Hamfrey Polepole na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
wamekabana kwa hoja kali kuhusu uamuzi wa Chadema na Ukawa kwa ujumla
kumpokea Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea Urais.Polepole na
Msigwa walikutana jana katika kipindi cha ‘Mada Moto’ kinachorushwa na
kituo cha runinga cha Chanel Ten kujadili mada iliyotajwa kama ‘Lowassa
Ndani ya CCM’.Polepole alionesha msimamo wake wa kumkataa Edward Lowassa
kuwa sio kiongozi sahihi aliyepaswa kuungana na Ukawa katika safari yao
ya kutaka kuongoza dola na kupata katiba mpya ya wananchi kwa kuwa ana
tuhuma nzito zilizompa madoa.Aliongeza kuwa dhana ya upinzani na
mwenendo wa Ukawa ulipotea pale walipomkaribisha Lowassa huku wakisahau
kuwa ni miaka michache iliyopita walizunguka nchi nzima kuwaaminisha
watanzania kuwa ni fisadina kwamba wana ushahidi wa kutosha.Polepole
ambaye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iyoongozwa na Jaji Warioba, alisema kuwa Ukawa iliundwa kwa madhumuni ya
kutetea Katiba ya Wananchi na sio kwa lengo la kisiasa kama ilivyo
sasa.Alisema kuwa Edward Lowassa hana msimamo thabiti kwenye maamuzi
yake kuhusu Katiba anayoitaka kwa kuwa aliwahi kumhoji awali akasema
anahitaji muundo wa serikali tatu lakini baadae alimfuata na kumueleza
kuwa amebadili anataka muundo wa serikali mbili.“Lowassa niliongea naye
wakati huo nakusanya maoni kuhusu katiba mpya, mara ya kwanza alisema
anataka serikali tatu na akaandika kwenye kumbukumbu maalum za bunge.
Lakini baadae alinifuata tena na kubadili msimamo wake akitaka serikali
mbili,” alisema Polepole.Anasema kilichomshangaza zaidi kwa Lowassa ni
pale alipopendekeza kuwa anataka muundo wa serikali mbili na kwamba
serikali hizi mbili ziwe na uhusiano wa kijeshi pekee.Akiendelea kutetea
hoja yake ya kumpinga Lowassa, PolePole alisema kuwa amewahi kufanya
kazi na Lowassa na kwa undani kabisa aligundua kuwa ni
mbinafsi.“Watanzania mnatakiwa kufahamu kuwa mnapokutana na Lowassa,
Ninyi sio kitu bali kitu ni Lowassa,” alisema.Mjadala huo ulitawaliwa na
mivutano binafsi iliyowalazimisha kutoka nje ya mada mara kadhaa
hususan baada ya Mchungaji Msigwa kutoa tuhuma za Polepole hadharani
kisha akampa nafasi ya kujitetea.Baada ya PolePole Kujitetea kufuatia
tuhuma hizo, Mchungaji Msigwa alimueleza kuwa alichokifanya ndio
kinaitwa ‘natural justice’ ambayo Edward Lowassa hakupewa wakati
ule.Akizijibu hoja za Polepole huku kukiwa na majibishano ya hapa na
pale, Mchungaji Msigwa alikiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wanachama wa
Ukawa waliomsema sana Edward Lowassa na kumuita fisadi lakini sasa
ameamua kukaa kimya.“It’s true tulisema. Hata mimi nilisema, it’s true I
can’t deny it. Lakini hata Joe Biden (Makomo wa pili wa Marekani)
alikuwa anamsema Obama kuwa ‘he does not fit for Commander in Chief,
lakini alipochaguliwa wakafanya kazi pamoja. Hatuwezi kusema kana kwamba
Lowassa ndiye muovu kuliko mtanzania yeyote hapa nchini,”
alisema.Aliongeza kuwa kitu kikubwa alichojifunza kwa Lowassa na
kumfanya amheshimu sana, ni moyo wa uvumilivu na kukaa kimya hata pale
alipokuwa akitukanwa kila kona na kuitwa Fisadi. Alisema moyo huo wa
uvumilivu hata watumishi wengi wa Mungu hawana.Alifafanua kuwa katika
