sitti mtemvu |
HAPATOSHI! Vita kali ya kugombea ubunge imezuka katika familia ya Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kufuatia watoto wake wawili, Lulu na Sitti Abbasi Mtemvu ambao kwa pamoja wamechukua fomu ya kugombea ubunge viti maalum kupitia kundi la umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Morogoro.
Mashuhuda wa tukio hilo walipenyeza ubuyu kuwa Lulu ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua fomu hiyo na siku iliyofuata Sitti aliyeongozana na mama yake mzazi Mariam Mtemvu walitinga kwenye ofisi hizo na kuchukua fomu hiyo huku mama yake akibeba jukumu la kupiga picha za tukio hilo.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, lgnas Said Kinywa alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa kigezo kikuu cha nafasi hiyo ni kwa mwanachama kuwa na kadi na kutozidi umri wa miaka 30.
Lulu anayeishi maeneo ya Kiwanja cha Ndege alithibitisha kuchukua fomu na mdogo wake, akidai ni demokrasia mpya katika familia yao, lakini Sitti aliyeachia ngazi ya umalkia wa urembo nchini (mwaka 2014) kwa kashfa ya kudanganya umri hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita bila kupokelewa.
Source GPL
Post a Comment Blogger Facebook