Tume ya Uchaguzi (NEC) imewaengua wagombea
urais wa vyama vya Ada/Tadea, DP, CCK na AFP leo kwa maelezo kuwa
wamekosa vigezo vya kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi hapa nchini.
Kwa
mantiki hiyo, Mchungaji Christopher Mtikila (DP), Godfrey Malissa (CCK)
na John Chipaka (Ada-Tadea) hawatashiriki katika kinyang’anyiro hicho
baada ya fomu zao kuonekana kuwa zina kasoro huku mgombea urais wa AFP,
Omari Sombi akiungana na wanasiasa hao kutogombea baada ya kushindwa
kurejesha fomu ya urais.
Kwa mujibu
wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, wagombea wa vyama vinane kati
ya 12 vilivyochukua fomu, wamekidhi matakwa ya sheria ya mchakato huo,
hivyo wanaruhusiwa kuanza kampeni rasmi kesho.
Amewataja
wagombea waliopitishwa na NEC ni Dk. John Magufuli (CCM), Edward
Lowassa (Chadema), Fahmi Dovutwa (UPDP), Macmillan Lyimo (TLP) na Chief
Lutalosa Yemba (ADC).
Wengine ni Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) na Hashimu Rungwe (Chaumma) na Malik Kasambala (NRA).
Post a Comment Blogger Facebook