Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Tuesday, October 4, 2016

Wi-Fi kupatikana bure maeneo ya umma na burudani Dar

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua mpango wa kuweka huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani jijini Dar es Salaam.
samia-one_478_295-1
Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini, utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo kuimarisha uchumi.
“Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu wataweza kupata huduma ya mtandao,” alisema Bi Samia.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa mradi huo juhudi za serikali ya awamu ya tano, kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.

BINADAMU ALIYEFUFUKA KUTOKA CHUMBA CHA MAITI "NDUGU ZAKE WAMEYASEMA HAYA"

Aliyoyazungumza Julius Mtatiro kuhusu mgogoro wa CUF

Saturday, September 17, 2016

Rais Magufuli Apokea Taarifa Ya Tetemeko La Ardhi Mkoani Kagera, Akabidhiwa Msaada Wa Dola Laki Mbili Utoka Kwa Rais Museveni Wa Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tetemeko hilo limetokea Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Kigoma.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na shs 437 milioni kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake  Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

Thursday, September 15, 2016

Malawi yadai kuishtaki Tanzania kwenye umoja wa Afrika (AU)



Foreign Affairs and International Cooperation minister Francis Katsaira said Tanzania has released a new Lake Malawi map which shows the east African country has taken a chunk of Lake Malawi, which is potentially rich in oil and gas..

“We have already reported them to the African Union and very soon we will be reporting them to Comesa and Sadc,” he said.

Kasaira said Tanzanian authorities have threatened to beat up and arrest Malawians who will disregard the new map.

The old map, drawn up by Germany and Britain gives the whole Lake Malawi, except a small part to Malawi.

Tanzania has taken much interest in the lake after oil was discovered in the lake popularly known as lake of stars.

Katsaira said both Malawi and Tanzania were supposed not to interfere with the Lake Malawi issue as the matter was with the African Union and a mediation team.

He therefore said the government is waiting for a response from Tanzsnia on the proposal for Mutharika and Magofuli to meet inorder to iron out the misunderstanding over the lake.

Malawi disputes Tanzania’s claim to half the lake – Africa’s third biggest.

It has accused Tanzania of raising tension by allegedly intimidating Malawian fishermen on the lake.

Malawi awarded oil exploration licences to firms to search for oil in the lake, which Tanzania calls Lake Nyasa.

Utafiti wa twaweza Watanzania 96% wampongeza Rais Magufuli


Taasisi inayojishughulisha na kufanya tafiti mbalimbali nchini ya TWAWEZA. Leo imetoa ripoti inayoonyesha kuwa asilimia 96 ya Watanzania wapongeza utendaji wa Rais Magufuli, huku asilimia 68 wapongeza uwajibikaji wa wabunge wao.

Aidha katika ripoti hiyo inabainisha kuwa jambo maarufu alilofanya Rais Magufuli ni uondoaji watumishi hewa huku zuio la kuingiza sukari likikosa umaarufu.

Kiwango cha kukubalika cha Rais Magufuli katika utafiti mpya ni cha juu kuliko marais 128 wa Afrika.

Wednesday, September 14, 2016

Tundu Lissu aishukia Serikali kuhusu kutumia fedha za mifuko ya kijamii bila kurudisha


*Anaandika Tundu Lissu*
Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu.
Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara.

Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja. Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja.

Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika.

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja.
Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao. Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa.

Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli




VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.

Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.

Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.

Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.

Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana  kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’

Gavana BOT afichua siri ya kilio cha fedha kupotea mtaani

i


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.

“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.

“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.

Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni  ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.

Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi  trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.

Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

Bodi ya mikopo: hatuhusiki kumtafutia mtu ajira


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala yake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipengele cha Kikaango cha EATV.

“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Alisema Mwaisobwa.

Aidha Mwaisobwa alisema wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.

Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji.

Serikali yabariki wenye jinsia mbili kuchunguzwa

Mamlaka  ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itakuwa na uwezo na mamlaka ya kuchunguza watu waliozaliwa na jinsi mbili na kubaini jinsi tawala yenye nguvu zaidi. 

Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016, uliopitishwa juzi usiku saa nne bungeni unampa Mkemia Mkuu mamlaka ya kuchunguza na kubaini jinsi ya mtu na kutatua utata kwa mtu atakayekuwa amezaliwa na jinsi mbili.

“Waheshimiwa wabunge naona wengi wenu mnadhani mkemia mkuu kazi yake ni kuchunguza vinasaba kubaini uhalali wa mzazi na mtoto, maana naona wabunge wengi wamelishabikia hilo, lakini katika teknolojia ya vinasaba yanahusu pia utambuzi wa jinsi, watu unakuta wanawake au wanaume wanazaliwa jinsi ya kike na kiume, kwa hiyo tunaangalia jinsi tawala ni ipi ina nguvu,” alisema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Ummy alikuwa akijibu michango ya wabunge waliochangia wakati wa kujadili Muswada wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu 2016 kabla ya kuupitisha juzi usiku, waliotaka mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli zake.

Alisema kwa sheria hiyo, sasa mkemia mkuu kupitia maabara yake anaweza kusema jinsi ya kike au ya kiume ndio yenye nguvu, lakini pia kuna suala la kuhakikisha utambuzi wa mwanadamu hasa wakati yanapotokea majanga pamoja na watu wanaosafiri kwa makundi.

Alikubaliana na wabunge kuwa iko haja ya kuwaelimisha wananchi juu ya kazi za maabara ya mkemia mkuu ambao wengi wao wanadhani inafanya kazi hiyo tu ya kubaini vinasaba vya mzazi na mtoto, lakini sasa wafahamu hata waliozaliwa na jinsi mbili wanaweza kutegua utata huo kwa kubaini jinsi tawala au jinsi yenye nguvu zaidi kama ni ya kiume au ya kike.

Alisema Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwepo kihistoria tangu mwaka 1890 na imekuwa chombo cha kiserikali cha uchunguzi cha kikemia wa kimaabara kwa bidhaa mbalimbali na kuongeza kuwa imekuwa ikifanya uchunguzi wa kikemia wa vyakula, dawa na vipodozi hasa pale inapotokea utata au kuhusisha masuala ya kesi za jinai.

Akifafanua zaidi, alisema kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wao wanafanya udhibiti wa ubora wa chakula, dawa na vipodozi na maabara hii inafanya uchunguzi wa kikemia.

“Maabara ya Mkemia Mkuu kazi yake ni kufanya uchunguzi wa kikemia, vinasaba, kesi za jinai na sayansi jinai. Chombo hiki hakipimi kudhibiti ila kufanya uchunguzi kwa ajili ya vitu vyenye maslahi ya taifa au masuala yenye utatanishi na ushindanishi,”alisema waziri huyo.

Akitoa mfano wa mahindi, alisema kulikuwa na tatizo la sumu kuvu, kwa hiyo mkemia mkuu anafanya uchunguzi wa kimaabara na kusema wamekuta mahindi yana sumu au la, au anaweza mfanyabiashara kuleta maziwa ya mtoto TFDA ikapata mashaka, mkemia mkuu atayafanya uchunguzi wa maabara atasema kama kuna sumu ama kuna kemikali isiyo salama kwa matumizi wa binadamu.

“Baada ya uchunguzi wa kimaabara mwenye jukumu la kusema mahindi haya yasiuzwe au maziwa haya yasiuzwe ni TFDA na sio maabara ya mkemia mkuu. Vile mfanyabiashara anaweza kuleta bidhaa, TFDA ikaitilia mashaka, kwa hiyo huyu mwenye bidhaa anaweza kukata rufaa kwa mkemia mkuu ili apimiwe bidhaa yake kuithibitishia TFDA kuwa bidhaa yake ni salama,” alisema.

Waziri Ummy alikuwa akijibu hoja za wabunge, ambao walikuwa wana hofu kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu inaweza kuingilia kazi za taasisi kama TFDA na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Alizungumzia pia kuhusu kuipa mamlaka ya mwisho maabara hiyo, akisema katika nchi zote duniani zenye maabara hizo, lazima serikali iwe na msemaji wa mwisho wa uchunguzi wa masuala ya kimaabara na kikemia, vinasaba, sayansi jinai na kesi za jinai, lakini pia haifuti sheria wala maabara zingine za uchunguzi zilizoanzishwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali.

