0
Director Adam Juma amejibu lawama ambazo amekuwa akizipata kwa muda mrefu kuhusu video zake kutochezwa na vituo vya kimataifa kama MTV na Trace licha ya kuwa na ubora mkubwa.

Adam amesema kuwa sababu kubwa ya video nyingi anazofanya kushindwa kuchezwa zinaanzia kwa wasanii wenyewe.

Hiki ndicho amekisema kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm:

“Mi mtaendelea kunilaumu mpaka mtafika sehemu mtakuja kugundua, hata akija kufanya mtu mwingine mwisho wa siku hamuwezi mka solve, lazima mjue source ya matatizo…mnaweza mkafikiri labda mimi sitaki hizo video ziende huko, lakini swala sio hilo video zisiende huko, wasanii wenyewe pia sio wavumilivu…Alikiba kafanya video akaja akaitoa, kachelewa sana kuitoa, Trace wanatumia wiki tatu kui review video…hawakubali kupiga video baada ya watu wengine kupiga wanataka wao waanze kupiga wao, kwahiyo kuna wasanii wengine wajanja, wanaipeleka kule video miezi miwili mitatu mpaka ije kupita wakishapewa hiyo exclusive baada ya siku mbili tatu ndio wanaaachia bongo…Sasa mtu anataka ashut leo leo ipigwe Tanzania halafu iende ikapigwe na Trace…sasa mtu mwingine anakua ananilalamikia mimi bila sababu utafikiri mimi nafanya kazi bure tu. “– AJ

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top