MTANGAZA nia ya kuomba ridhaa ya kuwania
nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo la Mikumi na Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimboni humo, Onesmo Mwakyambo,
ametangaza kujiengua katika chama hicho na kujiunga na ‘Alliance for
Change and Transparency-ACT Wazalendo, kwa madai ya kutukanwa na
kudhalilishwa.
Akizungumza na Mwanahalisi Online, Mwakyambo alikiri kukihama Chadema na Kujiunga na ACT Wazalendo, katika Mkutano uliofanywa na Katibu wa Kamati ya Maadili ya ACT-Wazalendo Taifa, Gibson Kachingwe.
Hata hivyo, Mwakyambo alipata wakati
mgumu pale alipojikuta akizomewa na nguvu ya umma kabla hajapanda
jukwaani, na hata aliposhuka huku akisindikizwa na nyimbo za kumzomea
kuwa ni msaliti, kama yuda Eskariote.
“Ni kweli Mwandishi nimejiunga
ACT-Wazalendo, kwa muda mrefu nimevumilia kutukanwa, kudhalilishwa, na
mbaya zaidi, nimeandikiwa ripoti mbaya kuhusiana na mgogoro wa uhusiano
wa uongozi wa Kata ya Ruaha na Kijiji hicho, hivyo ni bora nipumzike,
nitahamishia majeshi huko.
”Nimemwarifu Katibu wa Chadema Mkoa,
Samuel Kitwika, akate fomu yangu niliyowasilisha kwa utia nia wa ubunge
wa Chadema Jimbo la Mikumi, na badala yake nataka kuhamishia nia yangu
ACT-Wazalendo, lakini ninachokiona, nafanyiwa rafu, amesema Mwakyambo.
Kitwika alikanusha kwamba, Ofisi ya
Chadema Mkoa wa Morogoro ina madudu na upendeleo na kusema, “mko
tunafanya kazi zetu kwa kufuata Katiba ya Chadema, Sheria na Taratibu
zilizoweka, makandokando yake na kubanwa kwake jimboni, asihamishie
kwetu”.amesema
Mbali ya Kitwika kukiri Mwakyambo
kukihama Chadema, alikanusha taarifa kuwa alikuwa anatukanwa,
kudhalilishwa na kuandikiwa ripoti mbaya bila kumtaja aliyemtuka, ila
akasema, Chadema Mkoa kupitia Intelijensia yake, ilikuwa na taarifa za
mienendo yake mibaya ya Mwakyambo dhidi ya Chadema, ikiwemo la kuhamia
ACT-Wazalendo.
“Huyu ni Msaliti, tulimshitukia siku
nyingi,tukakosa imani naye, hana madhara yoyote kwa Chadema, tuko imara,
na ndiyo maana tumemzomea sana kwa kwenda mbele, tangu alipokuwa
jukwaani hadi aliposhuka kuelekea kwake,” amesema Mwilenga.
Post a Comment Blogger Facebook