Mwanafunzi
wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi, Ally Jacob ameuawa baada
kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa
mwanafunzi mwenzake asibakwe.
Tukio
hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri maeneo ya Nyasubi, Wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga. alikuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni.
Kamanda
wa Polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha alidai kuwa mwanafunzi
huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na
mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.
Kamugisha
alisema sababu za Jacob kuuawa ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi
mwenzake mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma
kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na mtuhumiwa ambaye
alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi mmoja wa Nyasubi.
Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Post a Comment Blogger Facebook