati ya kupikia, au fedha za kununua,kutayarisha na kumlisha mtoto kwa usalama vyakula hivyo mbadala. Watoto wao wana uwezekano mkubwa wakupatwa na utapiamlo, na ugonjwa wa kuhara, na wanaweza kupoteza maisha. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya mama ndiyo salama zaidi – hata kama mama au mtoto atakuwa hatumii dawa za VVU.

Kwa watoto na akina mama sehemu zote, ziwa ndiyo bora zaidi

Unyonyeshaji

  • Gharama yake ni nafuu. Hakuna haja ya kununua vyakula mbadala, chupa, au chochote kingine.
  • Husaidia kusimamisha utokaji damu baada ya mama kujifungua.
  • Husaidia kuzuia mimba miezi inayofuatia kujifugua.
  • Huwalinda akina mama dhidi ya saratani na matatizo ya mifupa baadaye katika maisha yao.
  • Maziwa ya mama yanakuwa ndiyo yametengenezwa, yakiwa na vuguvugu, na tayari kutumika.
  • Yana virutubishi vyote ambavyo mtoto anahitaji.
  • Husaidia kuwakinga watoto dhidi ya kuhara, kichomi (nimonia) na magonjwa mengine.
  • Ni kinga inayodumu muda mrefu dhidi ya ugonjwa wa kisukari, mzio na saratani mbalimbali katika maisha ya mtoto ya baadaye.
  • Humweka mtoto salama na mwenye joto la kutosha akiwa pembeni mwa mama yake.
  • Humfanya mama na mtoto wake kuwa karibu zaidi.

Friday, July 17, 2015

Ibada ya Eid yakumbwa na milipuko Nigeria


Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa takriban watu 9 wameuawa kwenye mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga kwenye mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Damaturu.
Wanasema kuwa washambuliaji wote walikuwa ni wanawake , mmoja mwenye mri mkubwa na mwingine mwenye umri wa miaka kumi.
Ripoti zingine zinasema kuwa idadi ya waliokufa ni kubwa.
Mashambulizi mengine yalifanyika kwenye maombi ya kusherehekea siku kuu ya Eid ul Fitr ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mashambulizi kama hayo hulaumiwa kwa kundi la kiislamu la Boko Haram ambalo limeongeza mashambulizi yake tangu rais Muhammadu Buhari aingie madarakani.

ISIS watumia mtoto kuchinja kichwa cha mateka

Horror: Video of the incident has been shared by ISIS supporters on social media and shows a child no older than 10 carrying out the brutal beheading
Brutal murder: The regime soldier is seen being forced to lay on his stomach as the young boy approaches him from behind, pulls his head back by the hair, and uses a small knife to behead himHarrowing footage: Today's savage murder is not the first time ISIS have used boys to commit a sickening murder. It isn't even the first time the terror group has employed child executioners in Palmyra (pictured)Waiting crowd: Earlier this month ISIS released an execution video from inside Palmyra, showing 25 child executioners lining up regime soldiers in a Roman amphitheatre and shooting them in the head
Blood-thirsty: A baying crowd of men and boys gathered in the restored ruin waiting for the slaughter, many wearing military uniforms and headscarves


ISIS' child killers are dubbed 'cubs of the caliphate' and have proven to be an increasingly common propaganda tool for a group determined to prove itself as the most depraved in human history.
The first confirmed example of child executioners being employed by ISIS is believed to have been in January, when two children shot dead a pair of former jihadis who 'confessed' to being spies operating undercover within the terror group on behalf of Russian intelligence.

Since then there have been numerous examples of ISIS jihadis using children to shoot their enemies dead - ranging from slick, professionally produced videos aimed at a Western audience, to grainy mobile phone footage intended for the private entertainment of the militants themselves.
Yesterday 17 government troops including a commander were killed fighting ISIS near Palmyra.
Palmyra, which is famed for its ancient ruins, has been under ISIS control since May, but in recent weeks government troops have advanced to within a few miles of the city.
Meanwhile in northeastern Syria, Kurdish forces backed by government shelling seized an area south of the city of Hasakeh from ISIS forces.

Saturday, July 11, 2015

Viongozi wa Ulaya kuamua hatima ya Ugiriki

waziri wa uchumi wa ugiriki awasili Brussel
Siku muhimu ya majadiliano kuhusu madeni ya Ugiriki, imeanza mjini Brussels, kuamua iwapo Ugiriki itabaki katika umoja wa nchi zinazotumia sarafu ya euro au la.
Jopokazi, linachambua ombi la Ugiriki, kutaka msaada mpya kabla ya mawaziri wa fedha kukutana.
Serikali ya Ugiriki inapendekeza kuchukua hatua kali zaidi za kubana matumizi, kama kuzidisha kodi ya mapato na kuzidisha umri wa kuweza kustaafu.
     Serikali inatumai hatua hizo zitaweza kuipatia mkopo wa dola bilioni-60, na kusamehewa baadhi ya mikopo ya sasa.
Mapendekezo hayo yalikubaliwa kwa sauti kubwa katika bunge la Ugiriki, kwenye kikao cha jana usiku.
Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya, wanatarajiwa kujadili mapendekezo hayo ya Ugiriki siku ya jumapili.
Awali, Bunge la Ugiriki liliunga mkono kwa asilimia kubwa mapendekezo ya hivi punde la serikali ya waziri mkuu Alexis Tsipras yenye lengo la kumaliza tatizo la deni la nchi hiyo.
Baada ya kikao kilichoendeleka hadi usiku wabunge 252 waliipa serikali idhini ya kufanya mazungumzo na wakopeshaji wake.
Waziri mkuu Alexis Tsipras alishindwa kupata kura za wabunge kumi kutoka chama chake cha Syriza wakiwemo mawaziri wawili wa serikali na spika wa bunge.