Kuhusu kutenga bajeti ya kutosha, Ummy alisema serikali imepokea maoni ya wabunge na kuwa baada ya kupitisha muswada huo maabara hiyo imepewa hadhi ya mamlaka na sasa imepewa hadhi na hivyo fungu lake lazima liwe zuri kwa ajili kuendesha shughuli za maabara lakini pia kuajiri watumishi 400 kwani waliopo sasa 192 hawatoshi.

Waziri Ummy alisema wamepokea ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, kufanya uchunguzi wa matumizi ya shisha na kuongeza kuwa tayari mkemia mkuu alifanya uchunguzi na kubaini watumiaji wa shisha wanachanganya bangi, heroine na kokeni na ndio maana serikali ilipiga marufuku kuitumia.

Hata hivyo, alisema sasa itajikita zaidi kuchunguza ili kubaini viambata kiasi gani vilivyopo katika shisha na kwa nini serikali iendelee kupiga marufuku matumizi ya shisha nchini.

kompyuta zenye majibu ya waliopima ukimwi zaibwa



Kompyuta mpakato zenye majibu ya watu waliopima ukimwi pamoja na majina yao zimeibwa mkoani Tabora.

Kompyuta hizo zipatazo 30 zenye thamani ya Sh70 milioni, zimeibwa kwenye ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego linaloshughulika na masuala ya Ukimwi na tohara.

Kompyuta hizo zimeibwa mwishoni mwa wiki kwenye ofisi hiyo iliyo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema tayari taarifa za tukio hilo zimewafikia  na wanaendelea na uchunguzi wa kina kufahamu kilichotokea.

Inadaiwa kuwa kompyuta hizo, zina majina ya watu waliopima VVU na majibu yao.

“Kinachotatiza ni kwamba kama majina ya watu wenye virusi yakijulikana itakuwa ni utata mkubwa kwani ofisi hiyo itakuwa imewaweka katika wakati mgumu pasipo wao kupenda,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Mkurugenzi wa Jhipego, Dk Albert Komba amethibitisha kutokea kwa wizi huo.

JK ayatoa ya moyoni kuhusu Rais Magufuli kutokwenda Zambia




Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli kuahirisha safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Kikwete amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia tatizo hilo.

Kikwete aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo, amesema misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za kibinadamu.

Kiongozi huyo mstaafu ameyasema hayo  katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22 za watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10 Mafia zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Pwani.

“Ndugu zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya mkoani kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii kutoa pole kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,”amesema.

Ameongeza kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa haya.”

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.

Waziri mkuu: wekeni majina ya Dodoma mjini, Chamwino


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka za serikali za mitaa nchini kuweka haraka majina katika barabara na mitaa katika maeneo yao, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.

Waziri Mkuu pia ameelekeza taasisi za serikali kuzipa kipaumbele kwa Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma wakati wa kutekeleza mpango huo.

“Dodoma na Chamwino ndio yawe maeneo ya kipaumbele wakati wa kutelekeza mradi hiyo kwani serikali imeshabainisha nia yake ya kuhamisha mji mkuu wa nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma,”amesisitiza.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maelekezo hayo jana wakati wa Uzinduzi wa Muongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa pamoja.

Amewataka mawaziri na mamlaka husika kukamilisha kuweka majina ya mitaa na barabara ifikapo Desemba, mwaka huu. Amezitaka taasisi za umma na binafsi, kuweka kipengele cha anwani za makazi ili kutekeleza mpango huo wa maendeleo.

Alizitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Wakala wa Barabara wa Tanzania (Tanroads), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) na Mipango Miji na Mradi wa Kuboresha Miji. Alisema mpango huo mpya utaboresha mpangilio wa miji, utasaidia masuala ya ulinzi na usalama, huduma za kijamii na kuboresha mazingira ya biashara na uchumi nchini.

