0
MAFAHARI wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliusoma ‘mchezo’ mwanzo mwisho, Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao walifika na kukaa meza nyingine.

Habari zinazidi kudai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt tangu ajifungue.
“Yaani kwa kweli hakuna hata mmoja aliyeamini kilichotokea pale kwa kuwa watu wengi wanajua ni marafiki wa damu lakini kiliwashangaza watu, hata kupeana salamu kweli? Kila mmoja aliendelea kufanya kilichompeleka,” kilisema chanzo chetu.

Mpashaji wetu huyo alizidi kumwaga ubuyu kuwa baada ya Aunt kumaliza kula Ice Cream na kundi lake, waliinuka na kuondoka zao na kumuacha Wema na marafiki zake.
Baada ya gazeti hili kupata habari hiyo lilimtafuta Aunt ili aweze kuzungumzia kitendo hicho na bifu lao ambapo alikiri kuonana na Wema lakini alisema kuwa kila mmoja alikuwa na shuguli zake eneo hilo.

“Jamani unajua kila mtu alienda kwa ajili ya kazi zake na ndiyo kama tulivyokutana kila mmoja alikuwa yupo na taratibu zake, sioni kama ni bifu, sina comment,” alisema Aunt.
Jitihada za kumpata Wema ambaye ametangaza nia ya kugombea ubunge mkoani Singida kupitia viti maalum ili aweze kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba lakini hivi karibuni alizungumza na mwanahabari wetu na kukiri kuwa kuna tatizo kati yao lakini hakutaka kuliweka wazi

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top