Showing posts with label ACT. Show all posts
Showing posts with label ACT. Show all posts

Friday, August 21, 2015

Huyu Ndo Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo baada ya Kitila Mkumbo Kukataa

Bi. Anna Mghwira (56
Hatimaye Chama cha ACT – Wazalendo kimempitisha mwenyekiti wake, Anna Mghwira (56) kuwania urais baada ya mshauri wake, Profesa Kitila Mkumbo aliyekuwa amechukuliwa fomu kukataa kubeba jukumu hilo.

Sambamba na Mghwira, mkutano mkuu wa chama hicho uliokutana jana ulimpitisha Hamad Mussa Yusuf kuwa mgombea mwenza.

Chama hicho kimefikia hatua hiyo baada ya kusota kwa siku kadhaa kutafuta mgombea na pigo kubwa lilikuwa juzi baada ya Profesa Mkumbo kukataa.

Akisoma maazimio ya Halmashauri Kuu katika mkutano mkuu jana usiku, mshauri wa chama hicho, Profesa Mkumbo alisema wameamua kumpitisha Mghwira kwa kuwa anazo sifa za kuwania urais.

Alisema mwenyekiti huyo anao uwezo na sifa za kuwa rais, kwa kuwa kazi za rais ambazo ni kufikiri, kuwa mlinzi mkuu wa umoja, tunu za Taifa na kuwa mfano bora wa ubinadamu anazimudu.

Alisema Mghwira anaweza kufikiri na amekuwa akiandika makala mbalimbali, jambo ambalo baadhi ya wagombea hawaliwezi kwa kuwa hata hotuba wanaandikiwa.

Baada ya kumtangaza, wajumbe wa mkutano huo walishangilia kwa mbwembwe kumpata mgombea huyo.

Kwa uteuzi huo, Mghwira atalazimika kuachia ule wa awali wa kuwania ubunge katika Jimbo la Singida Mjini na atakuwa na kibarua ya kutafuta wadhamini nchi nzima na kukamilisha kazi hiyo kabla ya kurejesha fomu kwa muda aliopangiwa wa saa 7.30 mchana leo.

Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo, Mghwira alisema Taifa linahitaji kiongozi mwenye moyo wa nyama, mwenye upendo, uadilifu na mwenye uwezo wa kuwaunganisha watu wote bila upendeleo.

Alisema wamechelewa kumtangaza mgombea kwa kuwa walikuwa wanatafakari kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya “Ikulu ni mahali patakatifu”, hivyo wamempata rais mtakatifu.

Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe alisema ilani ya uchaguzi ya chama hicho imejikita katika mambo matano ambayo ni hifadhi ya jamii, elimu, afya, ajira na utalii.

