0
Habari nilizopata sasa hivi ni kuwa kuna mpango wa haraka unaandaliwa ili kutengua adhabu iliyotolewa kwa wabunge zaidi ya 35 kutohudhuria vikao vya Bunge.

Sababu hasa ni kuwa inavyoonyesha ni kuwa hata wale ambao hawana hiyo adhabu nao wameamua kususia ili kuwaunga mkono wenzao na jambo hilo litakuwa la aibu sana kwa Bunge na Rais kuhutubia wabunge wa CCM Pekee ilihali nchi inajinadi katika jumuia ya kimataifa kama ya demokrasia ya vyama vingi.

Ikumbukwe pia hotuba ya kuvunja bunge kwa JK itakuwa kama ya kuhitimisha uongozi wake na mahusiano yake na mhimili huu unaowakilisha wananchi.

Kinachoogopwa ni picha gani itajengeka kwa mataifa mengine wahisani ukizingatia kutakuwa na mwaliko wa mabalozi na wawakilishi wa mashirika wahisani.

Nikipata updates au yeyote basi tuziweke ili tuone huu mtanange unaishaje ili kuokoa aibu kwa kiongozi wa nchi.

udakuspecially

Post a Comment Blogger

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
 
Top