Hai. Mwenyekiti wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe amesema kampeni za mwaka huu
zitakazofanywa na umoja huo, hazijawahi kuonekana tangu nchi ipate uhuru
1961.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema,
alisema Ukawa itafanya kampeni kwa kutumia usafiri wa anga na ardhini na
kuongeza kuwa safari hii hakutakuwa na mgombea wa CCM atakayesimama
bila kupingwa na upinzani.
Ukawa unaundwa na vyama
vinne ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF)
na vyote vimekubaliana kuweka mgombea mmoja wa urais, ubunge na udiwani.
Hata
hivyo, hadi sasa umoja huo haujamtangaza atakayewania urais na pia
haujaweka wazi majimbo ambayo wamekubaliana kuachiana ili kusimamisha
mgombea mmoja.
“Tutafanya kampeni, ambazo hazijawahi
kuonekana nchini. Naomba mtembee kifua mbele kwa sababu nina hakika
tunakwenda kuchukua dola kutokana na kampeni za kisayansi tutakazokwenda
kufanya,” alisisitiza Mbowe.
Mbowe alitoa kauli hiyo
juzi wilayani Hai, wakati akiwashukuru wanachama wa Chadema waliomchagua
baada ya kupata kura 269 kati ya kura 274 zilizopigwa katika Jimbo la
Hai.
Mbowe aliionya CCM kutotarajia mteremko na hata zile jitihada zao za kutaka kushinda uchaguzi kwa goli la mkono hazitakubalika.
“Tunaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanya kazi kwa weledi ili uchaguzi uwe wa huru na haki,” alisema na kuongeza:
Mwenyekiti
huyo aliwataka wanachama wanaounda Ukawa na wafuasi wake kujiandaa kwa
ushindi katika Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini wa Chadema, Mchungaji
Israel Natse alisema hawakichukii chama tawala, bali matendo mabaya kama
ufisadi na rushwa yanayofanywa na viongozi wake.
Post a Comment Blogger Facebook