| Baadhi ya waandishi wa habari na waumini wa Kanisala Ufufuo na Uzima wakifuatilia mkutano wa Askofu wa Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo |
Showing posts with label CHADEMA. Show all posts
Showing posts with label CHADEMA. Show all posts
Wednesday, September 9, 2015
VIDEO YA GWAJIMA AKIMUANIKA DOKTA SLAA
Monday, August 24, 2015
CHADEMA MOROGORO WAGANYIWAKA, KATIBU MAZIMBU AJIUZULU
KUPITISHWA kwa Majina ya Viongozi walioshindwa Kura za Maoni ndani ya
Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema) Morogoro, kumekigawa Chama
hicho na kusababisha, kujiuzulu nyadhifa zao wakipinga Kukatwa kwa Mshindi wao wa Udiwani wa Kata ya Mazimbu, Ebzyan Mokiwa, na kupewa, Mohamed Kilongo (Butelezi).Viongozi waliojiuzulu ni pamoja na Katibu wa Kata ya Mazimbu, Mchungaji James Power Mabula, na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (BAZECHA), Disckson Magambo, waliodai wanajiuzulu kutokana na kutoridhiwa na Maamuzi ya Chadema Wilaya ya Morogoro Mjini.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mchungaji Mabula amethibitisha Kujiuzulu Wadhifa wake wa Ukatibu wa Chadema Mazimbu, akisema kama Mtumishi wa Mungu hawezi kushiriki kuyaishi Maovu na Dhuluma ya aina yoyote ikiwemo Rushwa, isipokuwa kuyakemea kama Maandiko yanavyomuagiza.
“Ni kweli awali nilisema, Nimeitwa kuitumikia Chadema na nitaendelea na kuwa Mwanachama mwaminifu wa Chadema, ila siwezi kushiriki kuwanyima Haki maana, Haki huinua Taifa, dhambi ni aibu ya watu wote, sitaki kubeba dhambi”.alisema Mabula.
Mokiwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa MODECO alikiri kukatwa na Chadema Wilaya na kutoshirikishwa na Timu ya kumnadi Mgombea (Mshindani wake), ambapo yeye alidai, atendelea kuwa Mwanachama na Mwenyekiti wa Mtaa wa MODECO, ila “Nimeumizwa na niliyotendewa”.
Wachambuzi wa Siasa wamesema, Sakata la kukata Majina ya Washindi wa Chadema litakigharimu Chama hicho, na imefahamika kuwa kwenye Kata ya Kihonda Maghorofani, nako Mshindi wao wa Udiwani, Elizeus Rwegasira, alikatwa jina kuwekwa, Gabriel Temba, aliyeshindwa.
Hata hivyo wamedai, CCM imeshajihakikishia Ushindi wa Jimbo la Mvomero kupitia kwa Mgombea wake, Sadiq Murad, hata kama jimbo hilo linaonekana ni Ngome ya Chadema, wanadai kukatwa kwa jina la Mgombea wao aliyegombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema Mvomero, Matokeo Wodern Mang’eta, aliyeasisi Chama hicho huko na kupewa, Mchungaji Osward Mlay, ni Kigezo kikubwa cha Mtiti huo.
Wednesday, August 19, 2015
Walinzi wa CHADEMA Walioongoza Msafara wa Lowassa Jijini Mbeya Watakiwa Kujisalimisha Polisi Kwa Ajili ya Mahojiano
Mnamo
Tarehe 14.08.2015 Mgombea Urais Kwa Tiketi Ya Chadema Alikuja Mkoa Wa
Mbeya Akiwa Ameandamana Na Viongozi Wa Vyama Vya Cuf, Nccr – Mageuzi Na
Nld Kwa Dhumuni La Kumtambulisha Na Kuomba Udhamini Wa Kupeperusha
Bendera Ya Chadema Kwa Nafasi Ya Urais.
Katika
Msafara Wake Kutoka Uwanja Wa Ndege [songwe] Kulionekana Gari Moja
(pichani) Aina Ya Land Cruiser – Pick Up Yenye Rangi Nyeusi Na Ndani
Yake Lilikuwa Limebeba Vijana Ambao Walikuwa Wamevaa Mavazi Meusi, Kofia
– Bereti Nyeusi Na Miwani Nyeusi Na Mabuti.
Watu
Hao Walikuwa Na Muonekano Kama Askari Na Shughuli Waliyokuwa Wakifanya
Ya Kuongoza Msafara, Ulinzi Na Kazi Nyingine Zifanyazo Na Jeshi La
Polisi.
Kutokana Na Muonekano Wao Na Shughuli Walizokuwa Wakizifanya Ilikuwa Ikitafsirika Kuwa Ni Jeshi Lifanyazo Kazi Hizo Ambalo Halikuwa Likifahamika.
Kutokana Na Muonekano Wao Na Shughuli Walizokuwa Wakizifanya Ilikuwa Ikitafsirika Kuwa Ni Jeshi Lifanyazo Kazi Hizo Ambalo Halikuwa Likifahamika.
Kutokana
Na Sintofahamu Hiyo Wananchi Wengi Walikuwa Wakihoji “hilo Ni Jeshi
Gani” Sambamba Na Kutuma Picha Kwa Njia Ya Mtandao Wa Kijamii [whatsapp]
Wakionyesha Wasiwasi Waliokuwa Nao Dhidi Ya Kikundi Hicho.
Kufuatia
Hali Hiyo, Ofisi Ya Mkuu Wa Upelelezi Wa Makosa Ya Jinai Mkoa Wa Mbeya
Ilifungua Jalada La Uchunguzi Ili Kuwapata Vijana Wale Kwa Lengo La
Kuwahoji Na Kukamilisha Upelelezi Ili Jalada Lipelekwe Kwa Mwanasheria
Wa Serikali Kwa Ufafanuzi Wa Kisheria.
Hii Ni Kutokana Na Kuibuka Kwa Makundi Ya Aina Hii Hasa Kwa Vyama Vikubwa Vya Siasa Hapa Nchini.