Waziri wa zamani wa fedha Yanis Varoufakis hakuhudhuria kikao hicho.
Bwana Tsipras alikiri kuwa mabadiliko yaliyopendekezwa yalikuwa nje ya ahadi zilizotolewa na chama chake.
Mapendekezo hayo yatajadiliwa na mawaziri wa fedha wa nchi za ulaya hii leo na pia viongozi wa ulaya leo jumapili.
bbc

Burundi:Uchaguzi waahirishwa tena

Uchaguzi wa Burundi umeahirishwa tena.
Msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza amesema uchaguzi utafanyika tarehe 21 Julai.
Uchaguzi huo umekumbwa na utata baada ya makundi ya upinzani kuandamana na kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
     Upinzani unadai kuwa rais Nkurunziza anakiuka katiba ya taifa na mapatano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa mujibu wa Msemaji wa rais ,Gervais Abayeho uchaguzi huo umeahirishwa kutoka tarehe 15 hadi tarehe 21 kufuatia shinikizo la viongozi wa kanda ya Afrika mashariki na Kati.
Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta waliendekeza uchaguzi uahirishwe kufuatia mgogoro wa kisiasanchini Burundi.
Shinikizo hilo la kuahirisha uchaguzi lilitokana na Umoja wa Afrika, na Umoja wa mataifa, jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki, pamoja na kikosi cha kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba idadi kubwa ya watu waliokimbia walisema nchi hiyo inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kisiasa.

Zaidi ya raia laki moja wa Burundi wamekimbia nchi hiyo tangu mwezi Aprili wakati kulizuka ghasia kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa uchaguzi huo kuahirishwa baada ya tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi kwa majuma matatu kutokea tarehe 26 Juni hadi tarehe 15 Julai

bbc

Friday, July 10, 2015

Mapinduzi mengine yaandaliwa Burundi

Mmoja wa viongozi katika mapinduzi yaliyozimwa nchini Burundi hivi karibuni ya kumpindua Rais Piere Nkurunziza ameiambia BBC kuwa waasi wao wamekuwa wakiwapa mafunzo polisi na askari kwa ajili ya jaribio jingine la kumwondoa rais Pierre Nkurunziza.
Akiwa uhamishoni Generali Leornard Ngenda Kumana amekanusha kuwa walisaidia na mataifa ya nje.
Wamekuwa wakimshutumu Rais Nkurunziza kuwa kusababisha vurugu kaati ya jamii ya wahutu na watutsi na kuwapa silaha wapiginaji wa vijana waoiunga mkono serikali ambao wanaonekana wengi ni kutoka jamii ya wahutu.
Zaidi ya watu laki moja wamekimbia nchi hiyo wakihofia vurugu wakati wa uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Wanaompinga wanasema hatua ya kugombea urais kwa muhula wa tatu kwa rais huyo ni kinyume cha katiba.

Tuesday, July 7, 2015

Watu 25 wauawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitolea mhanga katika mji wa Zaria.





 


  watu 25 wameripotiwa kufariki dunia  katika shambulio la bomu la kujitolea mhanga katika mji wa Zaria.
 Maafisa wa serikali Kaskazini mwa Nigeria wamesema kuwa watu wengine 32 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo. Shambulio hilo lilitokea katika jengo moja la serikali ambako wafanyakazi wa serikali walikuwa wamekusanyika kusajiliwa.
 Wengi waliokuweko ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Katika kipindi cha majuma 2 yaliopita takriban watu 220 wameuawa katika mashambulizi kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Gavan wa jimbo la Kaduna amewaonya wenyeji kuwa waangalifu sana na kuepuka maeneo yaliyojaa watu kwani hayo ndio yanayolengwa na washambuliaji wa kujitolea mhanga.
 Gavana Nasir El-Rufa'I amewasihi wenyeji waepuke misikiti makanisa masoko na vituo vya mabasi hadi pale hali itakapotulia.
Inspekta wa polisi wa Nigeria ameomba wanigeria kuwa makini na waangalifu akisema kuwa ''kwa sasa inaonekana mabomu yameundwa mengi na kwa hakika likishaundwa bomu ni vigumu sana kuzuia mashambulizi ya kujilipua kwenye umati wa watu ilikuzidisha maafa''.
Tayari hofu imetanda katika mji wa Abuja ambapo Polisi wamepiga marufuku uuzaji na uchuuzi katika barabara za katikati ya mji.

Post Labels