watu 25 wameripotiwa kufariki dunia katika shambulio la bomu la kujitolea mhanga katika mji wa Zaria.
Maafisa wa serikali Kaskazini mwa Nigeria wamesema kuwa watu wengine 32 wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo. Shambulio hilo lilitokea katika jengo moja la serikali ambako wafanyakazi wa serikali walikuwa wamekusanyika kusajiliwa.
Wengi waliokuweko ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Katika kipindi cha majuma 2 yaliopita takriban watu 220 wameuawa katika mashambulizi kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Gavan wa jimbo la Kaduna amewaonya wenyeji kuwa waangalifu sana na kuepuka maeneo yaliyojaa watu kwani hayo ndio yanayolengwa na washambuliaji wa kujitolea mhanga.
Gavana Nasir El-Rufa'I amewasihi wenyeji waepuke misikiti makanisa masoko na vituo vya mabasi hadi pale hali itakapotulia.
Inspekta wa polisi wa Nigeria ameomba wanigeria kuwa makini na waangalifu akisema kuwa ''kwa sasa inaonekana mabomu yameundwa mengi na kwa hakika likishaundwa bomu ni vigumu sana kuzuia mashambulizi ya kujilipua kwenye umati wa watu ilikuzidisha maafa''.
Tayari hofu imetanda katika mji wa Abuja ambapo Polisi wamepiga marufuku uuzaji na uchuuzi katika barabara za katikati ya mji.
Post a Comment Blogger Facebook