Thursday, December 1, 2016

RAYVANNY Amshukuru Mungu Kwa Kumkutanisha na Diamond...Adai Mpaka Nguo Anazofanyia Video ni za Diamond



Ray Vanny Ameandika Haya Kupitia Ukurasa wake wa Instagram:

Rayvanny - Kwenye Video ya #KWETU Nguo zote Ulinipa wewe!!! #MUGACHERERE Nguo zote ulinipa zako... kiukweli Nimepata tabu nyingi Sana Kwenye Mziki wangu Lakini Niliamini Ipo Siku Namimi Nitaonekana.Nashukuru Mungu Sana Kunikutanisha nawewe Brother Naseeb Asante kwa Moyo Wako wa Upendo Kwangu Ulithamini kwa kidogo nilichonacho Nakuamini Nitaweza kufanya.Safari Bado Ndefu Tutafika Tunapotaka!!!

Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi kufutia kifo cha SACP Peter Kakamba


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu kufuatia kifo cha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Peter Kakamba kilichotokea tarehe 30 Novemba, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema anaungana na askari wote wa Jeshi la Polisi, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo cha SACP Peter Kakamba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Natambua mchango mkubwa alioutoa Marehemu (SACP) Peter Kakamba katika Jeshi la Polisi na katika jukumu kuu la ulinzi wa raia na mali zao, kwa hakika tumempoteza kiongozi aliyekuwa akifanya kazi zake vizuri” amesema Rais Magufuli.

“Nakuomba IGP Ernest Mangu unifikishie salamu nyingi za pole kwa familia ya marehemu, askari na wote walioguswa na msiba huu na sote tumuombee Marehemu (SACP) Peter Kakamba apumzishwe mahali pema peponi, Amina” Amemalizia Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Wanawake Waongoza Kuwa Na Virusi Vya Ukimwi Nchini




Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.

Waziri Mhagama alisema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.

“UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizo mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu”

Kwa mujibu wa Waziri Mhagama alisema Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani kuhakikisha wanatokomeza janga la ugonjwa huo  ifikapo mwaka 2030.

Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.

Waziri wa Mambo ya Nje kuongoza ujumbe wa Tanzania Mkutano wa Mawaziri wa Afrika na Korea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Afrika na Korea unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
 
Mkutano huu ambao umeandaliwa na Serikali ya Korea kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika una lenga kukuza ushirikiano pamoja na kuandaa maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Korea na mataifa ya Afrika katika miaka mitatu ijayo.
 
Tanzania ni moja ya nchi nne (4) za Afrika ambazo Korea imezichagua kuanzisha mahusiano ya kimkakati “strategic partnership” yatakayozifanya nchi hizo kupewa kipaumbele katika kupokea misaada na mikopo nafuu kutoka Korea katika kipindi cha miaka mitano ijayo kati ya 2016 hadi 2020.
 
Katika kipindi hicho Tanzania itapokea kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300 ikiwa ni asilimia 17.1 ya msaada utakaotolewa Barani Afrika, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza Barani humo kupata msaada wa Jamhuri ya Korea.
 
Pamoja na ushiriki kwenye Mkutano huo, imependekezwa ufanyike mkutano baina ya Tanzania na Serikali ya Korea kuzungumzia masuala ya ushirikiano baina ya nchi zetu mbili. 

Aidha, ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa Afrika na Korea ni fursa muhimu ya kukuza mahusiano baina ya nchi zetu mbili hususan katika Nyanja ya uchumi. Serikali ya Korea ilitoa ahadi ya kuongeza uwekezaji Barani Afrika hususan katikasekta za nishati, miundombinu na viwanda.
 
Itakumbukwa kuwa, tayari Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Mradi wa kuendeleza kilimo cha Mwani Zanzibar wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.6 na Awamu ya Pili ya Mradi wa kuboresha Uchunguzi wa Afya ya Uzazi Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni nne (4).
 
Miradi mingine ambayo Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania ni ujenzi wa Daraja la Selander Jijini Dar es Salaam, Mradi wa Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi Mkoani Kigoma na Ujenzi wa Hospitali ya Kimataifa iliyopo eneo la Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 01Desemba, 2016.