“Itakuwa rahisi kukusanya kodi za serikali kwa sababu itakuwa rahisi kutambua na kufuatilia walipa kodi katika maeneo yao,"amesema.

Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya Mwaka 2003 na Azimio la Umoja wa Posta Duniani (UPU) lililofikiwa Doha, Qatar mwaka 2012, lililotaka nchi zote duniani kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa na anuani. Kamu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Christine Mndeme alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa mamlaka za Dodoma, zimeanza kutekeleza mpango huo wa kuweka anuani katika mitaani na kwenye barabara za mji huo mkuu.

“Mpango wetu Dodoma ni kuipa mitaa na barabara majina ya viongozi waliohai na waliokwishafariki kutokana na mchango wao hapa nchini kama vile Pius Msekwa, Job Lusinde, Hayati Rashid Kawawa na George Kahama,” alisema Mndeme.

Nchini Tanzania mradi wa majaribio, ulianzia Mkoa wa Dar es Salaam na Arusha na baadaye ulifuatia Mkoa wa Dodoma na mpango ni kukamilika Juni, 2018.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania profesa Beno Ndulu atoa taarifa kuhusu hali halisi ya uchumi Tanzania




1.0    Hali ya Uchumi wa tanzani


1.1  Ukuaji wa Uchumi


Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 1).


Kielelezo Na. 1: Mwenendo wa Ukuaji wa Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)


Chanzo: NBS, Ukokotoaji - Benki Kuu



Shughuli zilizochangia ukuaji huu wa uchumi kwa kiasi kikubwa ni pamoja na kilimo (asilimia 11.7), biashara (asilimia 10.6), uchukuzi (asilimia 10.1), sekta ya fedha (asilimia 10.1) na mawasiliano (asilimia 10.0). Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ni sekta ya fedha (asilimia 13.5), mawasiliano (asilimia 13.4), na utawala wa umma (asilimia 10.2) (Kielelezo Na. 2).


Kielelezo Na. 2a: Ukuaji wa Shughuli Mbalimbali za Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)







Kielelezo Na. 2b: Mchango wa Shughuli Mbalimbali za Uchumi katika Ukuaji wa Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)







1.2 Matazamio ya Ukuaji wa Uchumi Mwaka 2016


Kwa kuangalia viashiria mbalimbali inaonekana kuwa hali ya uchumi wetu itaendelea kuimarika katika mwaka 2016. Kwa mfano:



Uzalishaji wa umeme nchini katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 umeongezeka kwa asilimia 14.5 kufikia kWh milioni 3,454.2 ikilinganishwa na kWh milioni 3,016.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Ongezeko hili limetokana kwa kiasi kikubwa na jitihada za serikali katika kutumia nishati ya gesi kwenye uzalishaji umeme kufuatia kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam pamoja na mtambo wa Kinyerezi I.

 Umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya gesi umeongezeka kwa asilimia 52.2 (Kielelezo Na. 3). Hali hii itasaidia kuongezeka kwa uzalishaji viwandani pamoja na sekta nyingine zinazotegemea nishati ya umeme, na hivyo kuchangia katika kuongeza kwa pato la Taifa.  Gharama ya umeme itashuka pia.



Kielelezo Na. 3: Mwenendo wa Uzalishaji Umeme Nchini

Januari - Juni



Uzalishaji wa saruji katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 umeongezeka kwa asilimia 7 kufikia tani elfu 725.4 ikilinganishwa na tani elfu 680.1 zilizozalishwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2015. Hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la uzalishaji wa kampuni ya Dangote ambayo ina uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka (Kielelezo Na. 4).  

Ni matarajio yetu kwamba uzalishaji katika kiwanda cha Dangote chenye uwezo wa tani milioni 3 na katika viwanda vingine vya saruji nchini utaongezeka katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2016 kwani mahitaji ya nchi bado ni makubwa kuliko uzalishaji ulivyo hivi sasa.  Aidha kuna miradi mikubwa mingi ya hapo baadaye itakayokuwa na mahitaji makubwa ya saruji kama vile mradi wa reli ya kati.