Katika
Kufanya Ufuatiliaji Huo, Wapo Watu Wawili Walikamatwa Alfajiri Ya Leo
Tarehe 18.08.2015 Kwa Mahojiano Na Baada Ya Maelezo Yao Kuchukuliwa
Walipewa Dhamana.
Baadhi
Ya Viongozi Wao Waliokuja Polisi Wameelezwa Kuhitajika Kwa Vijana Wale
Waliokuwa Katika Gari Lile Ili Wahojiwe Na Kukamilisha Upelelezi Wa
Jalada Hilo Mapema Ili Mwanasheria Wa Serikali Alitolee Mwongozo Wa
Kisheria.
Imesainiwa Na:
[ahmed Z. Msangi – Sacp]
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Imesainiwa Na:
[ahmed Z. Msangi – Sacp]
JESHI LA KAMPENI LA CCM DHIDI YA UKAWA hili hapa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza Kamati ya Kampeni yenye wajumbe 32, wengi wao wakiwa ni wale waliowahi kuvaana na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa katika masuala tofauti.
Lowassa, Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, alijiondoa CCM mwishoni mwa mwezi uliopita na kujiunga na Chadema, ambayo ilimpa fursa ya kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, akiwakilisha vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD.
Tangu ahamie Chadema, Lowassa amekuwa akivuta wafuasi wengi kwenye shughuli za Ukawa, hali inayoashiria uwezekano wa kuwapo kwa upinzani mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Jana katika taarifa yake, CCM haikutoa maelezo mengi kuhusu kamati hiyo zaidi ya kutangaza kuwa itaongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana na kutaja majina ya wajumbe.
“Hii ni kamati ambayo itakuwa inafanya oparations za kila siku,” alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakati akitangaza kamati hiyo jana.
Kinana anajulikana kutokana na kazi aliyoifanya ya kuongoza kampeni kwa mafanikio, akifanikisha ushindi wa marais wawili mwaka 1995, wakati alipoongoza kampeni za Rais Benjamin Mkapa na 2005 wakati Rais Jakaya Kikwete akiingia Ikulu.
Licha ya Nape kutozungumzia majukumu ya kamati hiyo, mmoja wa wajumbe, January Makamba alisema wamejipanga vizuri na mwaka huu watafanya kampeni za kisasa.
“Tumejipanga na namna tunavyojipanga ni siri yetu, ni mambo ya ndani ambayo sisi wenyewe kwenye timu tunayafahamu na hatuwezi kutoa siri hizo kwa kuwa ndizo silaha za maangamizi. Kwa kifupi tutashinda,” alisema naibu waziri huyo wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.
Makamba, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, alisema kampeni za CCM mwaka huu zitakuwa za kisasa zinazoendana na mazingira ya kisiasa ya msimu huu.
“Tumejitayarisha kushinda, juhudi zetu na ari yetu ni kushinda na kampeni zetu zitakuwa za kisasa zaidi,” alisema Makamba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo alitumia mfano wa mpira wa miguu kuelezea ukubwa wa kamati hiyo dhidi ya wapinzani.
“Timu hiyo ya kampeni ni sawa na kuileta Arsenal kuja kucheza na timu ya daraja la tatu. Kwa hiyo katika hali hiyo usiulize matokeo,” alisema Bulembo ambaye alikuwa mdau wa soka kabla ya kuingia kwenye siasa.
Kamati hiyo ina wajumbe ambao walitemwa kwenye mbio za urais ndani ya CCM, wajumbe wa Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, wajumbe ambao walikuwa kambi ya Lowassa alipokuwa kwenye mbio za urais ndani ya chama hicho, wajumbe ambao ni maarufu kwa kurusha vijembe dhidi ya wapinzani na wajumbe ambao walishaweka bayana uhasimu wao na mbunge huyo wa Monduli.
Nape alisema Kinana atasaidiwa na makamu wenyeviti wawili ambao ni Rajabu Luhwavi (Bara) na Vuai Ali Vuai (Zanzibar) ambao pia ni manaibu wake kwenye chama.
Wajumbe ambao ni wale waliotemwa kwenye mbio za urais ni Dk Asha-Rose Migiro, Samuel Sitta, Mwigulu Nchemba, Dk Harrison Mwakyembe, Makamba, Lazaro Nyalandu, Stephen Wasira, Bernard Membe na Makongoro Nyerere.
Pamoja na kutopitishwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, makada hao wamekuwa wakieleza kuwa hawawezi kuhama chama kama alivyofanya Lowassa na watakuwa wakionyesha kuwa wamevunja makundi kwa kushiriki kumpigia kampeni Dk Magufuli.
Kamati hiyo pia inamjumuisha Sitta, Spika wa Bunge la Tisa ambaye anajulikana kwa kuruhusu mijadala dhidi ya Serikali. Katika mijadala hiyo, Bunge lliliunda kamati iliyoongozwa na Dk Mwakyembe kuchunguza sakata la Richmond lililosababisha Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu.
Katika hotuba yake ya kujiuzulu, Lowassa alidai kuwa suala hilo lilipikwa na mahasimu wake wa kisiasa kwa sababu ya uwaziri mkuu.
Kundi jingine la wajumbe wa kamati hiyo linahusisha makada waliokuwa kambi ya Lowassa alipokuwa anawania urais kupitia CCM lakini hawakuhama naye. Wajumbe hao ni Christopher ole Sendeka, Sadifa Juma Khamis, Shamsi Vuai Nahodha na Sofia Simba, ambaye alipinga uamuzi wa Kamati Kuu wa kupitisha majina matano na kuacha mengine kinyume na katiba.
Wajumbe wengine ni Livingstone Lusinde, Abdallah Bulembo na Nape, ambao wanajulikana kwa kushambulia wapinzani. Lusinde alijipatia umaarufu katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, Machi 2012 alipoamua kutumia lugha chafu dhidi ya viongozi wakuu wa Chadema.
Tayari Kinana, Mwigulu, Nape, Bulembo na Wasira wameshanukuliwa wakirusha mashambulizi makali dhidi ya Lowassa na wote waliohama CCM kuwa ni makapi na mafuta machafu na kwamba Magufuli atashinda.