Wednesday, August 19, 2015

Mgombea urais aichanganya ACT- Wazalendo

Mchakato wa kumpata mgombea urais umeendelea kukichanganya Chama cha ACT – Wazalendo na sasa kimelazimika kuanza upya vikao vya kumpata mgombea mwingine atakayepeperusha bendera ya urais kwa tiketi ya chama hicho.
Mkanganyiko huo umetokea baada ya mgombea aliyeteuliwa   na kuchukuliwa fomu na chama hicho ya kugombea nafasi hiyo, Profesa Kitila Mkumbo kukataa uteuzi huo juzi, huku zikiwa huku zikiwa zimebaki siku mbili kumalizika kwa mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu. Katibu wa Mipango na Mikakati wa ACT – Wazalendo, Habibu Mchange aliwaambiwa waandishi wa habari jana kuwa chama hicho kinaanza leo mchakato wa kumpata mgombea atakayebeba jukumu hilo baada ya Profesa Mkumbo kukataa uteuzi wa chama.
Alisema mchakato huo utaanza na mkutano wa Kamati Kuu utakaofanyika leo na kufuatiwa na mkutano wa Halmashauri Kuu utakaofanyika kesho, kisha mkutano wa kidemokrasia kwa ajili ya kutafuta mbadala wa Profesa Mkumbo. “Baada ya vikao hivyo ndipo tutamtaja rasmi mgombea wetu na zoezi la kutafuta wadhamini litaanza siku hiyohiyo,” alisema Mchange. Mchange alisema tayari wagombea watatu wameshajitokeza kuwania nafasi hiyo.
“Tuna wagombea watatu tena wenye sifa, wameshachukua fomu za kuwania nafasi hiyo, kwa hiyo kazi ya vikao ni kuangalia yupi anafaa zaidi kati yao na ndiye atakayechaguliwa,” alisema Mchange ambaye alikataa kutaja majina hayo. Wakati ikiwa inaonekana kwamba chama hicho kitalazimika  kukimbizana na muda ili kukamilisha mambo hayo ndani ya muda uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kiongozi huyo alisema wameshasambaza fomu za wadhamini hivyo muda uliyobaki unatosha. “Fomu zimeshasambazwa mikoani kwa hiyo tukimpata mgombea zitajazwa na kurejeshwa ndani ya muda na  tutarudisha fomu NEC kama utaratibu unavyotaka,” aliongeza, Katibu wa Fedha na Rasilimali wa chama hicho, Peter Mwambuja.
Kuhusu mgombea mwenza aliyetajwa juzi kuwa ni kada wa chama hicho kwa muda mrefu, Hawra Shamte, kiongozi huyo alifafanua kuwa baada ya mgombea urais kutangazwa naye atatambulishwa rasmi. Hata hivyo alisema jina hilo halihusiani na Hawra Shamte ambaye ni mmoja wa wahariri wa gazeti la Mwananchi, jambo ambalo hata Shamte mwenyewe alilikanusha juzi.

Thursday, August 6, 2015

Prof:Ibrahim Lipumba Ang'atuka

Prof. Lipumba akiongea na waandishi wa Habari kwenye Hoteli ya Peacock

Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti kwenye chama chake cha Wananchi CUF.

Ametangaza kuachia ngazi uenyekiti wa chama hicho mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok.
Tazama video Prof: Lipumba akiongea na waandishi wa habari



Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.


Prof Lipumba akitaja sababu za kujiuzulu nafasi ya uenyekiti CUF
Na hizi ni baadhi ya kauli/sentensi alizo zitoa Prof. lipumba kwa waandishi wa habari

Tuesday, August 4, 2015

KUHUSU DK. SLAA KUMKATAA LOWASSA UKWELI NI HUU

slaa 
Kutoka gazeti la uwazi.
NI kweli, ukweli ni huu! Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na kupewa fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho, ukweli wa jambo hilo umeibuliwa,


