Kwa jinsi teknolojia ilivyokua watu wanapaswa kuwa makini sana kwa simu wanazopiga na maneno wanayoongea
Nuh Mziwanda amejikuta akiumbuka vibaya baada ya Wema Sepetu kuvujisha sauti anayosikika akimtongoza mrembo huyo. Mazungumzo hayo yanachekesha sana hasa kutokana na mistari anayompa Miss Tanzania huyo wa zamani. Haya ni maongezi yaliyofanyika mwezi June (siku moja kabla ya KTMA 2015). Tunafahamu wapo wasioweza kusikiliza clip yote hivyo tumekuandikia mazungumzo hayo.
Nuh Mziwanda: Kuna ua moja lilikuwa limefuatwa sana na vipepeo pamoja na nyuki kwaajili ya kutengeneza asali, unanielewa?
Wema Sepetu: Yeah
Nuh: Kwahiyo lile ua yule mama alikuwa anapenda sana kulitunza na kulifanya special kuliko maua yote. Mama yupo radhi maua yote yakauke lakini lile ua alimwagilie maji ili likue.
Wema: Hilo ua lilikuwa nyumbani kwenu?
Nuh Mziwanda: Yeah nyumbani kwetu Ilala Posta, alipokulia Shetta kwa akina Shetta pale kwetu hapa. Ua hilo hadi leo hii lipo. Ua ambalo mama analipenda na kulithamini kwakuwa lililikuwa linavutia. Kwahiyo katika kuvutia kwake, vipepeo walikuwa wanalipenda lile ua. Ni mfano wako wewe, you’re so beautiful!
Wema: Thank you lakini unanitafutia matatizo, wewe unataka mimi Shilole anifanye nini? Nuh mbona hivyo?
Nuh Mziwanda: Sijamalizia kuongea! Kwanza wewe ni mwanamke mzuri sana na wa kuvutia na mwanaume akikuona, anatamani aje kwenye ua kwakuwa wewe ni mfano wa ua. Na sisi ni mfano wa vipepeo na mfano wa nyuki.
Wema: Sasa hizo tattoo unazifanya nini?
Nuh: Eeeh!!
Wema: Hizo tattoo zako za Shishi Beibe unazifanya nini?
Nuh: Unajua kila kitu kinatokea kwa sababu kwenye hii dunia. Wema ulikuwa haujui mimi ni nani? Lakini hatujui Mungu alipanga nini kwenye muziki wangu na maisha yangu. Baada ya mimi kuchora tattoo nimejulika mimi ni nani. Kwahiyo namshukuru Mungu sasa hivi mashabiki wangu wanajua kwamba mimi naitwa Nuh! Nina mashabiki wachache lakini hao hao ndo wananifanya mimi niwe Nuh. Naamini nilichora tattoo kwa sababu ya Mungu na kila kitu kinatokeaga kwa sababu. Mimi naishi kama binadamu haya mambo yanatokeaga kwa binadamu yoyote. Vitu vingapi ulikuwa navyo leo hauna? Sisi tunaishi kama binadamu, haya mambo yalikuja na yanaweza kutokea kwa binadamu yoyote. Huwezi kujua mambo mangapi ya kipuuzi umeyafanya katika maisha yako. Lakini unaangalia unafanya nini ili uendelee na maisha, natamani niwe na wewe, natamani uwe mpenzi wangu serious!
Wema: Utanituliza akili yangu na wewe na Shilole itakuwaje mbona unataka kunifanyia vitu vya ajabu vya kunigombanisha mimi na rafiki yangu? Shilole is not my best friend lakini ni mshkaji sawa. Ni msichana ambaye namjua na ni rafiki yangu yaani. Itakuwa vibaya halafu mimi sipendi maneno sawa. Mimi napenda tunakutana mambo poa vipi, everybody is happy. Sasa hapo sasa hivi tunataka kuanza kubadilishana dunia tena. Mimi sipendi Nuh, mimi sipendi maneno na Shilole alishanitamkia na tena alisema mbele yako na umemsikia, kwamba hataki, mimi sitaki tuishi kama washkaji, Nuh unakosea kwa sababu kuna kesho kesho kutwa.