Kielelezo Na. 4: Mwenendo wa Uzalishaji Sarujii

Januari – Machi



Uagizaji wa malighafi za viwandanikutoka nje umeongezeka kwa asilimia 19.4 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 kufikia Dola za Marekani milioni 520.2 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 5). 

Hali hii imechangiwa na kuendelea kukua kwa shughuli za uzalishaji viwandani. Ukuaji huu utaendelea kuchangia pato la Taifa kiujumla katika mwaka 2016.



Kielelezo Na. 5: Mwenendo wa Uagizaji Malighafi za Viwandani

Januari – Juni



Mauzo ya bidhaa za viwanda nje ya nchiyameendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 mauzo ya bidhaa nje ya nchi yalifikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 728.5, sawa na ongezeko la asilimia 15.6 ikilinganishwa na kiasi kilichouzwa kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 6).



Kielelezo Na. 6: Mwenendo wa Uuzaji wa Bidhaa za Viwandani Nje ya Nchi

Januari – Juni




Makusanyo ya kodi katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 yameendelea kuwa bora zaidi ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka 2015, ikiashiria kuimarika kwa usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuendelea kuimarika kwa hali ya

uchumi wa nchi.



Mikopo itolewayo na mabenki ya biashara kwenye sekta binafsi, imeendelea kuongezeka kwa kasi ya kuridhisha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 kwa Shilingi bilioni 1,167.2, japo ni pungufu ikilinganishwa na ongezeko la Shilingi bilioni 1,577.5 la mwaka 2015. Ongezeko hili linaendana na malengo ya sera ya mwaka 2015/16 ambayo yanajumuisha utulivu wa mfumuko wa bei (Kielelezo Na. 7).



Kielelezo Na. 7: Mwenendo wa Ongezeko la Mikopo kwa Sekta Binafsi

Januari - Juni



Chanzo: Benki kuu



Miradi mikubwa ya viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarijiwa kuanza kazi siku za usoni itachangia katika kuimarisha uchumi. Hii ni pamoja na:

  1. Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha  kisasa (Standard gauge)
  2. Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo litahusu vile vile upanuzi wa bandari  ya Tanga
  3. Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini – itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika
  4. Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.
  5. Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya n.k.
  6. Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha mazao ya nafaka kwa wingi.
  7. Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara ambacho kipo mbioni kuzalisha kulingana na uwezo wake (full capacity);
  8. Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea
  9. Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi - kinajengwa
  10. Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani ambacho kiko mbioni kukamilika.


Kwa kuzingatia mwenendo wa viashiria mbalimbali vya shughuli za uchumi, ni dhahiri kwamba hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri na inatoa matumaini makubwa kwamba shughuli halali za kiuchumi zinaendelea kutekelezwa kama ilivyotarajiwa hapo awali hivyo lengo la ukuaji wa pato la Taifa la asilimia 7.2 kwa mwaka 2016 litafanikiwa. 

Hii inachangiwa pia na ukweli kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuimarisha uchumi endelevu usiokuwa na mianya ya rushwa; usimamizi thabiti wa rasilimali za umma; na ujenzi wa miundombinu bora kwa lengo la kujenga uchumi wa viwanda chini ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.



1.3  Mwenendowa Mfumuko wa bei


Wastani wa mfumuko wa bei katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016 umeendelea kuwa mzuri ukiendelea kushuka hadi kufikia asilimia 5.5 mwezi Juni 2016 na asilimia 4.9 mwezi Agosti 2016 kutoka asilimia 6.8 mwezi Desemba 2015 (Kielelezo Na. 8). 

Kushuka huku kwa wastani wa mfumuko wa bei kulichangiwa zaidi na bei zisizojumuisha bei za vyakula na nishati (core inflation) zikifuatiwa na zile za nishati na mafuta. Wastani wa mfumuko wa bei usiojumuisha bei za vyakula na nishati (core inflation), ambao ni kiashiria sahihi zaidi cha utekelezaji wa sera ya fedha, umeendelea kubaki katika viwango vya chini (wastani wa asilimia 2.8 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2016) kutokana na hatua mbalimbali thabiti za sera ya fedha na bajeti katika kudhibiti ujazi wa fedha na ukwasi katika uchumi.



Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea kubakia katika viwango vya tarakimu moja katika siku zijazo na kufikia lengo la muda wa kati la asilimia 5. 

Hii ni kutokana na matarajio ya hali nzuri ya hewa itakayochangia kupungua kwa kasi ya kuongezeka kwa bei za vyakula, pamoja na ongezeko dogo la bei ya mafuta nchini inayotokana na mwenendo wa bei ya mafuta katika soko la dunia, na utulivu wa thamani ya Shilingi. 

Pia, mwendelezo wa sera thabiti ya fedha, usimamizi mzuri wa matumizi na mapato ya Serikali, na upatikanaji wa umeme utokanao na gesi ambao utasaidia kupunguza gharama za uzalishaji viwandani vitaendelea kuimarisha utulivu wa mfumuko wa bei. 

Hata hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa upungufu wa mavuno ya mazao ya chakula uliojitokeza kwa baadhi ya nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika unaweza kusababisha shinikizo la mfumuko wa bei katika siku za usoni.


Kielelezo Na. 8: Mwenendo wa Mfumuko wa Bei (Badiliko la Miezi 12)


Chanzo: Benki kuu


1.4 Utekelezaji wa Sera ya Fedha


Ili kufikia malengo ya serikali ya kuimarisha uchumi na kudumisha utulivu wa mfumuko wa bei, Benki Kuu imeendelea kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti ukwasi ili uendane na mahitaji halisi ya uchumi. Ongezeko la fedha taslimu (reserve money) ambacho ni kipimo cha ukwasi kwenye uchumi limeendelea kubakia ndani ya malengo katika kipindi chote cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016. 

Katika kipindi hicho ujazi wa fedha taslimu ulikua kwa wastani wa asilimia 11.6; wakati ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ulikua kwa wastani wa asilimia 14.4, ikiwa ni ndani ya makadirio ya ukuaji usiozidi asilimia 16.0 kwa mwaka 2015/16.

Wakati huohuo sekta ya fedha imeendelea kuchangia ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kasi nzuri ya kutoa mikopo kwa wakati na kwa kiwango cha kutosha. Mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa wastani wa asilimia 21.3 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, sawa na kiwango kilichopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015. 

Mikopo mingi kwa sekta binafsi ilielekezwa kwenye shughuli za biashara kwa wastani wa asilimia 19.3 ya jumla ya mikopo yote, shughuli za watu binafsi wastani wa asilimia 19.0, uzalishaji viwandani wastani wa asilimia 10.6, uchukuzi na mawasiliano wastani wa asilimia 7.9, na shughuli za kilimo asilimia 7.8.

Benki Kuu inaendelea kutekeleza sera madhubuti ya fedha kwa kutumia zana mbalimbali za sera ili kuhakikisha kwamba mahitaji ya ukwasi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi yanafikiwa bila ya kuchochea mfumuko wa bei.



1.5     Mwenendo wa Thamani ya Shilingi ya Tanzania


Thamani ya Shilingi imeendelea kuwa tulivu katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, kufuatia hatua mbalimbali za sera ya fedha zilizochukuliwa na Benki Kuu katika kusimamia hali ya ukwasi kwenye uchumi pamoja na mwenendo wa uchumi ndani na nje ya nchi. 

Kuimarika kwa sekta ya nje kulikotokana na ongezeko la mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kupungua kwa thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kumechangia katika utulivu wa thamani ya shilingi. 

Kupungua kwa thamani ya bidhaa kutoka nje kumechangiwa zaidi na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2016 Shilingi imekuwa ikibadilishwa kwa kati shilingi 2,180 hadi 2,190 kwa dola moja ya Marekani (Kielelezo Na. 9).



Kielelezo Na. 9: Mwenendo wa Thamani ya Shilingi



Chanzo:Benki kuu



Hali hii ya utulivu wa thamani ya Shilingi kwenye soko huru la fedha inadhihirisha kuwa sera thabiti za uchumi pamoja na mwenendo mzuri wa urari wa mapato ya fedha za kigeni, ndio jawabu la kulinda thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni na sio kudhibiti matumizi ya dola kama ambayo imekuwa ikidaiwa mara kwa mara. 