Edward Lowassa na alipochukua fomu ya kuwania urais kupitia Chadema.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.
ALIANZA DK. SLAA, MBOWE MH!
Mjumbe huyo alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye mtu wa kwanza ndani ya Chadema kutoa wazo na hatimaye kushiriki kikamilifu katika vikao vya kumwezesha Lowassa kujiunga na chama hicho.
“Kwa taarifa yako, Dk. Slaa ndiye aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Taifa Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona jinsi gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk. Slaa yupo.”
MTOA HABARI ASHIRIKI VIKAO
“Mimi ninayekwambia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, nimeshiriki zaidi ya vikao 14 vilivyokuwa vikimjadili Lowassa na vyote hivyo, Dk. Slaa alikuwepo. Huyu jamaa hajakaribishwa kwa utashi wa mtu mmoja kama mnavyosikia huko nje na wala mzee Mtei (Edwin, mwasisi wa chama hicho) hahusiki na chochote,” alisema mjumbe huyo.
WABUNGE WAKOROFI WALIAFIKI
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, ili kuondoa dhana kuwa, Lowassa anapelekwa Chadema na uongozi, wabunge wote ‘wakorofi’ ndani ya chama hicho walikaribishwa kushiriki vikao 14 vya kumjadili ili pia wamuulize maswali na yapate majibu kitu ambacho kilifanyika kwa ufanisi wa hali ya juu.
Aliwataja baadhi ya wabunge hao ‘wakorofi’ na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Godbless Lema (Arusha Mjini), John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Halima Mdee (Kawe), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joshua Nassari (Arumeru), Ezekiel Wenje (Nyamagana),  David Silinde (Mbozi Magharibi) na Highness Kiwia (Ilemela).
“Unajua, kwa vyovyote vile, vikao kama vingefanywa na viongozi wa juu peke yao, hawa wabunge wakorofi wangesumbua sana, lakini wote walishiriki na hakuna ambacho hawakijui. Ndiyo maana wote wamekaa kimya kwa sababu taratibu zote zilifuatwa,” alisema mjumbe huyo.
UKWELI ULIVYO
“Hapa lazima nikueleze ukweli. Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake. Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea tena na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu kilichotokea hakina masilahi kwa familia.
YADAIWA DK. SLAA ALITAKIWA KUCHAGUA MOJA
Mjumbe huyo alikwenda mbali kwa kusema kuwa, wakati wa mchakato wa Dk. Slaa kutaka Lowassa aingie Chadema baada ya kukatwa jina na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma, hakuiambia familia yake mpaka dakika za mwisho, ikajulikana.
“Ndipo familia ikamweka chini na kumwambia achague moja. Aendelee na siasa za Chadema au aachane  na siasa hizo ili  aangalie familia yake kwani kitendo chake cha kuwa mstari wa mbele kumtaka Lowassa kiliashiria kuwa, yeye hatagombea tena urais hivyo kuua matumaini ya familia. Ndiyo maana yupo kimya na hafiki ofisini.”
CHADEMA YAPANGA SAFU YA KUMSHAWISHI
“Sasa dokta ni mtu mzima. Hawezi kuliamua hilo kirahisi kama unavyofikiria. Ni lazima aende nalo taratibu ili kuziridhisha pande zote mbili. Na kwa kutambua hilo, chama kimeunda jopo la watu, wakiwemo mapadri, mashehe na marafiki zake ili wamshawishi arejee Chadema lakini akiiweka familia yake katika kuridhia na kumwelewa,” alisema mjumbe huyo wa Kamati Kuu.
LOWASSA AANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND
Kuhusu madai ya muda mrefu ya chama hicho yanayomtaja Lowassa kuwa ni fisadi, mjumbe huyo alisema kiongozi huyo aliwaeleza kwa ufasaha kuhusu utajiri wake na wakaridhika. Kwa upande wa Richmond, aliwaeleza kuwa alishataka kuuvunja mkataba huo, lakini mamlaka ya juu ikamzuia.
TAASISI TOKA NJE YATUA NCHINI KUTAFITI
Juu ya nafasi yao kushinda urais wakiwa na Lowassa, mjumbe huyo alisema kabla ya kuafiki kumtangaza kugombea, kwa gharama za Chadema, walikodi taasisi ya utafiti kutoka nchini Ujerumani kuja Tanzania ili kufanya utafiti nchi nzima kama Lowassa anakubalika.
Alisema utafiti ulipokamilika, ikaonesha kuwa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika Julai 2015, Lowassa alikuwa mbele ya wagombea wenzake kwa asilimia 65.
SLAA KIMYAAA!
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, Dk. Slaa hajajitokeza kuelezea kilichosababisha ukimya wake huku akiwa hapokei simu ya Uwazi kitu kinachozidisha kwa kasi maneno mitandaoni juu ya hatima yake ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Alhamisi iliyopita gazeti dada na hili, Uwazi Mizengwe linalotoka kila Ijumaa, waandishi wake walishinda nyumbani kwa Dk. Slaa, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar lakini walishindwa kuongea naye licha ya kumpelekea karatasi yenye ujumbe wa kumuomba kuzungumza naye, waliambulia kumuona kwa mbali akiwa ndani ya geti la nyumba yak

Tuesday, July 28, 2015

Breaking News: LOWASSA Atangaza Rasmi Kuhamia CHADEMA.....Asema CCM siyo Baba Yake Wala Mama Yake

Waziri  mkuu wa  zamani  Edward  Lowassa  ametangaza  rasmi  kukihama  chama  cha  mapinduzi, CCM mchana  huu  na  kutangaza  kuhamia  CHADEMA.....

