0
MTABIRI maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ameibuka na kusema kwamba utabiri aliowahi kuutoa kwamba kuna mgombea urais atafariki, bado upo palepale.

Maalim Hassan alisema kuugua ghafla kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ni dalili tu za ukamilifu wa utabiri wake lakini suala la mgombea urais kudondoka na kufa akiwa jukwaani akifanya kampeni linakuja.

“Kuugua kwa Mbowe hakujatimiza utabiri kama ulivyosema ila hizo ni dalili tu lakini kuna mgombea atadondoka jukwaani akifanya kampeni na atakufa lakini haioneshi ni wa chama gani na hii ni kutokana tu na mwaka huu ulivyoanza kinyota,” alisema mtabiri huyo.

Mwaka huu mwanzoni mtabiri huyo alitoa utabiri uliyoonyesha kwamba kutakuwa na kifo cha mgombea urais pamoja na mambo mengine ikiwemo kuibuka kwa magonjwa ya kushangaza

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top