Vilevile, wamo makada waliowahi kutangaza hadharani kuwa mahasimu wa Lowassa tangu alipokuwa ndani ya CCM, akiwamo Anthony Diallo. Kundi jingine ni la makada vijana kama Ummy Mwalimu, Steven Masele na Pindi Chana.
Wakizungumzia uteuzi huo, baadhi ya wajumbe waliishukuru CCM kwa kuwaweka kwenye kamati hiyo huku wakitamba kwamba watahakikisha chama hicho kinaendelea kuongoza nchi.
Mwalimu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, alisema uteuzi wake ni jambo linaloonyesha kuwa anaaminika na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi kuhakikisha CCM inashinda.
“Kamati imejipanga,” alisema. “Kazi kubwa ni kuhakikisha Dk Magufuli anashinda na anaingia Ikulu kwa kuwa anauzika.
“Hatutishiwi na kitu, tunaamini katika kushinda na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunashinda kwa kupambana. Magufuli anauzika.”
Ahadi ya kufanya kazi kwa bidii pia ilitolewa na Mbunge wa Kiembesamaki, Waride Bakari Jabu ambaye alisema atajituma kwa asilimia 100 kuhakikisha CCM inashinda.
“Nimefurahi na nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote kuhakikisha kuwa tunashika dola Zanzibar na Bara,” alisema.
Wakati Jabu akiyasema hayo, Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Maua Daftari alitaka wananchi wawaunge mkono katika kazi hiyo.
“Hili jukumu si la kwanza, lakini ninachoweza kusema ni kuwa wananchi watuunge mkono ili tushinde,” alisema na kusisitiza kuwa watahakikisha kampeni zinafanyika kwa usalama na wala si kwa fujo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo alisema amepokea uteuzi huo na anachosubiri ni kukaa na kupanga kitakachofanyika.
Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), alisema hajapata taarifa rasmi kuhusu kuteuliwa kwake kwenye kamati hiyo.
Hata hivyo, alisema hiyo itakuwa ni mara yake ya pili kuwa kwenye kamati ya kampeni kwani aliwahi kufanya kazi kama hiyo alipokuwa NCCR-Mageuzi mwaka 1995. Alisema atazungumza zaidi kuhusu wajibu huo aliopewa pindi atakapopewa taarifa rasmi na Nape.
Wakati Diallo na Makongoro wakisubiri kikao, Nchemba, ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha, alitumia nafasi hiyo kumsifu Dk Magufuli.
“Sisi tunachokifanya ni kuweka njia tu ya kwa nini achaguliwe, kuwaambia Watanzania kwa nini anafaa, kwa kuwa awamu ya tano ni awamu ya kazi tu,” alisema.
Source: Mwananchi
Saturday, August 15, 2015
Wednesday, August 12, 2015
Lowassa ni mbinafsi “Watanzania mnatakiwa kufahamu kuwa mnapokutana na Lowassa, Ninyi sio kitu bali kitu ni Lowassa,”
“Ili niwaunge mkono, CCM mnatakiwa kuwakata watu wote katika mchakato wa kura za maoni wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali,” alisema Polepole ambaye awali alitangaza kutembea nchi nzima kuhamasisha watu wasimchague Lowassa.PolePole alitoa ushauri pia kwa chama chake cha CCM ili kiwe tofauti na makosa yaliyofanywa na wahasimu wao wa kisiasa, Ukawa.“Viongozi wa CCM, kama Ukawa wamewachukua watuhumiwa wamewakubali. Nyie onesheni uongozi na utofauti mhakikishe mnawakata wagombea wote wanaotuhumiwa. Onesheni kwamba watuhumiwa hawana nafasi kwenu.
BREAKING: Dr. Slaa aibuka tena kupitia Ukurasa wake wa Twitter na kusema Mambo Mazito kuhusu Lowassa
BREAKING: Dr. Slaa aibuka tena kupitia Ukurasa wake wa Twitter na kusema
Mambo Mazito kuhusu Lowassa...Hapa Chini unaweza Kusoma Mambo yote
aliyosema kuhusu Lowassa na Chadema... 




Habari Mpya Kutoka MUHIMBILI Ambako Freeman Mbowe Amelazwa Baada ya Kuugua Ghafla
Hali ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai
anayemaliza muda wake, mh Freeman Aikae Mbowe, imeendelea kuimarika.Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili, anakopatiwa matibabu, mh Mbowe, amesema anaendelea vizuri na kwamba bado anaendelea kupumzika hospitalini hapo, kama alivyopangiwa na madaktari wanaoangalia hali yake.
''Hali yangu imeendelea kuimarika na kilichonipata jana kwa mujibu wa uchunguzi wa madaktari ni uchovu wa muda mrefu, uliobainishwa kutokana na shughuli za muda mrefu bila kupumzika katika shughuli zangu za kisiasa'' amesema Mbowe.
Mh Mbowe ameongeza kwamba, madaktari wamemtaka kuendelea kuwa chini ya uangalizi wao mpaka hapo watakapo mruhusu kuendelea na shughuli zake za kwawaida.
Mmoja kati ya madaktari wanaoangalia afya ya mh Mbowe, Dr Tulizo Sanga(daktari bingwa wa magonjwa ya moyo) ,amewaambia waandishi wa habari hospitalini hapo kwamba, mh Mbowe alipokelewa jana akitokea Hospitali ya Doctors Plaza ya Kinondoni,jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya uangalizi na uchunguzi zaidi kutokana na kuugua ghafla wakati akiwa katika msafara wa mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.
Mh Mbowe amelazwa katika hospitali ya Muhimbili, kitengo cha moyo, baada ya kuugua ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo.
Nae James Mbatia mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA, amefika hospitalini hapo kumjulia hali mh Mbowe, na amesema pamoja na hali ya kuumwa ya mh Mbowe, wao bado wanaendelea kufanya kazi na kwamba ratiba mbalimbali za vikao vya UKAWA ziko palepale, na amewaomba watanzania kuwa watulivu na kuendelea kumuombea mh Mbowe, apone haraka.