Waziri Mkuu Majaliwa aiagiza Bodi ya Taifa ya Wahasibu Kuwaanika na Kuwachukulia Hatua Kali Wahasibu Wezi


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameiagiza Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) kuwachukulia hatua wale wote wanaoitia doa taaluma hiyo kwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.

Maagizo hayo yametolewa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango, wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) uliokwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa wahasibu unaojumuisha wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki, katika eneo la Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema kuwa Idadi ya Wahasibu wenye sifa inazidi kuongezeka na hivyo kuisaidia Serikali, japo kuwa Serikali hairidhiki kuona wanataaluma wa Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (CPA) wanaongezeka huku vitendo vya ubadhilifu wa fedha za Umma na ufisadi vikiendelea kuripotiwa.

“Wapo hata wahasibu wanaotumia taaluma yao vibaya, wanaowawezesha wafanyabiashara kukwepa kodi, wanachakachua vitabu vya taarifa za fedha na kufanya ufisadi kwa njia ya kalamu na kompyuta jambo ambalo halikubaliki hata kidogo” Aliongeza Dkt. Mpango

Alisema kuwa machozi ya masikini wa Tanzania yatawafuata mafisadi hadi kaburini lakini serikali ya Awamu ya Tano haitasubiri hao mafisadi wafe, itawatumbua na wala hakuna mzaha na kwamba tayari mahakama ya mafisadi imeanza kazi na itawashughulikia.

Aidha, Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaasa wanataaluma wa uhasibu na ukaguzi wa hesabu kuitumia taaluma yao kuisaidia Serikali katika hatua yake ya kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda kwa kuwa taaluma hiyo ina umuhimu mkubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, Bw. Pius Maneno alisema kuwa, Kituo hicho kilichozinduliwa cha APC hadi kumalizika, kitagharimu Sh. Bilioni 35 ambapo mpaka sasa fedha zilizotumika ni takribani Sh. Bilioni 31.5.

“Gharama halisi za ujenzi wa kituo hicho zilikuwa Bilioni 14 lakini kutokana na mzabuni wa ujenzi kuchelewesha ujenzi ndio maana kumekuwa na Ongezeko la kiasi hicho cha fedha” aliongeza Bw. Maneno.

Ujenzi wa kituo hicho ambao uko katika eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 14 umehusisha ujenzi wa Kumbi za mikutano zinazochukua zaidi ya watu 1600, viwanja vya michezo na vyumba vya kisasa 108 vya kulala wageni.
 
Bw. Maneno alisema kuwa kujengwa kwa kituo hicho kutaifanya Bodi hiyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikitumika kukodi kumbi za kufanyia na kusahisha mitihani ya Bodi (NBAA).

Alizitaja faida zingine kuwa ni kuboreshwa kwa mazingira ya kitaaluma na wanataaluma wa uhasibu pamoja na kuimarika kwa utawala bora na kuwa chachu ya uchumi wa viwanda, kwa kuwa Kituo hicho, kinatoa elimu bora itakayowawezesha wahitimu kuingia kwenye ushindani ndani ya nchi za Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla.

Ujenzi wa Kituo hicho umedhaminiwa na serikali kupitia mkopo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii-NSSF, Bodi ya Uhasibu-NBAA na Mbia mwenza wa kituo hicho, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali-GEPF.

Askofu Gwajima akutwa na kesi ya kujibu.......Mahakama Yamtaka Ajieleze Disemba 13




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuona Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anayekabiliwa na kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha, ana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha alitoa uamuzi huo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa upande wa Jamhuri pamoja na vielelezo.

Alisema kutokana na ushahidi huo, ameona upande wa Jamhuri umejenga kesi hivyo Gwajima na wenzake watatu, wana haki ya kujitetea, kuita mashahidi au kukaa kimya.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa washtakiwa watajitetea kwa njia ya kiapo na watakuwa na mashahidi watatu.

Hakimu Mkeha alisema Desemba 13, mwaka huu, washtakiwa watajitetea na siku hiyo atasikiliza utetezi wa washtakiwa wote wanne pamoja na mashahidi wao.

Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31).

