Idriss na Wema Sepetu |
Wema Sepetu leo kupitia ukurasa wake wa Instgram amefunguka mambo mengi na kuonyesha kufurahishwa na wala hajutii kuanzisha mahusiano na Idris Sultan, katika ujumbe wa Wema anasema wazi anampenda Idris si kwa sababu tu na yeye anampenda hapana bali ni kutokana na ukweli kwamba Idris ametengeneza historia nyingine katika maisha yake na kumfanya kuwa mtu bora na kubadili kabisa maisha yake.
Wema Sepetu alizidi kushusha shukrani kwa kijana huyo na kusema ikiwa leo ni siku yake ya kuzaliwa Idris Sultan anataka kumueleza kuwa yeye Wema Sepetu anajiona ni mtu mwenye bahati kumpata yeye kama mtu wake au mpenzi wake na kusema atamtunza na kumheshima kwa muda mrefu sana.
Zifuatazo ni baadhi ya nukuu kutoka kwa Wema Sepetu katika ujumbe wake huo ambao umekuwa ujumbe maalumu kwa mpenzi wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa.
" Nimeandika na kufuta karibia mara mia maana kila ninachotaka kuandika najikuta naona hakifai and maybe hakitoshi.... Im busy looking for the Proper words to tell you how I truly feel but naona kama sio.... I thought deep and I jus simply decided to write this Idris I love you, not only because you are my man or because you love me too No...!!! I love you because you make me a Better person, You changed my whole life.... You Complete me" Alisema Wema
"You are the only person That has really made me feel like a woman.... Oh...! I just love you with all my heart... Now before The Clock strikes 12, Let me be The 1st to wish you a Happy Birthday My Love " Alimaliza Wema Sepetu
Post a Comment Blogger Facebook