 Lowassa  ametoa  kauli hii Bahari  Beach , Dar akiwa  sambamba  na  viongozi  mbalimbali  wa  UKAWA   ambao  wamekutana  na  waandishi  wa habari  kuzungumzia  hatima  yake  kuelekea  ikulu  pamoja  na  mapungufu  yaliyojitokeza  wakati  wa  mchakato  wa  kumpata  mgombea  urais  wa  CCM.

Lowassa  amesema  baada ya  kutafakari  kwa  kina  na  kujiridhisha, ameamua  kujiondoa  CCM kwa  kuwa  siyo  baba  yake  wala  mama  yake  na  kuitikia  wito  wa  UKAWA  kupitia  CHADEMA.


 Amesema  safari  yake  haitafanikiwa  iwapo  hawatajitokeza  watu  wengi  kupiga  kura na  anaiomba  tume  ya  uchaguzi  iongeze  muda  ili  watu  wote  waweze  kujiandikisha

Lowassa  amesema  alinyimwa  haki  yake  na  CCM  kama  mtanzania  kujieleza  na  kujitetea, hivyo  atakuwa  mnafiki  akisema  anaimani  na  chama  hicho.

 Baada  ya  maelezo  hayo; Mwenyekiti  wa  CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe  alisimama  na  kumkabidhi  rasmi  Lowassa  Kadi  ya  CHADEMA

Monday, July 27, 2015

Maamuzi Rasmi ya ACT Wazalendo Kupitia Kwa Zitto Kabwe Kuhusu Kujiunga na UKAWA

Headlines zimeendelea kwenye mwaka huu wa Uchaguzi 2015 ambapo UKAWA sio jina geni kwa Watanzania, vyama mbalimbali vya upinzani vikiwemo CHADEMA na C.U.F vilijiunga na vinataka kumtangaza mgombea mmoja atakaewawakilisha.

Zitto Kabwe ambaye aliondolewa kwenye chama cha CHADEMA, alijiunga na chama cha A.C.T Wazalendo March 2015 ambapo siku kadhaa baadae chama hicho kilitaka kujiunga na UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) lakini imeshindikana, haya hapa chini ndio maneno ya Zitto Kabwe July 26 2015.

‘Leo siku nzima nilikua nina kikao cha mashauriano na viongozi wa chama wa kata zote za mkoa wa Dar es salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya Dar) jumla ya wajumbe 1023 walihudhuriam, tumesisitiza kuwa hatutajiunga UKAWA… ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya chama ndani ya UKAWA kilitangaza kuwa hawatutaki‘ – Zitto Kabwe

‘Hata juzi kwenye gazeti la Mawio waliandika kuwa tumefukuzwa UKAWA, sisi tumeamua kuingia kwenye uchaguzi wenyewe.. tarehe 10 Agosti 2015 tutatangaza mgombea Urais tutakayemuunga mkono baada ya mkutano mkuu wa kidemokrasia wa ACT Wazalendo.
Tutanadi ‪#‎AzimioLaTabora‬ kama zana ya kuleta mapinduzi katika nchi yetu‘- Zitto

Kwenye sentensi nyingine ya Facebook aliyoandika Zitto Kabwe saa kadhaa kabla ya hiyo ya juu aliandika:

 '‎ACTWazalendo‬ Tutaingia kwenye uchaguzi wenyewe. We will go it alone as a party to defend our principles. Mkutano Mkuu wa Chama wa Kidemokrasia ( National Convention) utafanyika tarehe 10 Agosti 2015′

Sunday, July 26, 2015

Team Lowassa Wazidi Kupigwa Chini Ubunge CCM!

Hadi sasa Pindi Chana, Diana Chilolo, Shamsa Mwangunga na Lediana Mng'ong'o wameshindwa katika kura za maoni viti maalum. Unaweza kuwaongeza pia Nchimbi, Ole Medeye etc etc.

Wiki Ya Mtikisiko: Lowassa na Timu Yake Wasubiriwa kwa Hamu UKAWA.......Zaidi ya Viongozi 950 Wa CCM Kutimkia CHADEMA Wiki hii

Ni wiki ya mtikisiko. Hivi ndiyo unavyoweza kuelezea hali itakavyokuwa nchini kutokana na matukio makubwa ya kisiasa yanayotazamiwa kutokea ndani ya wiki inayoanza leo ambayo yanaweza kubadili mwelekeo wa siasa za Tanzania.
 
