CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekanusha
uvumi kuwa kimejiengua na kukisusia kikao kinachoendelea cha Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwa kile kinachodaiwa kina uchu wa
madaraka. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Aidha, CUF imekanusha uvumi kuwa baadhi
ya wananchama na wenyeviti wa CUF kununuliwa na Chama cha Mapinduzi (
CCM), kwa lengo la kuuvuruga umoja wao na kuisambalatisha UKAWA.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambamo kimechukua fursa hiyo kuwaonya waandishi kuandika habari za kweli zinazohusu UKAWA kuliko kuandika habari zinazoweza kupotosha umma.
Sakaya ameendelea kusisitiza kuwa, CUF
haijajiengua na UKAWA, ambamo amebainisha sababu za kutoshiriki katika
kikao cha jana Julai 14,2015 kilichofanyika katika ukumbi wa Collesium
Dar, kumetokana na sababu za kikatiba za ndani ya Chama ambapo jana
walikaa kikao hivyo kupelekea kushindwa kutuma mwakilishi katika kikao
hicho.
“Baada ya kikao cha UKAWA cha Julai 11
mwaka huu CUF tumekuwa na vikao vinavyohusu viongozi wakuu wa Chama
akiwemo Mwenye kiti, manaibu katibu wakuu na wakurugenzi na jana ndo
tulikuwa na kikao na ndio maana hatukuweza kutoka” amesema Sakaya.
“Kutohudhura katika kikao cha jana hakuna
mahusiano yoyote na uvumi na maneno ya chini chini kwa baadhi ya
mitandao ya kijamii yanayopotosha umma”
Kuhusu uvumi unaodai kuwa UKAWA
umeshampitisha mgombea kwa kupiga kura na kwamba baadhi ya magazeti
kumuandika mgombea amesema halina ukweli, taarifa hizo pia zilipelekea
baadhi ya wananchama wa CUF kukusanyika makao makuu ya CUF ili kupata
ufafanuzi zaidi juu ya uvumi huo.
Nae Mkurugenzi mipango na uchaguzi
Shaweji Mketo amesema, kuhusu maneno yanadai kuwa UKAWA ni pasua
kichwa na kwamba unakaribia kuvunjika hayana ukweli isipokuwa
wanafuata katiba ya kila chama ndipo wamtoe mwali atakaye peperusha
bendele ya UKAWA.
Amesema, “niwatoe wasiwasi wananchi na
wapenzi wa UKAWA muondoe hofu tupo imara na tunatarajia baada ya siku
tano kumtangaza mgombea wetu, na kikubwa kinachojadiliwa sasa ni ugawaji
wa majimbo kutokana na kuongezeka kwa majimbo hivyo ni lazma tuyajadili
kwa kina na kujua yupi atachukuwa wapi”
Kuhusu kikao cha Baraza kuu la uongozi
wa kitaifa Mketo amesema, “tunatarajia kufanya kikao cha mwisho Julai
25 mwaka huu ili kupata Baraka ya chombo cha maamuzi kama ambavyo
wezetu wa washiriki wa UKAWA wamekwisha pitia hatua hizo katika vyama
vyao”
Post a Comment Blogger Facebook