Nuh: Nikwambie kitu Wema?
Wema: Uniambie nini Nuh? Uniambie kitu gani sasa hivi it’s not possible yaAni ni kitu ambacho kipo very impossible. Sio nakuvunja moyo nakwambia kweli, nakwambia ukweli unajua in love sio kila kitu unachokitaka unakipata si unajua hivyo?
Nuh: I know!
Wema: Kwamba katika maisha sio kila kitu unachokitaka utakipata. Basi mimi namheshimu sana Shilole na ninakuheshimu wewe pia. Nimekubali umenipigia simu na umeniambia lakini it’s something ambacho hakiwezekani tokea. Yaani haiwezekani kutokea. Najua sio rahisi ku-accept lakini jitahidi kuikubali kwa sababu ndio hali halisi, haiwezekani icho kitu.
Nuh: Nikwambie kitu?
Wema: Utaniambia kitu gani Nuh na nimeshakwambia kwamba haiwezekani!
Nuh: Kama unanikatisha tamaa kihivyo, unadhani nitakwambia kitu gani?
Wema: Haya kitu gani? Niambie nakusikiliza kitu gani?
Nuh: Kitu ninachotaka nikwambie ndio hicho tu, nothing new, kila siku unatongozwa lakini mimi naongea kwa mapenzi na na kama mwanaume na kwa kujiamini pia. Lakini inawezekana pia nikawa nimekukwaza.
Wema: Hamna haujanikwaza kwa sababu kumwambia mtu hisia zako sio kitu kibaya. Kusema hisia zako it’s not very bad. Tena it’s a very good thing kwa sababu umeshow kitu umekuwa jasiri. Halafu mpaka umenipigia simu na umeniambia yaani umetumia ujasiri sana, unaona so I appreciate it, and thank you. Kupendwa raha lakini unapopenda hapawezekani kwa sababu mimi siwezi siko kwenye nafasi ya kukukubalia what you are talking me. Ushanielewa kwamba nafasi yangu hairuhusu kukubali, kwa sababu moja nakuheshimu wewe kama shemeji yangu, wewe ni shemeji yangu, wewe ni boyfriend wa rafiki yangu. Mimi siko hivyo, mimi sio mtu wa kumchukulia rafiki yangu mwanaume, yaAni siko hivyo!
Nuh: Mimi najua kila kitu, najua nimejichora matatoo, najua ya mwanamke usinijudge kwa yale, ila nijudge kwa akili yako.
Wema: Sikia nikwambie Nuh, apart from everything mimi siwezi kukudanganya. Mimi siwezi kukukataa sijui, yaani kitu itanishusha. Kuingia mabifu na Shilole, unaanza kusikia Wema sasa hivi yupo na bifu na Shilole.
Nuh: Au wewe utatangaza kwa watu?
Wema: Akaa, no hakuna kitu kama hicho. Hakuna kitu ambacho kinafichika kama kuna mapenzi, mapenzi kitu kizito sana.
Nuh: Nikwambie kitu?
Wema: No, Nuh niache nilale, naomba niache nilale naomba niache nilale. Kesho naamka asubuhi sana natakiwa nijiandae na Kilimanjaro, si unaenda kwenye KTMA? .
Nuh: Unajua mimi nafikiria pia akilini mwangu na nina mawazo yangu kama binadamu na kila kitu kinatokea kwenye maisha kama vile nilivyokwambia, kuna vitu vingi vilitokea kwenye maisha yako,lakini inafika wakati unasahau. Na mimi nilifiwa na ndugu zangu lakini nikasahau, kwahiyo vyote vinaweza kutokea.
Wema: No! tutaongea kesho.
Post a Comment Blogger Facebook