0
rich mavoko
Staa wa Africa na Bongo flava, Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha nia yake ya kuwasaidia wengine kukua kimuziki baada ya kufikia hatua kumsainisha Rich Mavoko kwenye lebo yake ya Wasafi.

“Rich Mavoko mara ya mwisho nilikuwa natakiwa nimsaini wasafi, Rich mavoko alitakiwa awe signed wasafi kabla ya nyimbo yake hii kutoka, ilitakiwa ikitaka awe chini ya wasafi, lakini kuna vitu vilichelewesha kwasababu kulikuwa na project namalizia kwanza,”

Diamond aliiambia Ayo Tv, “Nikamwambia, alikuwa anazungumza na uongozi wangu, kwahiyo wakamwambia kwasababu ishafika time unatakiwa utoe wimbo basi itoe tu hii nyimbo alafu then after hapo ikiwezekana kuanzia next project ndo anaweza akawa anatoa nyimbo akiwa chini ya wasafi.” Alielezea.

Hadi sasa waanii ambao wapo chini ya label hiyo ni pamoja na Harmonize na Raymond.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top