0
Dar es Salaam. Kama alivyowashangaza wengi pale alipojitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais Mei 29 mwaka huu, ndivyo Dk John Magufuli alivyowashangaza tena jana kufikia hatua hii ya tano bora.
Bila makeke, majivuno wala majigambo, Magufuli ambaye ni waziri wa ujenzi alipochukua fomu alisema tu kuwa kipaumbelea chake ni kutekeleza ilani ya uchagzi ya CCM.
Hata katika safari yake ya kusaka wadhamini mikoani, mbunge huyo wa Chato alikwenda kimya kimya, bila mbwembwe, ahadi wala kukusanya mashabiki.
Bila hiyo ndiyo siri yake ya ushindi, alihofia kukatwa mapema kwa kukiuka masharti ya chama, kama ilivyowatokea wengine.
Hata kabla hajachukua fomu, Dk Magufuli hakuwahi kutangaza nia yake ya kuwania urais, hadi alipoibuka ghafla na papo hapo akapenya hadi hatua hii muhimu, hadi alipolidokeza gazeti hili mjini Dodoma.
“Swali hili nimeulizwa mara nyingi. Mara zote nimekataa kulijibu kwa sababu katika chama chetu (CCM) kuna utaratibu wake wa namna ya kuomba nafasi ya uongozi. Muda ulikuwa haujawadia.
“Lakini utakumbuka wiki hii hapa hapa Dodoma, vikao vya juu vya chama chetu vimetoa ratiba kwa wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali kujitokeza. Kwa maana hiyo sasa niko huru kujibu swali lako kwa kusema rasmi ‘nitagombea urais’.
“Nafanya hivyo kwa sababu naamini ninazo sifa za kuchagua na kuchaguliwa kama mwanachama wa CCM kwa nafasi yoyote inayojitokeza kulingana na Katiba ya chama chetu na pia Katiba ya nchi,” alisema Dk Magufuli.
Pamoja na kutokuwa na papara za kutangaza nia wala kuanza kupitapita kwa wanachama kutafuta kuungwa mkono, Dk Magufuli alikuwa vinywani mwa watu wengi, ndani na nje ya CCM, wakisema akiteuliwa anaweza kuleta ushindani dhidi ya upinzani.
Waziri huyo wa muda mrefu na maarufu kwa kumbukumbu na kukariri takwimu mbalimbali, kila wizara anayokwenda inageuka maarufu na kuanza kusikika, lakini kazi kubwa inayomweka kwenye mwanga wa kisiasa nap engine hata kumfikisha katika hatua hii ni wizara ya Ujenzi na hasa usimamizi wa ujenzi wa miundombinu.
Dk Magufuli alizaliwa katika Kijiji cha Rubambangwe kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita, ndipo unapoweza kukutana na wananchi ambao wanafahamu maisha yake ya ujana na hatua alizopita hadi hadi hatua ya leo.
Kuna simulizi za kusisimua kuhusu maisha ya Magufuli ambaye wananchi wengi wa jimbo lake wanamtumia kama alama ya ushindi, akihusishwa na mafanikio ya kujitenga kutoka Wilaya ya Biharamulo hadi wakapata jimbo na hatimaye Wilaya

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top