
Jeshi
la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam
limekusanya shilingi milioni 320.2 ambapo fedha hizo ni kutokana na tozo
za makosa ya usalama barabarani.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Kamanda wa wa polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema fedha hizo ni
kutokana na makosa 10,676 ambayo yamefanywa na watumiaji wa vyombo vya
moto.
‘’Toka
tarehe 25 hadi tarehe 28 tumefanikiwa kukusanya kiasi nilichotaja
ambapo makosa mengi ya madereva wa bodaboda tumeanza kuona kwamba
tunapowatoza faini ya elfu 30 au 60 haiwapi fundisho lolote ndiyo maana
tumekuwa tukiwapeleka mahakamani ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani’’ Alisema Kamanda Sirro
Aidha Kamishna Sirro alitumia
wasaa huo kuwataka watanzania kutii sheria bila shurti wanapokuwa
wanatumia vyombo vya moto barabarani na katika maeneo yao ya kuishi.
Post a Comment Blogger Facebook