0
Msanii wa muziki nchini, Linex Sunday Mjeda ameweka wazi mpango wake wa kufanya kolabo na staa wa muziki kutoka nchini Uganda, Dr. Jose Chameleone.
linex-na-jose-bongo5
Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Linex amesema tayari ameshamtumia Jose beat kwa ajili ya maandalizi ya wimbo huo mpya.
“Mimi kwa upande wangu nimeshaingiza verse, bado Jose lakini na yeye aliniambia ataingiza Jumatatu hii kwa sababu nilishamtua beat,” alisema Linex. “Kwa hiyo ni kazi ambao itakuja ikikamilika lakini siyo soon, kwa sababu kuna mambo mengi yanakuja kutoka kwangu hivi karibuni,”
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wake kuendelea kusubiria video ya wimbo ‘Hewala’ aliomshirikisha mkali wa masauti Christian Bella.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top