Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imetangaza siku ya urejeshaji fomu za Urais na Makamu wa rais kuwa ni Alhamis ijayo.
Aidha, imepiga marufuku maandamano na badala yake watu saba tu ndio wataruhusiwa kusindikiza wagombea.
Taarifa
ya Nec kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Mkurugenzi wa NEC,
Ramadhani Kailima, ilisema urejeshaji fomu utaanza saa 1:30 asubuhi hadi
saa 10:00 jioni.
Alisema
wagombea wote wanatakiwa kufika kwenye ofisi za Tume wakisindikizwa na
watu hao na majina yao yawasilishwe Tume kabla ya Agosti 20, ili
kuratibu kazi hiyo.
"Wagombea
hawaruhusiwi kuja Tume kwa maandamano, shamrashamra, nderemo wala
vifijo. Hii ni kwa sababu siku hiyo vyama vya siasa vitakavyowasilisha
fomu za kuomba uteuzi vitakuwa vingi hivyo kila chama kikija Tume kwa
maandamano na shamrashamra kunaweza kutokea uvujifu wa amani," alisema.
Alisema
sababu nyingine ni kuwawezesha wananchi wengine kuendelea na shughuli
zao na sababu ya tatu ni kuimarisha amani na utulivu na kwamba ni vyem
vyama vikafuata maelekezo hayo.
Post a Comment Blogger Facebook