Mwimbaji aliyetamba na video ya “Ole Themba”, Linah Sanga amesema kuwa ili kuwa msanii wa kimataifa kuna gharama kubwa tofauti na wengi wanavyodhani.
Linah alisema anafikiria kila siku kuendelea
kufanya kazi nzuri za kimataifa kama viedo ya ya Ole Themba, lakini kila
anapofikiria kwenda tena Afrika Kusini kurekodi anakumbuka namna
alivyotumia pesa nyingi kukamilisha wimbo huo.
“Siyo kwamba sipendi kurudi tena Afrika Kusini kwa
ajili ya kufanya video nyingine, bali kufanya kazi hizo nje ya
kunahitaji pesa nyingi kuliko hapa Bongo,” alisema Linah.
Linah alisema kufanya video au audio katika nchi
zilizoendelea kuna gharama kubwa, lakini ni lazima msanii atumie muda
mwingi kwa ajili ya kukaa hotelini, gharama za usafiri pamoja na malipo
makubwa ya kazi.
“Ninapenda kufanya kazi tofauti zenye kiwango cha
juu na hivi ndivyo ilivyo kwa wasanii wengi, lakini matumizi makubwa ya
fedha kwa kazi za kimataifa ni makubwa kinyume na watu wanavyodhani.
Ingawa kazi inakuwa nzuri, lakini gharama zake usipime, pengine
waandaaji wetu wa Bongo wanapaswa kujifunza zaidi kutoka kwa wenzao ili
kupunguza wimbi la gharama za kwenda kufanya video huko,” alisema Linah.
Post a Comment Blogger Facebook