Nchi zenye udhibiti mkubwa wa fedha za kigeni mfano Afrika Kusini imeshuhudia kuyumba sana kwa thamani ya fedha yake tofauti na shilingi ya Tanzania.

Hivyo nguvu kubwa inapaswa ielekezwe katika kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta mbalimbali hususan zile zinazoboresha urari wa malipo ya nje kama vile utalii, viwanda, uchimbaji madini, kilimo n.k. Ikumbukwe kuwa uhuru wa kumiliki na kutumia fedha za kigeni nchini Tanzania uliwekwa kama hatua ya kukabiliana na hali iliyokuwepo miaka ya 1980 ya kuadimika sana kwa fedha za kigeni na mchango wa uhuru huo tumeuona katika kuwepo kwa fedha za kigeni za kutosha. 

Nchi zilizojaribu kuondoa uhuru huo, mfano Zambia, zimeshuhudia kutoweka kwa fedha za kigeni kwenda nje. Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhimiza na kuweka mazingira mazuri ya uzalishaji na kuondokana na fikra za kuingilia soko huru kama jawabu la kulinda thamani ya shilingi.


1.6  Mwenendo wa Sekta ya Kibenki


Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, sekta ya kibenki imeendelea kukua ikichangiwa na uanzishwaji wa taasisi mpya za kifedha ikiwemo Benki ya Waalimu Tanzania (Mwalimu Commercial Bank Plc) na Canara Bank (Tanzania) Limited. Takwimu za awali za tathmini ya hali ya mabenki yetu zinaonesha kuwa mabenki yetu ni imara na salama, yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Kufikia mwezi Juni 2016, kulikuwa na jumla ya benki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu zipatazo 65 zenye matawi 739 nchini kote.

Kiwango cha mitaji kikilinganishwa na mali iliyowekezwa (total capital to total risk weighted assets and off-balance sheet exposures) kilikuwa asilimia 17.17 kikilinganishwa na kiwango cha chini kinachotakiwa kisheria cha asilimia 12.0. Hali ya ukwasi ambayo hupimwa kwa kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities) ulikuwa asilimia 37.03 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20 (Jedwali Na. 1).

Amana za wateja katika mabenki zilipungua kutoka shilingi trilioni 20.52 mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi trilioni 20.24 mwezi June 2016. Miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa amana kwenye mabenki ni pamoja na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu ya Tanzania. Aidha mikopo (loans and overdafts) iliongezeka kutoka shilingi trilioni 15.28 mwezi Desemba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 15.67 mwezi Juni 2016.

Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wasiofikiwa na mabenki umeendelea kuongezeka kutokana na ubunifu wa mipango ya utoaji wa huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mikononi, pamoja na huduma za uwakala wa mabenki (agent banking services).


Kiujumla kwa kuangalia viashiria vyote vya msingi hali ya ukwasi wa benki imeendelea kuwa ya kuridhisha. Benki Kuu katika kusimamia majukumu yake ya kisera, imeendelea kutoa mikopo ya muda mfupi kupitia “reverse repos” pamoja na kununua fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya bidhaa nje ya nchi kutoka kwenye benki. Kwa viashiria hivi ni dhahiri kwamba uamuzi wa serikali wa kuagiza fedha zake zote kuwekwa kwenye akaunti maalum Benki Kuu hakujasababisha sekta ya kibenki kutokuwa na ukwasi wa kutosha na kuacha kukopesha kwa sekta binafsi kama inavyofikiriwa na baadhi yetu.



Ni vyema jamii ya Watanzania ikafahamu kwamba akaunti ambazo fedha za mashirika zimehamishiwa Benki Kuu ni akaunti za kukusanya mapato tu. Akaunti za matumizi bado ziko katika benki za biashara ili kuyawezesha mashirika kufanya malipo kupitia akaunti hizo. Hivyo, bado benki za biashara ni kiungo muhimu kati ya mashirika ya umma na watoa huduma kwa mashirika hayo. Pia hali ya utoaji mikopo kama tulivyoona awali ni nzuri na watanzania wanaendelea kuhudumiwa na benki zetu kama inavyotarajiwa.