Inadaiwa kuwa, Machi 29 mwaka jana, katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, washitakiwa walikutwa wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Aidha, inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun. Gwajima anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Disemba 2


Scorpion Akana Hoja 6 . . . . Akiri Hoja 3 Ikiwemo Kupata Mafunzo ya Kareti




MSHITAKIWA katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete (34) ‘Scorpion’, amekiri kupata mafunzo ya kareti kutoka chuo cha mafunzo cha Ifakara aliyoyafanya mwaka 1989 hadi 1995.

Aidha, upande wa mashitaka katika kesi hiyo umemuongezea mashitaka ya shambulio kupitia kifungu namba 234 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ambacho kinaruhusu kuongeza au kubadilisha mashitaka.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kwamba kesi hiyo imekuja kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali ambapo katika maelezo ya zaidi ya saa nane, alikiri kuhusu jina lake, sehemu anayoishi ya Machimbo Yombo na mafunzo hayo.

Hata hivyo, alikana kuhusu jina la Scorpion, mashitaka yake na kwamba hakukamatwa wala kuhojiwa na Polisi kuhusu mashitaka hayo.

Katuga alidai kuwa Septemba 6, mwaka huu, mshitakiwa alikuwa maeneo ya Buguruni Sheli na kwamba Septemba 12, alihojiwa na kukamatwa na polisi maelezo ambayo aliyakana.

“Mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi hii wapo sita ambapo upande wetu wa mashitaka utawasilisha vielelezo viwili ikiwemo Fomu namba tatu ya Polisi (PF3) na ripoti ya daktari kwa ajili ya kuthibitisha mashitaka hayo,’’ alidai Katuga.

Hakimu Haule aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 14 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa. Katika mashitaka yake, mtuhumiwa inadaiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu katika maeneo ya Buguruni Sheli, wilaya ya Ilala.

Inadaiwa, Njwete aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 wenye thamani ya Sh 60,000, bangili ya mkononi na fedha taslimu Sh 331,000, vyote vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Said Mrisho.

Inadaiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.

Mwanafunzi Wa Kidato Cha Tatu Anusurika Kufa Mara Baada Ya Kubakwa Na Kutelekezwa Korongoni




Na Woinde Shizza,Meru
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kutelekezwa kwenye korongo la mchanga na kusababishiwa maumivu makali yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa 12:30 alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

“Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimenipelekea nishindwe kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu,” alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli Akyo alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vema Serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani tangu akamatwe mtuhumiwa huyo na kupelekwa kituoni bado hajasomewa shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus alisema kuwa tukio hilo limemfanya mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumpeleka sehemu nyingine jambo ambalo litamsaidia kurudi katika hali yake ya awali.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu Tanesco, Samweli Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara baada ya taarifa kutolewa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Wilson Elias ambae ndie aliyehusika na ukatili huo na kumfikisha katika kituo kidogo cha Polisi Usa River ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa Polisi, Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema  kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016 na atafikishwa mahamani upelelezi ukikamilika.

Sababu ya kuanguka kwa ndege iliyowabeba wachezaji wa timu ya Brazil yatajwa




Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia mawasiliano.

Katika mnara wa mawasiliano ya ndege , rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.

Kabla hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho ,rubani alisikika akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha ajali ya ndege hiyo.

Wanajeshi wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika nguvu ingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.

Wadadisi wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.

Wachezaji wa timu ya Chapecoense walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian kwenye mji wa Medellin mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa miguu ya kihistoria na badala yake wachezaji hao wameacha historia .Kufuatia vifo vya wachezaji wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana kuomboleza vifo vyao.

Kwa muujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika shirika la ndege la Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wameponea chupuchupu kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kukosa tiketi.

Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza namna alivyokwepa kifo, kwamba yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya kujiokoa ,anasema abiria wenzie , walio wengi walisimama na kuanza kupiga kelele nay eye aliamua kuweka sanduku lake la kusafiria kati kati ya miguu yake na kuamua kubaki hivyo.

Visanduku viwili vya mawasiliano vya ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari vimeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga.

Wachunguzi wataalamu kutoka nchini Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika Kusini kwasababu ndege iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa Uingereza BAE nchini Uingereza.

