0
Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limesusa kusafirisha mwili wa askari polisi, Konstebo Nobart Chacha (25) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akifanya ujambazi.

Kwa mujibu wa habari zilipatikana, jukumu la kusafirisha mwili wa marehermu huyo limechukuliwa na marafiki wa chama cha watu wanaotoka mkoani Mara wambao wanaishi Mkoa wa Katavi.

Mmoja wa wajumbe katika chama hicho, Julius Marwa alisema kuwa wamelazimika kusafirisha mwili wa marehemu baada ya polisi kukataa kusafirisha na kushiriki mazishi kwa madai kuwa kitendo alichofanya askari huyo tayari amejifukuzisha kazi.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema kwa taratibu za kijeshi mwili wake haustahili kupewa heshima yoyote, ikiwa pamoja na kusafirishwa kwa kuwa tayari amejifukuzisha kazi kwa aibu na fedheha kubwa.

Askari Polisi huyo wa kituo cha polisi wilaya ya Mpanda, aliuawa juzi usiku akiwa katika harakati za kufanya ujambazi nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Daniel John katika kijiji cha Ibindi  kilichopo Kata ya Machimboni, Wilayani Mlele.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Machimboni, Raphael Kalinga, askari huyo akiwa na kundi la wenzake ambao idadi yao hakufahamika mara moja, walifika kijijini hapo kwa lengo la kumvamia na kumpora kwa kutumia silaha mfanya biashara huyo wa Madini ya dhahabu na mashine za kusaga.

Inadaiwa kuwa majambazi hao walivunja mlango kuingia ndani ya nyumba hiyo yakimwamuru mfanyabiashara huyo kukaa kimya, lakini hakutii agizo hilo ambapo alichukua bunduki yake na kufyatua risasi ambayo ilimpiga askari huyo kifuani na mgongoni na kufa hapo hapo.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top