0

Jengo la shule ya msingi Donyonaado

Na Woinde Shizza,Monduli

Wakati shule nyingi nchini zinafunguliwa baada kumalizika kwa likizo
Wanakijiji wa kijiji cha Donyonaado kilichopo wilaya ya Monduli mkoani
Arusha wameeleza wasi wasi juu ya uchakavu wa jengo la shule ya Msingi
Idonyonaado huenda linaweza kuanguka na kusababisha maafa kwa
wanafunzi.

 Shule hiyo iliyoko umbali wa kilomita 64  kutoka Monduli mjini
iliyojengwa kwa udongo na mawe na wanakijiji waliojitoa haina milango
na madirisha hivyo wanafunzi kupata adha ya vumbi na baridi  kali hasa
kipindi cha mvua.

 Wanakijiji hao wamesema kuwa  hali mbaya  ya miundombinu ya shule hiyo
imewafanya wazazi wengi kusita  kuwapeleka watoto mashuleni  hivyo
ameiomba serikali na mashirika binafsi yajitokeze kusaidia kutatua
changamoto hizo.

 Mwenyekiti wa kijiji cha Donyonaado ,Malulu Kutetei amesema kuwa licha
ya changamoto za shule hiyo bado wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa
nyumba bora za walimu pamoja na uhaba wa maji jambo linalokwamisha
maendeleo ya taaluma shuni hapo.

 Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wafugaji la Monduli
Pastodalist Development Initiative (MPDI) ,Erasto Sanare ameeleza
kusikitishwa na changamoto zinazoikabili shule hiyo hivyo kushiriki
katika  ujenzi wa shule ya kudumu ,ameieomba serikali isaidia shule
hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji.

 Licha ya Jamii ya Wafugaji kuamka katika masuala ya elimu tofauti na
miaka iliyopita bado kuna mazingira duni ya elimu ikiwemo kukosekana
kwa shule za kutosha,miundombinu mibovu,uhaba wa maji na vifaa vya
kufundishia na nyumba za walimu

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top