ume
ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeshtushwa na kauli iliyotolewa na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe, kwamba watasusia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hata
hivyo, Nec imetetea kauli iliyotolewa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
ya Mgombea urais ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, kwamba
CCM haitakubali kuiachia Ikulu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Nec,
Jaji Damian Lubuva, alisema kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi wa chama
kikubwa iliwashtua na kwamba katika vipindi vyote vya uchaguzi
vilivyopita, hawajawahi kukumbana nayo.
Hata hivyo, Jaji Lubuva alisema baada Nec kufuatilia, ilibaini kuwa kilichosemwa na Bulembo, hakiendani na kauli iliyotolewa na Mbowe.
Hata hivyo, Jaji Lubuva alisema baada Nec kufuatilia, ilibaini kuwa kilichosemwa na Bulembo, hakiendani na kauli iliyotolewa na Mbowe.
Jaji
Lubuva alisema kauli iliyotolewa na Mbowe si tu kwamba inashtua,
lakini ni hatari kutolewa katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi
ambacho Watanzania na nchi nyingine, zinaamini kwamba uchaguzi
utafanyika katika hali ya amani na utulivu.
Lakini alisema baada ya kufuatilia, wamebaini kuwa kauli iliyotolewa na Bulembo katika mkutano wa kampeni za CCM mjini Kigoma ilikuwa ni ya kisiasa na si vinginevyo.
Lakini alisema baada ya kufuatilia, wamebaini kuwa kauli iliyotolewa na Bulembo katika mkutano wa kampeni za CCM mjini Kigoma ilikuwa ni ya kisiasa na si vinginevyo.
“Bulembo
katika kauli yake hajasema kwamba hata kama Nec ikitangaza matokeo CCM
wakiwa wameshindwa, hawatakuwa tayari kuwaachia Ikulu Chadema. Alikuwa
anamaanisha kuwa watawashawishi wapiga kura wao wasiwapigie kura ili
wasipate nafasi ya kwenda Ikulu,” alisema.
Alisema kauli iliyotolewa na Mbowe na Bulembo zinakinzana na kwamba baada ya kufuatilia walizinukuu.
Alisema kauli iliyotolewa na Mbowe na Bulembo zinakinzana na kwamba baada ya kufuatilia walizinukuu.
“Kukataa matokeo ya uchaguzi hata kama umeshindwa kihalali ni uhaini,” alisema Jani Lubuva.
“Hii ni kauli ya kisiasa kama ambavyo Chadema nao wamekuwa wakitamka kwamba hii ndiyo awamu ya mwisho kwa CCM kukaa madarakani,” alisema Lubuva.
Kadhalika,
Jaji Lubuva alikemea na kulaani kauli mbalimbali ambazo zimekuwa
zikitolewa na wagombea, viongozi wa vyama vya siasa na makada wake
katika kampeni zinazoendelea kote nchini.
Post a Comment Blogger Facebook