Gazeti la Uhuru: Vijana waliomsindikiza Lowasa kuchukua fomu jana ni VIBAKA
Ni kitambo sana gazeti dada la chama Cha Mapinduzi limekua likinanga
Harakati za vyama pinzani. Yote tisa kumi ni ripoti zilizomo kwa gazeti
hili tar 11/08/2015 siku moja baada ya MTETEMO WA UKAWA JIJINI DAR."Ati Kundi la vibaka latikisa Ukawa. " hao vibaka mliwaona wapi, hizo fedha walizolipwa mliziona kwa nani, na hizo Pombe walizokunywa mliwanywesha?
Mmeanza kukata mauno hata ngoma bado haijaanza kudunda? Mtachoka mapemaaa. Kama Gazeti ni la kimapinduzi wapeni watu habari zenuu, msiwapotoshe watu kwa vitu walivyovishuhudia.
Niwaulize kidogo.
Hiviii Wizi wa kura katika michakato ya majimboni si habari? Semeni hayo.
Na je Rushwa iliyoota mizizi katika Harakati za uteuzi si habari? Andikeni hiyo
Monday, August 10, 2015
Breaking News: Jeshi la Polisi Lakanusha Kupiga Marufuku Maandamano ya Kumsindikiza Kuchukua fomu Mgombea urais Chadema,Edward Lowassa
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
amekanusha kupiga marufuku maandamano ya kumsindikiza Lowassa
Kuchukua fomu ya kugombea urais ofisi za tume ya taifa ya
uchaguzi.Kova amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yale yanayo anzia ofisi za CHADEMA kwenda NEC,lakini ya kutoka Nec kwenda makao makuu ya CUF Buguruni hawayatambui.
Katika Hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe amesema hawana taarifa yoyote ya zuio la maandamano toka jeshi la polisi.
Mbowe amesisitiza kuwa maandamano ya kumsindikiza Lowassa NEC yako palepale na amewataka wapenzi na wafuasi wa UKAWA wasiogope.
Friday, August 7, 2015
Mke wa Dk Slaa afunguka
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na gazeti hili na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.
Tetesi hizo zilivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Dk Slaa kutoonekana katika vikao muhimu vya Chadema na Ukawa, kuwa Mushumbusi hakupendezwa na kitendo cha Lowassa kupitishwa kuwania urais chini ya mwavuli wa Ukawa na badala yake alitaka Dk Slaa ndiye awe mpeperusha bendera.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo Mushumbusi amezikanusha, aliamua alimfungia ndani Dk Slaa kama moja ya mbinu za kumzuia asishiriki shughuli za kichama, tuhuma ambazo amezikanusha.
“Bosi wako akija kukuomba ushauri utamsaidia, lakini akija akakuambia ameshafanya maamuzi unaweza kupingana naye?” alihoji Mushumbusi akianza kutoa maelezo yake na kuendelea:
“Wakati wa vikao nilikuwa namwona (Dk Slaa) anachelewa kurudi kila siku, siku moja akaja akaniambia uamuzi aliouchukua na mimi sikuwa na la kusema, nikachukua shuka nikajifunika.”
Katika mahojiano yake ya kwanza na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa tetesi hizo, Mushumbusi pia alikana kumfungia Dk Slaa ndani ya nyumba, akisema wakati maneno hayo yalipokuwa yanazagaa, alikuwa nje ya nchi na wala hakujua kinachoendelea.
“Mwenyewe najiuliza nini kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba yangu ina milango miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata watoto siwezi kuwafungia. Kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya kwa mwanamume. Mwanamume ni mwanamume tu,” alisema.
Alisema viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wanafika nyumbani kwake na walikutana na Dk Slaa na kuzungumza naye... “Kama ningekuwa nimemfungia wangezungumza naye vipi?”
Mushumbusi alisema mwanamke anaweza kufanya chochote lakini kuna baadhi ya mambo ambayo mwanamume akiamua ni vigumu kumzuia.
Akifafanua tuhuma za kumshinikiza Dk Slaa kujiuzulu Chadema, Mushumbusi alisema kiongozi huyo wa Chadema ana uamuzi wake na yeye ni msaidizi tu ambaye hana uamuzi wa mwisho kwenye familia.
Hata hivyo, alisema endapo angeamua kumshawishi, uwezo wa kufanya hivyo anao lakini yeye ni mwanamke mwadilifu anayependa mafanikio ya mumewe.
“Kwani unanionaje? Mimi ni ‘strong’ (nina nguvu), ningetaka ningefanya hivyo, nisingeshindwa,” alisema.
Pamoja na hayo, Mushumbusi alilalamika kuwa tuhuma hizo dhidi yake zimesababisha asisikilizwe kama ilivyokuwa awali.
Bila kufafanua kwa undani, alisema kuna kundi linalounda propaganda hizo ili abadili mtazamo kuhusu mumewe lakini jambo hilo haliwezi kutokea.
“Nilisema nitampenda kama alivyo, sitajali chochote wala akiwa katika hali gani au chama gani. Kazi yangu ni kumtia moyo ili kile atakachofanya kifanikiwe,” alisema.
Auza mkaa
Mbali na kukanusha vikali tuhuma hizo, Mushumbusi alisema alikwishajitoa kwenye masuala ya siasa kwa miaka miwili sasa na badala yake ameamua kufanya biashara ya kuuza mkaa.
“Nimenyamaza kimya, nimekaa kando ninaendelea na biashara yangu ya kuuza mkaa, nipo mbali na siasa na sitaki kujua kinachoendelea, kwanza hata mchakato wenyewe siujui,” alisema.
Aliwashauri wanawake kuacha kushabikia masuala yanayotokea ndani ya ndoa yake na kuwataka wavae viatu anavyovivaa na wajue kuwa anapitia wakati mgumu
Thursday, August 6, 2015
Prof:Ibrahim Lipumba Ang'atuka
Prof. Lipumba akiongea na waandishi wa Habari kwenye Hoteli ya Peacock
Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti kwenye chama chake cha Wananchi CUF.
Ametangaza kuachia ngazi uenyekiti wa chama hicho mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok.
Tazama video Prof: Lipumba akiongea na waandishi wa habari
Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.
