Mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Bi. Hillary Clinton, amesema nusu ya wafuasi wa mpinzani wake, Donald Trump ni wahuni.
Akiongea katika hafla ya kuchangisha fedha za kampeni yake, Clinton alisema wengi wa wafuasi wa Trump ni wabaguzi wa rangi, wanaotenga watu kutokana na jinsia zao, mataifa yao na dini zao.
Aliongeza kuwa wafuasi wengine wa mpinzani wake ni watu wanaotaka tu mabadiliko kwa namna yoyote. Trump amedai kuwa kauli hiyo ya Clinton ni tusi kwa mamilioni ya wafuasi wake.
Kwa mujibu kura za maoni zilizotoka wiki hii, Trump anazidi kumsogelea Bi. Clinton.
Post a Comment Blogger Facebook