0
Wakati Watanzania tukiendelea kupata matumaini kwa kuona idadi ya wasanii wetu inaongezeka katika nominations za tuzo za kimataifa, namba ya wasanii wanaofanikiwa kupata collabo kubwa za kimataifa nayo inazidi kuongezeka.

Baada ya kufanya collabo na Diamond ‘Number 1 remix’ ambayo ilimuongezea mashabiki wa Bongo, muimbaji wa Nigeria, Davido amethibitisha kuwa amefanya collabo na msanii mwingine mkubwa wa Tanzania, naye si mwingine bali ni Alikiba a.k.a King Kiba.

Akizungumza na Ayo TV katika Red Carpet ya tuzo za MAMA, Davido hakutoa maelezo mengi juu ya collabo hiyo zaidi ya kusema kuwa itatoka hivi karibuni.

“I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy” alisema Davido.

Tunaisubiri kwa hamu collabo hiyo.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top