Prof Lipumba akitaja sababu za kujiuzulu nafasi ya uenyekiti CUF
Na hizi ni baadhi ya kauli/sentensi alizo zitoa Prof. lipumba kwa waandishi wa habari
Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti kwenye chama chake cha Wananchi CUF.
Ametangaza kuachia ngazi uenyekiti wa chama hicho mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok.
Tazama video Prof: Lipumba akiongea na waandishi wa habari
Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.
Prof Lipumba akitaja sababu za kujiuzulu nafasi ya uenyekiti CUF
Na hizi ni baadhi ya kauli/sentensi alizo zitoa Prof. lipumba kwa waandishi wa habari
Tuesday, August 4, 2015
Angalizo Kwa Dr. Slaa na Edward Lowassa!
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taaluma ya upadri.Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata badiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.
Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.
Bila shaka kuna watu ndani ya CHADEMA na hata nje ya CHADEMA wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASSA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowassa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowassa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASSA ana hasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASSA kama waziri Mkuu mstaafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowassa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miaka zaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowassa ambaye ameshika nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki.Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowassa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowassa ambaye hawajajipanga na ni Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani.Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine,
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
(3)Slaa aliwahi kusema kuwa anapata Nyaraka kwa watu wa Tiss , sasa angalia Mkurungezi wa zamani Tiss Apson ameonekana kwa Lowassa, Kingunge ambaye hajawahi kukaa na Slaa amejitokeza kwa Lowassa , akina Emmanuel Nchimbi na Sophia Simba ambao ni watu wa ndani serikalini na wameshiriki kukuibia wewe Slaa kura wamejitokeza Nyuma ya Lowassa na wala hawawezi kujitokeza kwako. Je, wewe huna akili ya kuona haya?
(4) Lowassa hadi leo ana ulinzi wa Ikulu ambao hauwezi kuhujumiwa , wewe Slaa juzi tu mlinzi wako amenunuliwa.
Lowassa hawezi kupewa nyaraka feki toka ikulu kwa kuwa kuna akina Apson , je wewe una nani zaidi ya Mkeo ambaye umempora kutoka kwa watu wa CCM?
Nina hasira na wewe Slaa pamoja na mkeo toka haraka huko uje huku Mungu anakuita kwa mara ya mwisho umuunge Lowassa katika urais vinginevyo utapotea Kisiasa bado wiki moja tu utapoteza mwelekeo
MAONI KWA LOWASSA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama.Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimpa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowassa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.
(4)Kama Lowassa ni mwizi na dhaifu kisiasa kwanini CCM wanahangaika baada ya Lowassa kuchukua form??
(5)Kama Lowassa ni mgonjwa , Kwanini CCM wananahaha baada ya Lowassa kuchukua form? Je, wanamuogopa mgonjwa??
HOJA DHAIFU KWA CCM
(1)CCM walisema Lowassa ni Mwizi na anatakiwa kujivua Gamba sasa Lowassa ameondoka kwanini munahofu???
(2)Kama Lowassa ni mwizi Kama wanavyoamini CCM basi nawashauri CCM wasihangaike na jina la Lowassa kwenye tume ya Uchaguzi , waliache harafu wapime nguvu ya Lowassa na Mangufili!!
Kikwete alisema Chama si mtu sasa uje umnadi Magufuli wakati anapambana na Lowassa!!
(3)Nawaomba CCM waje na ushahidi kwenye majukwaa ya Siasa kuonesha kuwa Lowassa ni fisadi, wasikimbilie kwenye kamati ya maadili na NEC.Wakifanya hivyo basi wananchi watachambua pumba na mchele.
Location:
Tanzania
Wasomi waishangaa UKAWA
Wakitoa maoni yao Dar es Salaam jana, wasomi hao kutoka taasisi za vyuo na zile za utafiti, walisema pamoja na kwamba kuhama chama ni haki ya mtu na hakuna anayeweza kuhoji, lakini wakahoji ni nini dhamira ya kuhama huko na kama kuna maslahi kwa wananchi.
Akizungumzia uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Vyama Vinne vya Upinzani (Ukawa) na kukihama chama tawala, CCM, Mhadhiri Mwandamizi aliyebobea katika uchambuzi wa masuala ya siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alihoji dhamira yake ni ipi.
“Kuhama chama ni haki ya raia, hakuna anayehoji, lakini dhamira inayompeleka Ukawa ni nini, hivi mtu aliyekuwa haramu kwao leo ni lulu, hapa ndio wasiwasi unaanza. Mwaka 2010 walimtumia Lowassa kama mtaji, mwaka 2015 wanamuona ni dhahabu, kuna uwalakini hapa”, alisema Dk Bana.
Alifafanua kwamba katika medani za siasa, haiwezekani mtu mmoja tena kwa ghafla anakuwa maarufu ndani ya vyama vinne na kusema huo ni unafiki uliokubuhu na hakuna demokrasia, kwani hata huko anakokwenda ataasi na kuwageuka.
“Lowassa anatoka CCM kimwili, na Ukawa walimdhalilisha sana Lowassa, walimnyanyasa na sasa ni vyema wakatubu hadharani kabla ya kupiga hatua nyingine yoyote, wamuombe awasamehe, na kwa vile Lowassa alishasema yeye ni Mkristo safi, basi awasamehe”, alisema Dk Bana.
Dk Bana akifafanua zaidi alisema haiwezekani taasisi hizo nne yaani vyama vya siasa vinne vinavyounda Ukawa, NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD, kukosa mtu wa kumsimamisha kwenye uchaguzi ujao hadi kusubiri CCM ikamkate jina Lowassa na ndio wao wakaona anafaa kupitia umoja wao.
“Tunapozungumzia masuala ya siasa tuangalie mbele zaidi, tujiulize hivi hawa viongozi wa vyama hivi vinne wana dhamira ya kweli kwa nchi hii, kinachoonekana hapa ni uroho wa madaraka na jambo hilo litafifisha vyama hivyo vyote kisiasa,” alionya Dk Bana.