Hali hiyo inatokana na vuguvugu la kisiasa linalohusisha viongozi wenye ushawishi kuhama vyama vyao vya siasa na kutimkia kwenye vyama vingine, ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
 
Ni wiki ambayo itapambwa na matokeo ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF kilichofanyika jana mjini Zanzibar kuhusu mustakabali wake ndani ya Ukawa, ikizingatiwa kuwa hivi karibuni chama hicho kiliamua kujiweka kando ya vikao vya umoja huo hadi vikao vya juu viamue.
 
Hata hivyo, habari ambazo tumezipata zinasema kuwa uwezekano wa chama hicho kujitoa ndani ya Ukawa ulikuwa mdogo kutokana na kuogopa hasira za wananchi wenye matumaini na umoja huo.
 
Aidha, kulikuwa na taarifa kuwa kikao cha jana kilikuwa kinaangalia jinsi watakavyoshiriki katika umoja huo na kwamba kulikuwa na matumaini makubwa.
 
Vile vile, hii ni wiki ambayo kura za maoni zinazoendelea katika vyama vikubwa vya siasa, kuonyesha baadhi ya vigogo wakiangushwa na kujaribu kutafuta upenyo wa madaraka katika vyama vingine.
 
Pia, ni wiki ambayo chama kikuu cha upinzani, Chadema kimeamua kusogeza mbele tarehe za kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais kutoka jana hadi Ijumaa, katika kile kinachotazamwa kama kusubiri mchakato wa kumpata mgombea urais.
 
Kana kwamba hiyo haitoshi, hii ni wiki ambayo minong’ono ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye jina lake limekatwa katika orodha ya wasaka urais wa CCM anaweza kuhamia Chadema.
 
Tayari baadhi ya viashiria vya hali hiyo vimeanza kuonekana ambapo wiki iliyopita wabunge wawili wa chama tawala cha CCM, James Lembeli na Ester Bulaya waliachana na chama hicho na kujiunga na Chadema huku chama hicho cha upinzani kikitamba kujiandaa kuwapokea vigogo wengine zaidi.
 
Kiashiria kingine cha mtikisiko ni hatua ya madiwani 18 wa CCM wilayani Monduli na wengine 10 wa UDP na CCM Bariadi kuhamia Chadema.
 
Lakini pia wapo wabunge na madiwani wanaohama Chadema kwenda chama cha ACT-Wazalendo.
 
Vuguvugu hilo la kisiasa limekolezwa na kauli za wanasiasa wawili vijana kwa nyakati tofauti, Godbless Lema na Zitto Kabwe kuwa wiki hii itakuwa ya mshikemshike kutokana na mambo yaliyopangwa kufanyika.
 
Zitto: Ni wiki ya mabadiliko
Akiandika kwenye kurasa zake za Facebook na Twitter jana, Zitto alisema, “Wiki ya kuanzia Jumatatu tarehe 27 Julai 2015 itashuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye siasa za Tanzania. Kuimarika kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni jambo jema kwa nchi yetu.”
 
Alipotakiwa kufafanua kauli yake, Zitto hakutaka kutaja matukio husika, lakini alisisitiza kuwa mtikisiko wa kisiasa utatokea na mazingira ya hali hiyo yataanza kubadilika kuanza kesho.
 
“Na huu ujumbe nilioandika hauna uhusiano na chama cha ACT-Wazalendo,” alisema.
 
Alipotakiwa kufafanua zaidi, alisema “Watanzania wasubiri mabadiliko ya siasa za Tanzania.”
 
Lema asema ni mtikisiko
Kwa upande wake Lema, akiwa jimboni kwake Arusha, alisema wiki hii itakuwa ya mtikisiko kwa CCM kwa sababu zaidi ya viongozi wake 950 kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na taifa watahamia Chadema.
 
Akizungumza wakati wa kuwapokea vigogo watatu na wanachama 30 kutoka CCM jana, Lema alisema kuanzia kesho kimbunga cha viongozi na wana CCM kuhamia Chadema kitavuma kila kona ya nchi.
 
