Vyama
vilivyoshindwa kukidhi vigezo ni CCK, TADEA, DP na AFP amabyo imeingia
mitini ambapo akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za tume
baada ya tume kuwatangazia kushindwa kukidhi vigezo mwenyekiti wa CCK Bw
Costantine Akitanda amesema.
Wagombea
urais waliowahi mapema asubuhi ni Mh Edward Lowassa Chadema na Dk Jonh
Magufuli wa CCM ambapo kwa nyakati tofauti waliowasili ofisi hizo za
tume wakiwa na wapambe wao wachache na mara baada ya kuidhinishwa na
mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi wakapata fursa ya kuzungumza na
waandishi wa habari.
Wagombea
wengine waliofika majira ya mchana ni mgombea urais kupitia TLP
Maxmilian Lyimo na mgombea urais kupitia ACT Bi Anna Mghwira ambaye ni
mwanamke pekee aliyeingia katika kinyang'anyiro hicho kwa uchaguzi wa
mwaka huu ambaye chama chake kimemteua siku chache kabla ya ukomo wa
kurudisha fomu lakini pia kimevunja rekodi kwa kutafuta wadhamini kwa
siku moja na hatimaye kukidhi vigezo vya tume.
Katika
zoezi hilo vituko vya hapa na pale navyo havikukosekana katika ofisi za
tume ya uchaguzi baada ya mgombea urais kupitia tiketi ya chauma kufika
katika ofisi hizo na kujikuta akiwa hana picha hivyo kulazimika kurudi
nyumbani kuzifuata huku akirudi dakika za majeruhi lakini pia wapo
walioelezea changamoto walizokumbana nazo wakati wa kutafuta wadhamini.
Post a Comment Blogger Facebook