Alisema haitakuwa ajabu ifikapo siku ya uchaguzi, watanzania sio mbumbumbu wataamua, hawawezi kuvutwa na mtu mmoja tu, bali wataangalia dhamira zao na maslahi ya taifa.
Alihadharisha kwamba jambo hilo la Lowassa kuondoka CCM litambomoa kisiasa na kamwe haliwezi kuijenga Ukawa kwani inavyoonesha kila mmoja ana dhamira yake binafsi na kwamba hakuna maadili wala sheria inayotumika kuongoza safari hiyo ya Ukawa.
Kwa upande wake, Mtafiti Mwandamizi wa masuala ya Uchumi kutoka REPOA, Dk Abel Kinyondo alisema Ukawa wamemtumia Lowassa kama chambo cha kuvuta watu wengi, jambo ambalo alisema ni mbinu moja ya kushinda uchaguzi.
Lakini akaonya kuwa, siasa ni zaidi ya kushinda uchaguzi, na kusema ni vyema Ukawa wakatafakari uamuzi wao kwani jambo hilo linauweka umoja huo njia panda. “Kwa kumpata Lowassa wanaweza kushinda uchaguzi, lakini je, maadili na sheria, Ukawa inasimamia wapi?
Vyama vinatakiwa kuwa na maadili na msimamo vilete sera nzuri kwa wananchi sasa, miaka mitatu mfululizo walimsema Lowassa mchafu, na anatakiwa awe amefungwa, sasa wamemsafisha lini hadi awe msafi kusimama Ukawa? Alihoji Dk Kinyondo.
Alisema, Tanzania haijafika kipindi cha wagombea kushinda kwa gharama yoyote, bali inahitaji viongozi wasafi na wanaoweza kutetea maslahi ya wananchi, na sio wenye nia na maslahi binafsi ya kung’ang’ania madaraka kwa nguvu.
“Ni vyema tungeambiwa Ukawa wanasimamia wapi, walishatoa matamko sio, Dk Slaa wala Mbowe ya kuwa Lowassa ni fisadi na anatakiwa afungwe, sasa leo amegeuka kuwa msafi kiasi gani hadi wamsimamishe kuwakilisha vyama hivyo vilivyomtuhumu? Alihoji Dk Kinyondo.
Katika hilo, Dk Kinyondo alisema uamuzi wao huo, utawaacha njia panda na utashusha hadhi ya vyama hivyo kwani kama wanashindwa kusimamia misimamo yao miaka chini ya mitatu tu, wakiwa nje ya madaraka, je, wakiingia watawezaje kuongoza kwa utawala bora na kuhadharisha wananchi wanatakiwa kuwa macho.
“Siasa ni zaidi ya kushinda uchaguzi, ni kuangalia maendeleo ya watu yatakuwaje na misingi ya utawala bora ni ipi na misimamo ya chama au vyama ni ipi katika kuongoza nchi,” alisema Dk Kinyondo.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ally, alisema hadi sasa hakuna mwanasiasa yeyote aliyehamia chama kingine cha siasa, kutokana na kuendeshwa na itikadi ila wengi wanahama kutokana na maslahi yao binafsi.
“Hata hivyo, kuhama huku hakujaanza leo, katika historia ya vyama vingi tumeona wanasiasa wengi tu wakubwa, wakihama vyama vyao kwenda vyama vingine hasa ikifikia nyakati za uchaguzi na sababu kubwa ni malengo ya kisiasa,” alisema.
Alisema wengi wa wanasiasa hao huhama kutokana na njaa ya kutawala hivyo wanapokosa fursa walikotoka huhamia kwingine kuitafuta fursa hiyo. “Huu si mwenendo mzuri kwani unaonesha kuwa wanasiasa wengi hawafuati kanuni za vyama vyao bali malengo yao binafsi,” alihtimisha.
Amkimbia Lowassa Katika hatua nyingine, kada wa Chadema, Innocent Peter Kamani akizungumza kupitia kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na kituo cha Redio cha Uhuru FM jijini Dar es Salaam, alitangaza kurudisha kadi ya Chadema na kuwa mwanaharakati kutokana na chama hicho kumpokea Lowassa, akisema kimehadaa wanachama wake, kwani kwa muda mrefu walikuwa wakimsema kwa mabaya mwanachama mpya waliyempokea, hivyo kuwayumbisha wanachama kuhusu msimamo halisi wa chama hicho.
KUHUSU DK. SLAA KUMKATAA LOWASSA UKWELI NI HUU
Kutoka gazeti la uwazi.
NI kweli, ukweli ni huu! Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na kupewa fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho, ukweli wa jambo hilo umeibuliwa,
Edward Lowassa na alipochukua fomu ya kuwania urais kupitia Chadema.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama
hicho, aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa,
madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii
yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.
ALIANZA DK. SLAA, MBOWE MH!
Mjumbe huyo alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye
mtu wa kwanza ndani ya Chadema kutoa wazo na hatimaye kushiriki
kikamilifu katika vikao vya kumwezesha Lowassa kujiunga na chama hicho.
“Kwa taarifa yako, Dk. Slaa ndiye
aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Taifa
Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona jinsi
gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na
vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk.
Slaa yupo.”
MTOA HABARI ASHIRIKI VIKAO
“Mimi ninayekwambia ni Mjumbe wa Kamati
Kuu, nimeshiriki zaidi ya vikao 14 vilivyokuwa vikimjadili Lowassa na
vyote hivyo, Dk. Slaa alikuwepo. Huyu jamaa hajakaribishwa kwa utashi wa
mtu mmoja kama mnavyosikia huko nje na wala mzee Mtei (Edwin, mwasisi
wa chama hicho) hahusiki na chochote,” alisema mjumbe huyo.
WABUNGE WAKOROFI WALIAFIKI
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, ili kuondoa
dhana kuwa, Lowassa anapelekwa Chadema na uongozi, wabunge wote
‘wakorofi’ ndani ya chama hicho walikaribishwa kushiriki vikao 14 vya
kumjadili ili pia wamuulize maswali na yapate majibu kitu ambacho
kilifanyika kwa ufanisi wa hali ya juu.