Brazil imeanza siku tatu za maombolezo wakati maelfu ya watu na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika mji yaliko makao makuu ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa maombolezo wakati maandalizi ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil ili kuzikwa kwa pamoja katika uwanja wa Chapeco.

Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.

Timu hiyo iliandika historia ya mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi ya Brazil kwamara ya kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa wameabiri ndege hiyo miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika .Abiria walio wengi walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na waandishi habari wapatao ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza maisha.

Chanzo: bbcswahili

Tuesday, October 4, 2016

Wi-Fi kupatikana bure maeneo ya umma na burudani Dar

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua mpango wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani jijini Dar es Salaam.
samia-one_478_295-1
Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini, utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo kuimarisha uchumi.
“Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu wataweza kupata huduma ya mtandao,” alisema Bi Samia.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa mradi huo juhudi za serikali ya awamu ya tano, kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.

Barnaba: Nimeshauza maji, nshafanya kazi kwa mamantilie, nshaitiwa mwizi…

Anaweza kuwa mmoja wa wanamuziki wa Bongo Flava waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sasa, lakini Barnaba amepitia mengi. Ameshawahi kufanya karibu kila kazi unayoweza kuifikiria.
14574163_1654664108179037_5724717438747017216_n
“Kabla ya kuanza huu muziki nishauza maji, nshauza mamantilie, nishakuwa fundi makenika,” Barnaba alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times kinachoendeshwa na Lil Ommy hivi karibuni.
“Nishaitiwa mwizi, nshauza siso, nshauza vyuma, nshakuwa fundi umeme, nshakuwa fundi nyumba,” aliongeza.
Alidai kuwa kuna wakati alikuwa akilala kwenye makuti katika kibanda kilichokuwa nje ya studio ya dada aitwaye Nzela baada ya kufukuzwa THT.
Msikilize hapo chini.

Wastara arudiana na mpenzi wake wa zamani Bond Bin Sinan

Malkia wa filamu Wastara Juma baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma, amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Bond Bin Sinan.
bondi
Mwigizaji huyo amesema Bond Bin Sinan alikiri makosa yake kwenye vyombo vya habari ndio maana imekuwa rahisi kwake kumsamehe na kurudiana naye.
“Makosa yake aliyokuwa ameyafanya mwanzo ndiyo yaliyosababisha tukaachana nikaamua kuolewa na mtu mwingine,” Wastara alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM. “Kwa hiyo baada ya mimi kuachana na aliyekuwa mume wangu na yeye bado alikuwa ananihitaji, nikaona nimkubalie kwa sababu tayari tulikuwa tunafahamiana naye,”
Bond Bin Sinan ni mwigizaji na pia ni director wa filamu.

Hali ya Rigobert Song yaendelea vizuri, ahamishiwa nchini Ufaransa

Hali ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na nahodha wa timu hiyo, Rigobert Song imedaiwa kuendelea vizuri baada ya kukimbizwa hospitali ya mjini Yaounde Jumapili hii baada ya kuugua ghafla na kuanguka wakati akiwa nyumbani kwake huko Odza. Alishambuliwa na kiharusi.
928422_650483625016814_241768128_n
Song alikuwa akitumia mashine za kupumulia tangu siku aliyofikishwa hospitalini hapo lakini kwa sasa kwa mujibu wa taarifa ya daktari Louis Joss Bitang imesema kuwa hali ya mchezaji huyo inaendelea vizuri kwakuwa hapumulii mashine kwa sasa na amepelekwa nchini Ufaransa kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
“He has come out of his coma and the oxygen has been disconnected. His high blood pressure has returned to normal and the cerebral haemorrhage has been controlled. A medical aircraft will be in Cameroon in (Tuesday) he morning, we will have a working session with the French team and then he will be flown to France,” amesema daktari Bitang.
Song amewahi kuichezea Cameroon jumla ya mechi 137 na kufunga magoli 5 na aliwahi kuchezea timu ya Liverpool na West Ham United lakini pia aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Chad mwaka 2015.

Mke wa Roma Mkatoliki kayaongea kuhusu Uhusiano na ndoa...

Post Labels