Vigogo hao ni Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Matthysen na mwenyekiti wa CCM Kata ya Terat, Simon Mollel wote wa jijini Arusha.
 
Haya yametokea ikiwa ni siku chache baada ya katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Longido, Tostau Mollel kahamia Chadema, huku baadhi ya watiania wa udiwani na ubunge waliokamilisha maandalizi wakikacha kuchukua fomu za chama hicho.
 
Miongoni mwa waliokacha kuchukua fomu bila kutoa sababu ni mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Robinson Meitinyiku, mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, Mathias Manga na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, wote wakitajwa kuwa kwenye timu ya Lowassa.
 
“Hii iliyoanzia Bariadi, Monduli, Longido na Arusha mjini ni mvua za rasharasha. Masika yataanza wiki ijayo (kuanzia kesho Jumatatu) kwa zaidi ya viongozi 950 wa ngazi mbalimbali watakapohama CCM na kujiunga Chadema,” alisema Lema.
 
Alifananisha Chadema na kanisa au msikiti akisema milango yake iko wazi kuwapokea wanachama wa vyama vingine wanaotaka kutumikia umma kujiunga nacho kwa kutubu makosa yao na kusamehewa kabla ya kuingia kazini Oktoba 25, mwaka huu.
 
Wabunge wanne Chadema watua ACT
Wakati upepo ukivuma kutoka CCM kwenda Chadema, hali kama hiyo imekinufaisha chama kipya cha ACT-Wazalendo baada ya kuvuna wabunge watatu wa viti maalumu na diwani mmoja kwa mpigo kutoka Chadema.
 
Wabunge hao ni Mhonga Ruhwanya (Kigoma), Chiku Abwao (Iringa ) na AnnaMaryStella Mallac (Mpanda) wote kutoka Chadema, huku mwingine ambaye jina lake tunalihifadhi kwa kuwa hatukumpata, akitimkia CCM.
 
Wabunge hao wanaungana na Mbunge wa Kasulu mjini, (NCCR – Mageuzi ) Moses Machali aliyehama kutoka NCCR-Mageuzi kwenda ACT Wazalendo, hivi karibuni.
 
Akizungumza na mwandishi jana, Zitto alisema atawatangaza wakati wowote wabunge wengine sita kutoka CCM, Chadema na CUF.
 
Kauli ya Chiku Abwao
Akizungumza kwa simu akiwa India, Abwao alikiri kuhamia ACT-Wazalendo akidai kutoridhisha na mwenendo wa Chadema na hasa taarifa anazosikia za Lowassa ambaye amekuwa akituhumiwa mambo mbalimbali kuhusishwa na Chadema.
 
“Mimi kwa historia yangu kitu kilichonipeleka upinzani ni kutafuta haki uwajibikaji na kupinga vitendo vya ufisadi na rushwa, lakini nimekishangaa chama changu katika suala hili,” alisema.
 
“ Licha ya mambo ya sintofahamu yanayoendelea Chadema lakini hili la Lowassa kama kweli atajiunga na chama hiki basi suala litakuwa ni moja tu, ni chaneli ya kuingia Ikulu, lakini haya mambo mimi siyapendi kwa sababu ni mtu wa kupinga ufisadi na kupigania haki za wanyonge,” alisema Abwao
 
Alisema ameamua kuhamia ACT-Wazalendo, kwa sababu ni chama pekee kitakachowakomboa Watanzania na kwamba ataenda moja kwa moja kugombea jimbo la Iringa Mjini badala ya Isimani.
 
“Niliamua kwenda Isimani kipindi kile ili kuijenga Chadema, lakini safari hii nipo huku ACT-Wazalendo nitaenda kupambana na Mchungaji (Peter) Msigwa na yeyote yule atakayepitishwa na CCM,” alisema Abwao.
 
Mhonga: Ni uamuzi tu
Mhonga Rhuwanya alipouliwa alijibu kwa kifupi, “Kama ulivyosikia ndiyo hivyo hivyo, mimi ni mtu mzima na nina maamuzi yangu kwani chama siyo dini.”
 
