0
 
Patashika nguo kuchanika katika uwanja wa Estadio Nacional de Chile Jijini Santiago kati ya timu ya taifa ya argentina wakivaana na wenyeji Chile katika Fainali ya Copa America, wao wakisaka Taji la kwanza baada ya Miaka 22 wakati Chile wakitaka kubeba Kombe lao la kwanza katika Historia yao.
   Mahasimu hawa kutoka bara la amerika ya kusini wamevaana mara 36 na wenyeji kufanikiwa kushinda mechi moja tu katika mechi ya kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2008 njini santiago, katika mechi za Copa america timu ya chile haijawahi pata ushindi dhidi ya Argentina kwenye mechi 24 walizowahi kutana. 
  Timu ya taifa ya Argentina imewahi kutwaa kombe hilo mara 14 na endapo itashinda leo itakua imeifikia timu ya Uruguay ambayo imewah litwaa mara 15, kwa upande wa chile imefika fainali mara 4 na kulikosa kombe hilo.
mchezaji bora duniani mara 4 ambae pia ni kapteni wa timu ya taifa ya Argentina, Leonel Messi anatarajia kuchukua kombe kwa mara ya kwanza akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina. Kwenye Fainali hii, Argentina itaingia ikiwa na Kikosi kamili wakati Chile itamkosa Sentahafu wao Gonzalo Jara ambae amefungiwa Mechi 3 baada ya kunaswa akimsakama Dole makalioni Straika wa Uruguay Edinson Cavani kwenye Mechi ya Robo Fainali.
                   
vikosi vinavyotarajiwa kuwa: Chile: Claudio Bravo; Isla, Medel, Rojas, Albornos; Vidal, Diaz, Aranguiz; Valdivia, Vargas, Sanchez. Argentina: Romero; Zabaleta, Demichelis, Otamendi, Rojo; Biglia, Mascherano, Pastore; Messi, Aguero, Di Maria.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top