Aliwataja baadhi ya wabunge hao
‘wakorofi’ na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Godbless Lema
(Arusha Mjini), John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki),
Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Halima Mdee (Kawe), Peter Msigwa (Iringa
Mjini), Joshua Nassari (Arumeru), Ezekiel Wenje (Nyamagana), David
Silinde (Mbozi Magharibi) na Highness Kiwia (Ilemela).
“Unajua, kwa vyovyote vile, vikao kama
vingefanywa na viongozi wa juu peke yao, hawa wabunge wakorofi
wangesumbua sana, lakini wote walishiriki na hakuna ambacho hawakijui.
Ndiyo maana wote wamekaa kimya kwa sababu taratibu zote zilifuatwa,”
alisema mjumbe huyo.
UKWELI ULIVYO
“Hapa lazima nikueleze ukweli.
Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake. Kuna watu
walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea tena
na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu
kilichotokea hakina masilahi kwa familia.
YADAIWA DK. SLAA ALITAKIWA KUCHAGUA MOJA
Mjumbe huyo alikwenda mbali kwa kusema
kuwa, wakati wa mchakato wa Dk. Slaa kutaka Lowassa aingie Chadema baada
ya kukatwa jina na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini
Dodoma, hakuiambia familia yake mpaka dakika za mwisho, ikajulikana.
“Ndipo familia ikamweka chini na
kumwambia achague moja. Aendelee na siasa za Chadema au aachane na
siasa hizo ili aangalie familia yake kwani kitendo chake cha kuwa
mstari wa mbele kumtaka Lowassa kiliashiria kuwa, yeye hatagombea tena
urais hivyo kuua matumaini ya familia. Ndiyo maana yupo kimya na hafiki
ofisini.”
CHADEMA YAPANGA SAFU YA KUMSHAWISHI
“Sasa dokta ni mtu mzima. Hawezi
kuliamua hilo kirahisi kama unavyofikiria. Ni lazima aende nalo taratibu
ili kuziridhisha pande zote mbili. Na kwa kutambua hilo, chama kimeunda
jopo la watu, wakiwemo mapadri, mashehe na marafiki zake ili
wamshawishi arejee Chadema lakini akiiweka familia yake katika kuridhia
na kumwelewa,” alisema mjumbe huyo wa Kamati Kuu.
LOWASSA AANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND
Kuhusu madai ya muda mrefu ya chama
hicho yanayomtaja Lowassa kuwa ni fisadi, mjumbe huyo alisema kiongozi
huyo aliwaeleza kwa ufasaha kuhusu utajiri wake na wakaridhika. Kwa
upande wa Richmond, aliwaeleza kuwa alishataka kuuvunja mkataba huo,
lakini mamlaka ya juu ikamzuia.
TAASISI TOKA NJE YATUA NCHINI KUTAFITI
Juu ya nafasi yao kushinda urais wakiwa
na Lowassa, mjumbe huyo alisema kabla ya kuafiki kumtangaza kugombea,
kwa gharama za Chadema, walikodi taasisi ya utafiti kutoka nchini
Ujerumani kuja Tanzania ili kufanya utafiti nchi nzima kama Lowassa
anakubalika.
Alisema utafiti ulipokamilika, ikaonesha
kuwa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika Julai 2015, Lowassa alikuwa mbele
ya wagombea wenzake kwa asilimia 65.
SLAA KIMYAAA!
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni,
Dk. Slaa hajajitokeza kuelezea kilichosababisha ukimya wake huku akiwa
hapokei simu ya Uwazi kitu kinachozidisha kwa kasi maneno mitandaoni juu
ya hatima yake ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Alhamisi iliyopita gazeti dada na hili,
Uwazi Mizengwe linalotoka kila Ijumaa, waandishi wake walishinda
nyumbani kwa Dk. Slaa, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar lakini
walishindwa kuongea naye licha ya kumpelekea karatasi yenye ujumbe wa
kumuomba kuzungumza naye, waliambulia kumuona kwa mbali akiwa ndani ya
geti la nyumba yak
Saturday, August 1, 2015
Kada wa Vijana Chadema Dar auawa kwa risasi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa
Vijana Chadema Tawi la Luis, Mbezi Luis, Dar es Salaam, Dennis Kasanga
ameuawa kwa kupigwa risasi shingoni usiku wa kuamkia jana, huku taarifa
zilizotolewa na polisi zikitofautiana na mashuhuda wa tukio hilo.
Kasanga,
mkazi wa Mbezi Luis alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa majambazi
waliovamia baa inayojulikana kwa jina la Mtauli iliyopo njiapanda ya
Barabara ya Goba na Makabe saa saba usiku. Hata hivyo, polisi wamesema
tukio hilo halihusiani na ujambazi na wala halikutokea muda huo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema jana
kuwa tukio hilo lilitokea saa 10 alfajiri kuamkia jana.
Alisema
tukio hilo lilitokea Barabara ya Goba baada ya watu wanne waliokuwa
wakisukuma gari bovu kuvamiwa na watu wengine wanne na kuibuka mzozo
kati yao.
“Baada ya mzozo, ghafla mmoja aliibuka na
kuanza kuwafyatulia risasi iliyowajeruhi watu wawili na kuua mmoja
aliyepigwa risasi shingoni,” alisema Kamanda Wambura.
Kamanda
Wambura alisema tukio hilo halihusiani na ujambazi kama watu
wanavyodai. “Siyo kila mtu anayefyatua risasi ni jambazi, subiri kwanza
tunaendelea na uchunguzi wa tukio.”
Hata hivyo,
mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa marehemu aliuawa kwa kupigwa risasi
na majambazi, ambao pia waliwajeruhi watu wengine wawili akiwamo mlinzi
wa baa hiyo.
Mbali na kujeruhi, watu waliokuwa na
bastola, mapanga na marungu pia waliwapora simu na fedha wateja wachache
waliokuwapo kwenye baa hiyo.
Kati ya waliojeruhiwa,
mmoja ni mlinzi aliyepigwa rungu usoni na mwingine aitwaye Erasmo
Basheja, mkazi wa eneo la Basondole aliyepigwa risasi begani.
