0
Msanii wa Nigeria, Davido ameelezea mapenzi aliyonayo kwa nchi ya Tanzania kutokana na jinsi mashabiki wa TZ wanavyompa sapoti.

Davido amesema kuwa Tanzania anapachukulia kama nyumbani, baada ya Nigeria.

Mshindi huyo wa tuzo ya 2015 MAMA Best Male, amesema kuwa mapokezi aliyoyapata siku alipokuja nchini kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta, pamoja na sapoti anayoendelea kuipata vimemfanya apathamini Tanzania na kupaona ni kama nyumbani (second home), baada ya Nigeria.

Akizungumza na Ayo Tv mjini Durban, Davido amesema kuwa hiyo ndio sababu iliyompelekea kupost bendera ya Tanzania Instagram wiki kadhaa zilizopita, kama shukrani.

“The first time I ever went to Tanzania from when I left , I said from today Tanzania is my second home, that’s why I put the picture, and I get a lot of support from Tanzania too, so I was like showing gratitude.” Maneno ya David Adeleke ambaye ni baba wa mtoto mmoja.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top