Wakati
zikiwa zimebaki siku 29 kuelekea uchaguzi mkuu, kampeni za mgombea
urais wa chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira zinakabiliwa na uhaba wa
fedha ambazo sasa zimebaki Sh. milioni mbili tu.
Tangu
mgombea huyo alipozindua kampeni zake Agosti 30, mwaka huu hadi sasa,
chama hicho kimeshatumia Sh. milioni 363 ambazo ni wastani wa takribani
Sh. milioni 15 kwa siku.
Lakini kutokana na ukata unaokikabili, kwa sasa kinalazimika kutumia Sh. 66,667 kwa siku.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa ACT-Wazalendo, Nixon Tugara,
juzi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kutokana
na changamoto wanayokabiliana nayo ya uhaba wa fedha anatoa wito kwa
Watanzania popote walipo kuchangia kampeni za chama hicho.
“Mtu
anaweza kutoa kiasi chochote na tutashukuru sana kwa ushirikiano wa
kuijenga Tanzania yenye misingi ya haki...chama chetu kinakabiliwa na
wakati mgumu kifedha, tumekuwa tukijitahidi kuzunguka sana kutafuta
fedha kwa marafiki zetu na kuchangishana miongoni mwa wanachama lakini
hatujafikia lengo letu la kiwango tunachohitaji cha fedha za kufanya
kampeni bora”
Post a Comment Blogger Facebook