0
URAFIKI wa mashaka! Mastaa wawili wa filamu Bongo, ambao walikuwa mashosti  kwa muda mrefu kabla ya kidudumtu kuingilia kati hivi karibuni na kusuluhishwa, hivi sasa bifu kati yao limeanza upya, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Chanzo chetu ambacho hakipepesi macho kinasema tangu Aunt ajifungue mtoto, Wema hakuwahi kukanyaga nyumbani kwake kwa ajili ya kumuona, kutoa hongera au hata pole kwa rafiki yake huyo, isipokuwa wamekuwa wakichati kupitia simu za mikononi, kitu ambacho si sahihi.

Lakini kali zaidi, ni kitendo cha Wema kushindwa kuhudhuria sherehe ya kutimiza siku 40 tangu azaliwe mtoto huyo, Cookie, kitu kilichomfanya mwenzake kumuondoa kabisa katika orodha ya marafiki zake.

“Yaani Aunt kipindi chote alimvumilia akijua huenda yuko ‘bize’, lakini kwa kutofika kwenye siku hiyo muhimu, amemtoa kabisa akilini mwake,” kilisema.

Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Aunt ili kuthibitisha ubuyu huo, lakini akakubali tu juu ya kutohudhuria kwenye tukio hilo muhimu la mtoto wake, licha ya kuwa alimpa taarifa.

“Hakuja, lakini siwezi mlaumu sana, labda alikuwa na majukumu mengi, ukizingatia hivi sasa ana mambo ya ubunge,” alisema.

Wema hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutopokelewa kwa muda wote alipopigiwa.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top