Jedwali Na. 1: Viashiria vya Uimara wa Sekta ya Fedha







1.7 Sekta ya Nje na Akiba ya Fedha za Kigeni


Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje (current account deficit) ilipungua kwa asilimia 61.7 na kufikia nakisi ya dola za Kimarekani milioni 970.4, kutoka nakisi ya dola za Kimarekani milioni 2,532.5 mwaka 2015. Kupungua huko kulitokana zaidi na ongezeko la thamani ya bidhaa za viwandani, mapato yatokanayo na utalii na huduma za usafirishaji nje ya nchi, pamoja na kupungua kwa thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ya nchi hususan bidhaa za mitaji, na bidhaa za matumizi ya kawaida. 

Katika kipindi cha miezi sita iliyoishia Juni 2016, kikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia, thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi ziliongezeka kwa asilimia 14.2 na kufikia dola za Kimarekani milioni 4,473.2 wakati thamani ya bidhaa na huduma toka nje zilipungua kwa asilimia 18.3 na kufikia dola za Kimarekani milioni 5,360.7

Hazina ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuongeza imani kwa wawekezaji katika uchumi wetu; japo kumekuwepo na ucheleweshwaji wa fedha za wahisani na mikopo ya kibiashara kutoka nje ya nchi.

 Hadi mwezi June 2016, akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Kimarekani milioni 3,870.3 ambazo zinatosheleza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4. Wakati huo huo, rasilimali za fedha za kigeni za mabenki (gross foreign assets) zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 835.0

1.8  Deni la Taifa


Deni la Taifa limeendelea kuongezeka na kufikia dola za Kimarekani milioni 20,851 mwishoni mwa mwezi Juni 2016, kutoka dola za Kimarekani milioni 19,861 mwezi Desemba 2015. Deni la nje liliongezeka kwa asilimia 2.6 na kufikia dola za Kimarekani milioni 16,281 mwezi Juni 2016 (sawa na asilimia 77.8 ya deni la taifa), kutoka dola za Kimarekani milioni 15,864 mwezi Desemba 2015. Hii ilitokana na kuongezeka kwa mikopo mipya pamoja na malimbikizo ya malipo ya madeni. 

Katika deni hilo la nje, asilimia 83.4 ni deni la Serikali na taasisi za umma. Pamoja na ongezeko hilo, takwimu zinaonyesha kuwa deni letu bado ni stahimilivu. Kwa mfano, deni la nje kwa thamani ya sasa (Net Present Value) ni karibu ya asilimia 20 ya Pato la Taifa, ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 50 ya Pato la Taifa (Sept-15 DSA). Hii inaonyesha kuwa bado kuna nafasi kubwa ya kukopa bila kuhatarisha ustahimilivu wa deni letu.

Deni la ndani liliongezeka kufikia shilingi bilioni 10,038.4 mwishoni mwa mwezi Juni 2016 kutoka shilingi bilioni 8,597.0 mwezi Desemba 2015.

 Ongezeko hilo lilitokana na Serikali kukopa kupitia dhamana na hati fungani ajili ya kugharamia bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015/16, ikichangiwa pia na kupungua kwa misaada na mikopo kutoka nje.

Jedwali Na 2 linaonyesha vyanzo vya fedha za Serikali na matumizi yake katika kipindi cha miezi 6 kuanzia Januari hadi Juni 2016. Kama inavyoonekana jumla ya mapato ya ndani ilikuwa shilingi bilioni 7,267 wakati matumizi ya kawaida (ukiondoa riba) yalikuwa shilingi bilioni 6,488, hivyo mapato yalitosha kulipia matumizi ya kawaida ya Serikali. Hii ni kuonyesha kwamba madeni ya nje na ndani yalitumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kurejesha madeni yaliyopita.



Jedwali Na. 2: Vyanzo vya Fedha vya Serikali na Matumizi Yake (Shilingi bilioni)

Post Labels