MSANII wa maigizo Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anatarajia kutifuana vilivyo na wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Kinondoni, Emmanuel Makene kwenye kinyanganyiro cha kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Steve, amechukua fomu ya kugombea kiti cha ubunge leo na kuijaza kisha kuirudisha tayari ikiwa imekwisha jazwa.
Wakati akichukua fomu ya kugombea ubunge, Steve alisema haoni sababu ya kiongozi bora kuchukua fomu na kukaa nayo zaidi ya siku mbili hivyo huo ni uzembe kwani yeye amechukua na kurejesha papo hapo.
Hata hivyo, katika uchukuaji fomu hizo alijitokeza wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni, Emmanuel Makene ambaye naye anatarajia kugombea katika Jimbo la Wilaya ya Kinondoni.
Post a Comment Blogger Facebook