0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakati wa mkutano wa dharura wa wakuu wan chi za jumuiya hiyo uliofanyika ikulu jijini Dar es salaam leo.
Mkutano wa tatu wa dharura umeitishwa jana  na Mwenyekiti  jumuiya, rais Jakaya Kikwete  kujadili mzozo na mkwamo wa kisiasa nchini Burundi uliosababisha maelfu ya raia kuitoroka nchi hiyo.
Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, ambao tayari wamewasili kwenye kikao hicho, wanajadili na kuwasilisha mapendekezo ya ripoti mbili kuhusu mgogoro wa Burundi.
Ripoti hizo ni pamoja na ya kikosi cha pamoja cha kimataifa cha Usuluhishi wa mgogoro wa Burundi, kinachojumuisha, Umoja wa Afrika, na Umoja wa mataifa, jumuiya hiyo ya Afrika mashariki, pamoja na kikosi cha kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu. Pamoja na ripoti ya baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza hatohudhuria mkutano huo wakati akisubiria matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliofanyika tarehe 29 Juni na badala yake amewakilishwa na mawaziri wa mambo ya nje na wa mambo na ndani pamoja na waziri wa Afrika mashariki na msemaji wa rais.
Viongozi wa Rwanda na Kenya pia hawahudhurii kikao hicho, badala yake wanawakilishwa na mawaziri wa mambo ya nje.

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top