Mhudumu
mmoja wa baa hiyo aliyekataa kutaja jina lake, aliliambia gazeti hili
jana kuwa watu kati ya sita au saba walifika kwenye baa hiyo saa saba
usiku wakijifanya wateja waliotaka kuhudumiwa vinywaji.
Alisema
wakati wakifika, baa ilishafungwa ila kulikuwa na wateja wachache nje
na yeye muda huo alikuwa ndani. “Baa ilishafungwa zamani, ila kulikuwa
na wateja wachache nje wakimalizia vinywaji,” alisema shuhuda huyo.
Alisema
baada ya watu hao kuelezwa kuwa baa imeshafungwa, ghafla walibadilika
na kuwataka watu waliokuwa hapo kulala chini na wakaanza kuwapekua
mifukoni na kupora simu zao.
“Nilisikia mlio wa risasi
na haraka haraka nilifunga mlango wa kuingia kaunta ya vinywaji kisha
nikalala uvunguni kwenye chumba kinachotumia mlango mmoja na kaunta,”
alisema shuhuda huyo.
Aliongeza: “Niliwasikia wale
majambazi wakisema, ‘hawa wanawake wameshafunga geti.’ Nilikaa kimya
nikiwa nimejilaza chini ya godoro.”
Alisema majambazi
hao wanaijua fika baa hiyo, kwani baada ya kuwalaza watu chini
walizunguka nyuma, ambako ndiko kwenye geti la kuingia kaunta na vyumba
vya ndani.
Mlinzi wa baa hiyo, ambaye amejeruhiwa usoni
kwa kupigwa na rungu aliiambia gazeti hili kuwa majambazi hao walifika
kwenye baa hiyo saa saba usiku wakati tayari pameshafungwa.
Alisema
alikuwa amekaa kaunta pamoja na marehemu na mtu mwingine ambaye
hakumbuki jina lake, ndipo aliposikia mlio wa risasi na wakati
akitaharuki, alivamiwa na mmoja wa watu hao na kupigwa rungu usoni huku
akisema: “Usiniangalie usoni.”
“Nilidondoka chini na
wakaanza kunisachi mifukoni huku wakinitaka kutoa simu na fedha,
niliwajibu sina kitu na baada ya kunipiga niliamua kutoa simu na
kuwapa,” alisema mlinzi huyo.
Alisema marehemu alipigwa
risasi wakati akiondoka alipoketi na kwenda sehemu ambayo alisikia mlio
wa risasi. “Alikuwa kaunta na baada ya mlio wa risasi alinyanyuka na
kwenda sehemu ya nje ya baa huko ndiko alikopigwa risasi na kufariki
dunia papo hapo,” alisema.
Kifo cha kiongozi huyo wa vijana Chadema pia kimethibitishwa na mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Luis, Finna Massawe.
Majirani
wa eneo ilipo baa hiyo walidai kuwa baa hiyo imekuwa ikivamiwa na
majambazi, mara kwa mara, na kwamba ingawa tukio la kuuawa mtu ni mara
ya kwanza kutokea, lakini tayari uhalifu wa kuvamiwa baa hiyo
ulishafanyika mara mbili.
Tuesday, July 28, 2015
Breaking News: LOWASSA Atangaza Rasmi Kuhamia CHADEMA.....Asema CCM siyo Baba Yake Wala Mama Yake
Waziri
mkuu wa zamani Edward Lowassa ametangaza rasmi kukihama chama
cha mapinduzi, CCM mchana huu na kutangaza kuhamia CHADEMA.....Lowassa ametoa kauli hii Bahari Beach , Dar akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa UKAWA ambao wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia hatima yake kuelekea ikulu pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Lowassa amesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha, ameamua kujiondoa CCM kwa kuwa siyo baba yake wala mama yake na kuitikia wito wa UKAWA kupitia CHADEMA.
Amesema safari yake haitafanikiwa iwapo hawatajitokeza watu wengi kupiga kura na anaiomba tume ya uchaguzi iongeze muda ili watu wote waweze kujiandikisha
Lowassa amesema alinyimwa haki yake na CCM kama mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakuwa mnafiki akisema anaimani na chama hicho.
Fedha alizochangiwa Lowassa na kundi la Marafiki wa Edward Lowassa zatafunwa....
WANACHAMA wa kundi la Marafiki wa Edward Lowassa waliochanga fedha za
kumwezesha waziri mkuu huyo wa zamani kuchukua fomu ya kugombea urais,
wamemtuhumu aliyekuwa naibu katibu wao, George Kivuyo kutafuna fedha
hizo.Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wanachama hao wanaojulikana kama Team Lowassa 4 President, zinadai naibu katibu mkuu huyo ambaye pia ni mweka hazina wao, alitafuna kiasi cha shilingi laki saba zilizochangwa.
Walidai fedha hizo ziligunduliwa kutotumika ilivyopaswa baada ya kutojulikana zilipo na alipoulizwa hakuwa na majibu ya kueleweka.
Baadhi ya wanachama hao, Fauzia Ally, Hassan Mollel na Yussuf Hamis walisema kutokana na kitendo hicho, wanachama hao wameanza kufarakana kutokana na mgogoro.
“Hizi fedha zilitumiwa tofauti na ilivyokusudiwa, zinatakiwa zirudishwe, akabidhiwe mzee Lowassa,” alisema Hassan Mollel.
Naibu katibu mkuu huyo alipopigiwa simu na mwandishi wetu juzi Jumapili alisema kwamba madai hayo ni ya uongo na fedha hizo hazikuwa laki saba bali zilikuwa Sh. 526,000.
“Mimi ni mweka hazina msaidizi na tatizo limekuja baada ya kuhoji kuhusu fedha hizo alizokabidhiwa bosi wangu.”
Katibu mkuu wa chama hicho, Mohamed Mkindi alipoulizwa alikiri kusikia malalamiko hayo lakini alidai yupo mikoani na akirudi jijini Dar es Salaam atazifuatilia.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Post Labels
.disqus.com/recent_comments_widget.js?num_items=4&avatar_size=32&excerpt_length=100&hide_mods=0">













