0
Dar es Salaam. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) lililoahirishwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani hivi karibuni, utaanza Julai 16 hadi 25 kwa Dar es Salaam na Julai 7 hadi 20 kwa Pwani.

Uboreshaji wa daftari hilo uliahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa kutoka mikoani kwa ajili ya kuongezea ufanisi kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi kubwa ya watu wenye sifa ya kuandikishwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Julius Mallaba kwa vyombo vya habari, iliwataka wananchi wote wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishaji vitakavyokuwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa ili kujiandikisha waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Aliwataja wanaopaswa kuandikishwa ni watu wote waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza miaka 18 ifikapo Oktoba mwaka huu.
Wengine ni waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupatiwa kadi mpya.
Mallaba aliwataja wengine wenye sifa ya kujiandikisha kuwa ni wale wote wenye sifa lakini hawakuwahi kujiandikisha kwenye daftari hilo.
Alisema wale wote wenye kadi za kupigia kura za zamani wanatakiwa kwenda na kadi zao ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao na kadi hizo zitarudishwa NEC na watapata vitambulisho vipya. Pia, wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika vituo vilivyopo ndani ya kata zao.
Mallaba aliwataka pia wananchi wa mikoa hiyo kuhakikisha wanajiandikisha kwani bila kufanya hivyo hawataweza kupiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa ifikapo saa 12:00 jioni.
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top