Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye,
leo amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Umoja wa Katiba
ya Wananchi (UKAWA).
Sumaye amejiunga rasmi na Ukawa wakati
wa mkutano wa wanahabari na viongozi wa Umoja huo, mkutano uliofanyika
mchana wa leo katika ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar.
Aidha Sumaye hakusema ni chama gani
amejiunga nacho, licha ya kubainisha lengo lake kuu la kuondoka CCM ni
kwenda kuimarisha Ukawa na kuongeza nguvu kwenye vyama vya upinzani hasa
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Post a Comment Blogger Facebook