Mtazamo wangu kisiasa juu ya sakata linaloendelea katika nchi yetu kutokana na kitendo cha mhe. Edward lowasa kuhama chama kutoka CCM na kwenda CHADEMA, nadhani naweza kuwa tofauti na watu wengi sana hasa wanachama wa chadema, ni wazi kitendo cha mbunge wa monduli bwana edward lowasa kuhamiachadema nadhani kimebadilisha mtazamo mkubwa katika swala la siasa la Tanzania.
mbunge huyo aliyetangaza kujiunga na ukawa siku ya jumatatu tarehe 27. mgombea huyo alipokelewa na baadhi ya viongozi wa ukawa akiwepo Mhe. James mbatia kutoka NCCR-mageuzi, Mhe. Freeman Mbowe kutoka CHADEMA, mwenyekiti wa CUF prof Ibrahim lipumba, mwenyekiti wa NDL Dkt Emanuel Makaidi, na wanachama wengi kutoka vyama mbalimbali vinavounda UKAWA.
Kiukweli moja ya vitu vilivoipa umaarufu chadema ni uhodari wao wa kukemea maovu na uchafu unaofanywa na viongozi na hata watu ambao ni wanachama cha chadema ili kuhakikisha chama kinaenda sawa na ilani za chama. ni wazi sio kwamba kila mwanachama wa chadema ameridhika na uhamiaji huo kutokana na mazingira ambayo mhe. edward lowasa ametumia kuingiliakwenye chama hicho.
maswali mengi watu wanajiuliza
Je nguvu ya chama na ya lowasa vitalingana?, kiukweli mhe. Edward lowasa ananguvu kubwa ya ushawishi pia na nguvu ya kiuchumi ni wazi kitendo cha yeye kuhamia chadema ameisha chukua imani ya wanachama wa chadema. na kuna baadhi ya wanachama ambao walikua waaminifu kwenye chama wataondoka kutokana na kutokuridhika na maamuzi hayo. mhe. edward lowasa ananguvu kubwa kwenye chama cha chadema kwa sasa tofauti na watu wengine wote waliowahi kukiongoza chama hicho.
Nini sababu ya kuhama kwa lowasa? hili ni swali ambalo wengi wanatakiwa kujiuliza kwanini mhe. edward lowasa alihama ccm kuja chadema na kwanini amehama sasa. ni wengi tunajua tatizo kubwa la ccm ni mfumo ambao umekaa kifisadi lakini huo huo mfumo ndio ambao mhe. Edward lowasa alitangaza nia mwezi mmoja uliopita akitaka kuomgoza kwenye huohuo mfumo na baada ya kukatwa ndipo akahamia chadema. sidhani kama baada ya kukatwa ndipo aligundua mfumo umebadilika.
TAFAKARI
by doc Kalinga
Post a Comment Blogger Facebook