Msanii na mtayarishaji wa muziki wa ‘High Table Sound’ Barnaba
amesema ameshangazwa na mapokezi makubwa ya video yake mpya ya wimbo
‘Lover Boy.
Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Barnaba amesema kwa upande wake video ya ‘Lover Boy’ imekuja kuwathibitishia watu kwamba anaweza kufanya video kubwa.
“Unajua watu walikuwa wanauliza sana kuhusu kufanya video kubwa, nikaona ngoja niwaridhishe na pia kuboresha kazi zangu pamoja na muziki wangu, kwa hiyo hili ni jibu kwa wale ambao walikuwa wanauliza kuhusu video kubwa”alisema Barnaba. Lakini yote kwa yote mapokezi yamekuwa makubwa sana,nawashukuru mashabiki wangu pamoja na wadau kwa kupokea vizuri kazi yangu, sitawaangusha kuna mambo mazuri yakuja,”
Pia muimbaji huyo amesema kufanya video kubwa siyo kufanya na director wa nje kama baadhi ya wasanii wanavyofikiria.
“Wasanii wanatakiwa kujua kufanya video kali siyo lazima ufanye na Godfather au nani, unaweza ukamchukua hata director wa ndani ukaenda naye Afrika Kusini na mkafanya mambo makubwa, unatakiwa kuwa na idea nzuri ya video yako,”
Video ya wimbo ‘Lover Boy’ ‘imeshutiwa’ Tanzania na Afrika Kusini na imeandaliwa na Kwetu Studio chini ya director Msafiri.

Post a Comment Blogger Facebook