0
Diamond Platnumz ambaye ameonesha kuwa na shauku kubwa ya kuwa baba, amesema kuwa mpenzi wake Zari yupo Tanzania kwasababu zimebaki wiki chache kabla hajajifungua.

Akizungumza kwenye exclusive Interview ya Mambo Mseto na Willy M. Tuva wa Radio Citizen ya Kenya, Diamond amesema kuwa anataka mtoto wake azaliwe nyumbani Tanzania.

Diamond na Zari ambao wanatarajia mtoto wa kike, kila mmoja alikuwa ana jina ambalo angependa kumuita mtoto wake, Zari anataka wamuite mtoto wao Zara huku Diamond naye anataka amuite Candy, lakini mwisho wa siku Diamond amesema kuwa wamekubaliana watafute jina litakalokuwa katikati lakini lenye maadili ya dini ya Kiislam.

Katika hatua nyingine Diamond amedai kuwa awali alikuwa amepanga kumshirikisha rapper wa Marekani Ludacris kwenye wimbo wake Nana.

Akiongea kwenye kipindi hicho, muimbaji huyo amesema kutokana na aina ya mdundo uliotumika kwenye Nana, waliona rapper huyo wa ‘How Low’ asingeweza kufit na ndio maana aliamua kufanya na Flavour.

Amedai kuwa mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni kabisa mwa mwaka ujao, anaweza kuachia collabo inayosubiriwa na msanii wa Marekani.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top