Alipoulizwa atagombea ubunge kupitia ACT-Wazalendo, alijibu, “Kwani mtu akihamia chama kingine ni lazima agombea ubunge… hata hivyo naweza kugombea tena.”
 
Mallac aenda kupokewa
Kwa upande wake, Mallac alisema alikuwa safarini kwenda Katavi kupokewa ACT-Wazalendo.
 
“Niko njiani naelekea Katavi mkoani kwangu kupokewa rasmi na kiongozi wangu wa chama cha ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe,” uliosomeka ujumbe mfupi wa maneno.
 
Zitto awapokea
Zitto alisema huo ni mwendelezo wa chama hicho kuwapokea wabunge kutoka katika vyama mbalimbali na hivi karibuni atawapokea wengine katika mikoa ya Kagera, Tabora, Rukwa na Zanzibar.
 
“Tabora wako wawili na Kagera mbunge mmoja wote wa CCM, kutoka wilaya ya Karagwe, pia Zanzibar wawili kutoka CUF na Chadema. Hawa wote wanasubiri mchakato wa kura za maoni umalizike ndipo tuwatangaze.
 
“Hawa wabunge tuliowapokea ni sawa na asilimia 10 kati ya 50 niliosema, maana watu walikuwa wananiuliza, ‘Zitto ulisema utawapokea wa kiasi kadhaa mbona kimyaa?’ mambo ndiyo yameanza sasa.”
 
Diwani Chadema atua ACT
Katika hatua nyingine, aliyekuwa diwani wa Kata ya Segerea (Chadema), Azuri Mwambagi amejiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ya uhusiano mbaya kati yake na viongozi wa Chadema wa jimbo hilo.
 
Mwambagi alisema kuwa amekuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka mitano lakini hakukuwa na ushirikiano mzuri kati yake na uongozi wa jimbo hilo.
 
“Kila ninachokifanya wenzangu wanasema sijafanya kitu na wanaamua kunizunguka kwa wananchi, hali hii imenichosha,” alisema Mwambagi.
 
Katibu wa jimbo hilo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Anna alisema hata yeye amezisikia taarifa za diwani huyo kuhamia ACT- Wazalendo, lakini akakana kuwapo mizengwe aliyofanyiwa Mwambagi.
 
“Tupo katika mchakato wa kura za maoni na yeye ameomba kuteuliwa kugombea udiwani Kata mpya ya Liwiti, kama anahisi alikuwa kiongozi bora enzi za utawala wake kwa nini asisubiri matokeo ya kura za maoni ndipo afanye uamuzi huo?” alihoji Anna.
 
(Imeandikwa na Bakari Kiango na Peter Saramba-Mwananchi)

Friday, July 24, 2015

ACT-Wazalendo Kuvuna Wabunge Kutoka CCM na CHADEMA

Baada ya vumbi la uchaguzi mkuu kuanza kumtika tumeona kura za maoni zinazoendelea kupigwa kutoka Chadema na CCM kwenye kila jimbo.

Chadema wanachagua wagombea ili baadae watakapokubaliana na wenzao CUF, NCCR Mageuzi, NLD, itabidi baadhi ya Majimbo wapewe vyama hivyo ambavyo vipo kwenye umoja huo UKAWA.

Na hapo ndiyo utazuka mgogoro mkubwa wa baadhi ya wagombea ambao majimbo yao watapewa UKAWA, hapo ndipo ACT-Wazalendo watakapojipatia wagombea wanaokubalika na kuwasimamisha kama wagombea wa ACT-Wazalendo.

Vile wagombea wa CCM ambao watakatwa pia kuna uwezekano mkubwa wakakimbilia ACT-Wazalendo.

Hapo ndiyo kauli ya Zitto kuwa wagombea hamsini watahamia ACT-Wazalendo itatimia.

Huu ndiyo ukweli ingawa unauma kuusoma hii hali kwenye siasa uwa inatumika sana.

Wale wote waliofanyiwa fitna watatumia mbinu hii ambayo imewahi kutumiwa na Dr.W.Slaa wakati yupo CCM kabla ya kutimkia Chadema na kushinda ubunge.

Post Labels