Akizungumza na waandishi wa habari katika semina fursa
zinazopatikana kwenye msimamizi wa maswala ya ushiriki katika sekta ya
mafuta na gesi kutoka wizara ya nishati na madini Bibi Neema Abson
amesema ushiriki mdogo wa makampuni ya Tanzania katika sekta ya mafuta
na gesi umetokana na mitaji na uelewa mdogo juu ya sekta hiyo na
kusisitiza serikali inachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka sera ya
gesi inatoa kipaumbele cha ushiriki wa makampuni ya kitanzania pamoja na
kutoa elimu kwa watanzania.
Sekta ya mafuta na gesi kwa makampuni ya ndani, mkurugenzi mkuu wa
taasisi ya sekta binafsi Bw. Godfrey Simbeye amesema idadi kubwa ya
watanzania hawana mitaji ya kutosha na mabenki yaliyopo hayanauwezo wa
kutoa mikopo inayokidhi mahitaji ya viwango vya kimataifa
vinavyohitajika katika sekta ya mafuta na gesi.
Post a Comment Blogger Facebook