0

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Aunty Ezekiel akiwa na mzazi mwenzake Mose Iyobo
msanii wa filamu nchini Tanzania, Aunty Ezekiel, amefunguka na kudai kuwa haoni kama ni tatizo kuchora tattoo ya mtoto wake Cookie na mzazi mwenzake Mose Iyobo katika mwili wake.
Akihojiwa baada ya kuchora hina yenye jina la mtoto wake na mpenzi wake Mose Iyobo, amesema kuwa amechora hivyo katika kusherehekea sherehe ya mtoto wake ambaye ametimiza siku 40 leo tangu kuzaliwa kwake.
Amekiri kuwa akipata mtu anayejua kuchora vizuri tattoo atachora majina hayo kama ambavyo yameonekana kwenye mchoro wa hina.
Alipoulizwa kuhusu ndoa yake aliyofunga na tattoo hiyo ambayo anataka kuchora, amesema kuwa hayo mambo hapendi kuongelea kwa sasa na kudai kuwa anachora kwa kuwa ni jina la mtoto wake na mzazi mwenzake hivyo haoni kama ni ajabu kufanya hivyo.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top