ulimwengu wa siasa ni kawaida kufanya kazi na mwanasiasa ambaye awali
ulikuwa ukimpinga sana kwa kuwa muda ukifika akaamua kubadilika mambo
hubadilika pia.Msigwa alisema kuwa chama chao ni chama cha demokrasia na
maendeleo na kwamba hilo ndilo limewapelekea kumfungulia mlango Edward
Lowassa baada ya kumhoji na kumuelewa.Alipinga hoja ya Polepole kuwa
Lowassa ana mapesa mengi ambayo ameyapata kwa njia zisizofahamika,
Msingwa alisema kuwa maelezo hayo hutolewa bila kuelezewa kwa undani
kama ana pesa nyingi kuliko nani (serikalini).“Unasema Lowassa ana
mapesa mengi, ni kama vile unajua akaunti zote za Lowassa zina shilingi
ngapi. Na husema ana fedha nyingi kuliko nani?”Aliwataka watanzania
kutomchukulia Lowassa kama vile ndiye mtanzania mwenye dhambi nyingi
kuliko wote bali wajikite katika kuangalia nia yake ya dhati ya kuleta
mabadiliko ya kweli nchini.Alisisitiza kuwa Chadema hawana muda wa
kumsafisha Lowassa kwa kuwa umati uliofurika kumsindikiza kuchukua fomu
ya kugombea urais katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Mkuu (NEC) inaonesha
jinsi ambavyo watanzania wana Imani naye.Alisema kuwa kwa mujibu wa
tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonesha kuwa ni asilimia 5 hadi 8
tu ya watanzania ambao wamejikita katika kufahamu ufisadi wa wagombea na
kwamba umma mkubwa unataka mabadiliko kwa kuwa wamechoshwa na
muundo.Msigwa alimtaka PolePole kutomzungumzia Lowassa pekee kwa mtazamo
hasi bali azungumzie pia ubaya wa Magufuli ambaye anaunga mkono muundo
wa serikali mbili kinyume na ile anayoisapoti Polepole na Tume Ya
Mabadiliko Ya Katiba. Na kwamba yapo maovu mengi kwenye wizara ya ujenzi
inayoongozwa na Mafuli.Akijibu hoja ya Msigwa, PolePole alisema kuwa
yeye ni mmoja kati ya watu walioishawishi CCM kukata majina ya wagombea
wote wenye madoa katika mchakato wa kura za maoni kumpata mgombea
urais.Alisisitiza kuwa ingawa CCM ni chama chake, hatampigia kampeni
Magufuli hadi pale ambapo rufaa zilizokatwa dhidi ya wagombea
waliotangazwa kuwa washindi wa kura za maoni ziangaliwe na wote wenye
madoa waondolewe.
“Ili niwaunge mkono, CCM mnatakiwa kuwakata watu wote katika mchakato wa kura za maoni wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali,” alisema Polepole ambaye awali alitangaza kutembea nchi nzima kuhamasisha watu wasimchague Lowassa.PolePole alitoa ushauri pia kwa chama chake cha CCM ili kiwe tofauti na makosa yaliyofanywa na wahasimu wao wa kisiasa, Ukawa.“Viongozi wa CCM, kama Ukawa wamewachukua watuhumiwa wamewakubali. Nyie onesheni uongozi na utofauti mhakikishe mnawakata wagombea wote wanaotuhumiwa. Onesheni kwamba watuhumiwa hawana nafasi kwenu.
“Ili niwaunge mkono, CCM mnatakiwa kuwakata watu wote katika mchakato wa kura za maoni wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali,” alisema Polepole ambaye awali alitangaza kutembea nchi nzima kuhamasisha watu wasimchague Lowassa.PolePole alitoa ushauri pia kwa chama chake cha CCM ili kiwe tofauti na makosa yaliyofanywa na wahasimu wao wa kisiasa, Ukawa.“Viongozi wa CCM, kama Ukawa wamewachukua watuhumiwa wamewakubali. Nyie onesheni uongozi na utofauti mhakikishe mnawakata wagombea wote wanaotuhumiwa. Onesheni kwamba watuhumiwa hawana nafasi kwenu.
Post a Comment Blogger Facebook